Vita vya dunia? Kwanini Wahispania wanajenga vyumba vya kujilinda dhidi ya mabomu ya nyuklia?

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVES
- Author, Lucila Runnacles
- Nafasi, BBC News Brazil
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Kama vile nchi za Nordic zilivyofanya hivi karibuni,serikali ya Hispania sasa inaandaa mwongozo wa kutoa ushauri kwa wananchi wake kuhusu jinsi ya kujilinda endapo kutatokea vita.
Mradi huu, ambao bado haujaanzishwa rasmi, ni sehemu ya mkakati wa pili wa kitaifa wa ulinzi wa raia wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Hispania, nyenzo hizi zitakuwa na maelekezo ya jinsi wananchi wanavyopaswa kujiandaa endapo vita vitatokea au wanapokutana na vitu vya kemikali, kibayolojia, nyuklia, au radiamu.
Kutokana na kuongezeka kwa vita na tishio ya mashambulizi ya silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa ,sehemu ya raia wa Hispania wanatafuta kujilinda na kujifadhi iwapo vita kati ya Urusi na Ukraine zitavuka upande wao au iwapo vita vinavyoendelea katika mataifa ya kiarabu kuzidi.
"Tumeona ongezeko la asilimia 90 ya watu kutaka kujengewa hifadhi za siri chini ya ardhi Hispania. Kwa sasa napokea maombi karibu ishirini kwa siku," anasema Fernando Diaz Llorente, Mkurugenzi Mtendaji wa Bunker Vip.
Mjasiriamali huyu anaamini kuwa ongezeko hili linatokana na matukio ya sasa. "Watu wanachukulia mambo kwa uzito zaidi na wanadhani kuwa tishio la vita kuenea ni la kweli."
Makampuni mengine ya Hispania katika sekta hii pia yameona ongezeko hili.
"Mahitaji yetu yameongezeka mara tatu katika miezi ya hivi karibuni. Awali, watu wangeomba kujua kuhusuhifadhi hizo kisha kuchukua muda kutafakari kama wanahitaji au la, lakini leo hii wengi wanapiga simu moja kwa moja kuagiza," anasema Guillermo Ortega, mmiliki wa Bunker World.
Mjasiriamali huyu anafafanua kwamba hifadhi za siri chini ya ardhi kama zile anazozitengeneza, ambazo ni makasha yaliyotengezwa kabla ya kuyaunganisha, hutumia takribani siku 75 kuwa tayari, na kwa sababu ya ongezeko la sasa la mahitaji, tayari ana orodha ya watu wanaosubiri huduma. "Hata naagiza kutoka Ufaransa, wengi kutoka Ujerumani, na hata nimepokea maombi kutoka kwa watu wa Colombia," anasema.

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVES
Kumiliki hifadhi ya siri chini ya ardhi sio jambo rahisi kwa kila mtu,kwasababu kujenga hifadhi chini ya ardhi ni ghali mno.
Katika kampuni ya Bunkers Worlds ,hifadhi ya siri chini ya ardhi yenye ukubwa wa mita za mraba 15 inayoweza kuhifadhi hadi watu sita na ina chumba cha kujisaidia, inagharimu takribani euro 60,000.
Bei hii pia inajumuisha chumba cha kutoa uchafu na mfumo wa ufanisi wa hewa unaondoa gesi hatarishi.
"Hivi sasa tunajenga hifadhi za chini ya ardhi mbili zenye thamani ya euro nusu milioni huko Barcelona. Watu wanajua zaidi kuhusu kutokuwa na utulivu duniani kote. Zaidi ya hayo, jamii haiogopi tu dharura zinazohusiana na vita. Wengine wanataka kujenga hifadhi za chini ya ardhi kujikinga na majanga mengine hatarishi kwa afya ya binadamu," anasema Llorente.
Hifadhi za umma zilizojegwa chini ya ardhi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hispania ina hifadhi zilizojengwa chini ya ardhi za umma chache ukilingaisha na idadi ya watu -kuna tatu mjini Maldrid.
Kubwa lipo katika kambi ya kijeshi ya Torrejón de Ardoz na lina uwezo wa kuhifadhi hadi watu 600.
Katika Hifadhi ya El Capricho, hifadhi iliyo chini ya ardhi iliyojengwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania mwaka 1937, ikiwa na ukubwa wa mita za mraba 2,000 na kina cha mita 15, inaweza kuhifadhi hadi watu 200, lakini sasa imefungwa.
La tatu lipo katika Jumba la Moncloa, makao makuu ya serikali ya Hispania. Hifadi inayojengwa chini ya ardhi ilijengwa ili kustahimili mashambulizi ya nyuklia na kemikali na inaupana wa zaidi ya mita za mraba 7,000.
Katika sekta hii,siku za usoni itakuwa ni uhalisia wale watashndwa kumiliki hifadhi ya kujengwa chini ya ardhi kutokana na gharama au kukosa shamba watakuwa wanaweza kuishi katik ahifadhi zilizojengwa chini ya ardhi za umma.Llorente anasema kampuni yake inajipanga kujenga hifadhi za siri chini ya ardhi za umma ili familia zinaweza kujilinda kwa pamoja kwa wakati mmoja.
"Wazo ni kwamba kundi la watu linaweza kukodisha nafasi na kuwa na ufikivu kwa miaka 25, endapo dharura ya vita itatokea, kwa chumba chenye choo ndani ya hifadhi hiyo ya siri. Gharama ya huduma hii itakuwa takribani euro 40,000," anasema.
Hali ya Hispania ni tofauti sana na ile ya Uswisi.
Nchini Uswisi, aina hii ya ulinzi ni sheria.
Mwaka 1963, Uswisi ilipitisha sera inayowataka wananchi wake wote kuwa na ufikivu kwenye hifadhi za siri chini ya ardhi.
Kwa miaka mingi, hii ilikuwa sehemu ya mkakati wa ulinzi wa raia wa nchi hii ya Ulaya, ambayo sasa ina hifadhi kama hizo za kutosha kuhifadhi hadi watu milioni tisa.
Raia wa Brazil ni watulivu
Wakati baadhi ya Wahispania wanajiandaa kujenga hifadhi za siri chini ya ardhi ili kujilinda, raia wa Brazil wanaoishi Hispania hawaamini kuwa vita vinaweza kufika katika nchi hiyo ya Iberia.
"Kutoka kwa mtazamo wa kijiografia, tunapata hali nyeti sasa. Kuna hofu, kila wakati mimi najiwazia (Rais wa Urusi, Vladimir) Putin akiweka kidole chake juu ya kitufe, karibu kuzindua shambulio la nyuklia, lakini katika maisha ya kila siku, hofu hii haiwezi kujulikana. Tunaendelea kuishi. Hata kama Hispania ingeenda vitani, singeona sababu ya kurudi Brazil kwa sababu mume wangu ni Mhispania. Ikiwa singekuwa na ndoa, ningeweza kufanya hivyo," anasema Alessandra Ribeiro, mwandishi wa habari na mtafsiri kutoka Brazili, ambaye ameishi Madrid kwa miaka nane.

Chanzo cha picha, PERSONAL ARCHIVES
Alexandre Muscalu, mtaalamu wa historia na mwelekezi wa watalii, haamini kwa sasa kuwa vita kati ya Urusi na Ukraine inaweza kupanuka na kufika Hispania.
"Najiuliza zaidi kuhusu usalama wangu wa kiuchumi kuliko usalama wa kibinafsi. Kinachonitia wasiwasi ni kupoteza njia yangu ya kupata kipato hapa ili kulipa gharama zangu. Ikiwa ningeishi Uingereza au Poland, kwa mfano, ningehofia na ningefanya kila kitu kuondoka, lakini sio hapa Hispania," anasema Muscalu, ambaye pia anaishi Madrid.
Simone Henrique Pirani, ambaye ameishi mji mkuu wa Hispania kwa miaka minne, pia anaamini kuwa kanda hii haitaguswa moja kwa moja.
"Mimi ni mmoja wa watu wa matumaini. Nakiri kuwa sijihisi wasiwasi leo. Sidhani kama itafika hapo. Zaidi ya hayo, ninajaribu kuepuka habari zinazojenga hofu. Hata hivyo, ikiwa vita kweli vitafika Hispania au jambo zito litajitokeza, familia yangu na mimi tutarudi Brazil kwa haraka," anasema kwa dhati.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












