Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Mateta akubali uhamisho wa kujiunga na AC Milan

Chanzo cha picha, Getty Images
Jean-Philippe Mateta amekubali kandarasi na AC Milan hadi 2030, lakini meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner hatamruhusu mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 kuondoka isipokuwa kama watakuwa na mbadala wake aliye tayari. (Times - Subscription)
Mateta anasubiri ruhusa ya kwenda AC Milan kufanyiwa vipimo vya afya, lakini uamuzi wa mwisho kuhusu mkataba wowote ni wa Crystal Palace. (Kaveh Solhekol),
Fulham wamekuwa na ofa ya pauni milioni 20 kwa ajili ya Joe Willock iliyokataliwa na Newcastle United, ambao hawataidhinisha uhamisho wa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26 isipokuwa watampata mbadala wake. (Sportsport)
Iwapo Michael Carrick atabakia kama kocha mkuu wa Manchester United zaidi ya msimu huu, anataka fowadi wa Uingereza Marcus Rashford, 28, arejeshwe kutoka kwa muda wake wa mkopo Barcelona. (Telegraph - Subscription}

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland na Everton zinaonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa chini ya miaka 21 wa Chelsea Tyrique George. Vilabu vya Uhispania, Ufaransa na Italia pia vinamfuatilia. (Sky Sports)
Sunderland wametoa ofa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Wilson Isidor, 25, kwa Napoli. (Calciomercato - In Itali)
Tottenham na Leeds United ni miongoni mwa vilabu vya ligi ya Premier vilivyopewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 22, ambaye yuko kwa mkopo Fenerbahce kutoka Al-Nassr. (TeamTalks)
Liverpool na Chelsea wako kwenye mazungumzo na Rennes ili kumsajili beki wa Ufaransa Jeremy Jacquet, 20, lakini atahama tu msimu wa joto. (Fabrizio Romano),

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanafikiria kumwita mlinzi wa Senegal Mamadou Sarr mwenye umri wa miaka 20 kutoka kwa mkopo katika klabu dada ya Strasbourg. (Sky Sports), nje
Auxerre inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ivory Coast David Datro Fofana, 23. (L'Equipe)












