Je, vita vikuu vya tatu vya dunia tayari vimeanza?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi, China, Iran na Korea Kaskazini zimeunda mhimili wa kiimla dhidi dhidi ya ulimwengu wa Magharibi, anaandika Wall Street Journal
Muda wa kusoma: Dakika 6

Vita vikuu vya tatu vya Dunia viko karibu kuanza au vinaweza kuwa tayari vimeanza, lakini ubinadamu bado haujatambua, limeandika jarida la Wall Street Journal katika makala yake ya uchambuzi.

Vita vya karibu miaka mitatu nchini Ukraine, migogoro kadhaa katika Mashariki ya Kati, kuongezeka kwa mvutano katika Asia ya Mashariki, na migogoro mingine ambayo wakati mmoja ilichukuliwa kama iliosahaulika imekuwa hatua za kwanza kuelekea Vita vya Dunia vya III, chapisho hilo la Marekani linaandika.

"Hii ni enzi ya mapambano ya kimataifa''.

Vurugu zinazoendelea sasa ulimwenguni zinathibitisha jambo moja: hatuna tena migogoro ambayo inaweza kutofautishwa na ambayo inaweza kutatuliwa kwa tofauti kila mmoja .

Kuna jaribio moja ambalo limekuwa ni la kawaida la kuharibu mamlaka ya kimataifa, na lazima tufanye kila kitu kuzuia hili," Waziri wa mambo ya nje wa Czech Jan Lipavsky alisema hivi karibuni, akitoa maoni kuhusu kuwasili kwa vikosi vya Korea Kaskazini kwenye upande wa Urusi na Ukraine.

Amiri Jeshi Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Ukraine Valeriy Zaluzhny hivi karibuni alizungumzia kuhusu mwanzo wa Vita vikuu vya tatu vya dunia

Unaweza pia kusoma:

Mgawanyiko kuhusu demokrasia na vita vya waamuzi

Kulingana na jarida la Wall Street Journal inavyosema, muongo mmoja uliopita, Urusi na China zilikuwa zikishirikiana na Marekani na washirika wa Magharibi kudhibiti utawala wa Iran na Korea Kaskazini, na pia walipiga kura ya vikwazo dhidi ya nchi hizo.

Hatahivyo, leo Urusi, China, Iran, na Korea Kaskazini wameunda mhimili wa kiimla ambao unashirikiana dhidi ya ulimwengu wa Magharibi, waandishi wa makala hiyo wameelezea na kumnukuu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, ambaye hivi karibuni, kwa mtindo wa George Orwell, aliuita muungano wa "ulimwengu huru."

Hatua ya kugeuka kwa ushirikiano wa karibu kati ya tawala hizi za kiimla ulikuja katika mwaka 2014, wakati nchi za Magharibi zilipojibu uvamizi wa kwanza wa Urusi wa Ukraine kwa vikwazo vidogo tu, kumshawishi Putin juu ya udhaifu wa demokrasia, WSJ inasema.

Makala inaongeza kuwa tayari mwaka 2015, Iran na Urusi zilianza kwa pamoja kuuokoa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria.

Uhusiano kati ya nchi hizo nne umeimarika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022, vita ambavyo Urusi inapigana kwa msaada wa China na vifaa vya silaha kutoka Korea Kaskazini na Iran, chapisho hilo linaeleza.

Inatukumbusha pia kwamba: mwaka jana, Moscow ilipiga kura ya turufu dhidi ya Pyongyang, na baadaye nchi hizo zilitia saini mkataba wa ulinzi wa pamoja.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vladimir Putin na Xi Jinping wakati wa mkutano wa Beijing, Mei 2024

Ushirikiano wa Urusi na Iran pia umekuwa wa kimkakati zaidi: Moscow na Tehran zimeweka makubaliano ya "kuelewa" yanayohusu ushirikiano wa ulinzi.

"Ushindani mkubwa wa mamlaka unaharakisha na kugawanya ulimwengu," alisema Wang Huiyao, rais wa Kituo cha China na Utandawazi.

Alibainisha kuwa dunia iko kwenye ukingo wa Vita viuu vya Tatu vya Dunia. Anataja vita nchini Ukraine, katika Ukanda wa Gaza, na pia anaita matukio nchini Syria "utawala mwingine katika mchezo huu."

"Tunahitaji kuwa makini sana ili kusiwe na utawala kama huo," mtaalamu huyo anabainisha.

Mgawanyiko baina ya nchi za Magharibi na vita vya mawakala

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

WSJ inaita marekebisho ya Moscow na Beijing sababu za mapambano mapya ya kimataifa.

Leo, Urusi na China zina ndoto ya utukufu wa zamani wa kifalme, kutafuta kujenga au kurejesha nyanja zao za ushawishi na kusahihisha kile wanachoona kuwa udhalimu wa kihistoria, kama vile kupoteza Ukraine au Taiwan, waandishi wa makala hiyo wanaonyesha.

China na Urusi zinaamini kuwa "mfumo wa kimataifa unaotegemea sheria" ni chombo tu cha utawala wa kimataifa wa Marekani. Kwahiyo, wanataka kuharibu mfumo huu wa mamlaka ili kuanzisha utawala wao wenyewe.

Wakati huo huo, Moscow na Beijing wanaamini kwamba ushawishi wa kisiasa na kiuchumi wa Magharibi na demokrasia yake huria utapungua kwa kawaida kama sehemu ya demokrasia ya Magharibi katika uchumi wa dunia .

Wakati mataifa ya magharibi yakiratibu mipango ya kupindua mfumo wa mamlaka wa dunia, mataifa ya magharibi yako ukingoni kugawanyika, kama mshindi wa uchaguzi wa Marekani, Donald Trump, tayari ametangaza njia ya kujitenga kiuchumi na kisiasa kwa Marekani.

"Umoja wa vyama vya siasa huenda sasa una nguvu zaidi kuliko umoja wa mataifa yenye demokrasia," anasema Jenerali Onno Eichelsheim, kuu wa jeshi la ulinzi la Uholanzi.

Ni muhimu kwamba miko kadhaa ambayo ilikuwepo wakati wa Vita Baridi imevunjwa hivi karibuni. Kwa mfano, eneo la "nguvu moja ya ulimwengu" sasa linashambuliwa na makombora yaliyotolewa na "nguvu nyingine ya ulimwengu," linaandika WSJ, ikimaanisha makombora ya Marekani ya ATACMS ambayo jeshi la Ukraine hutumia kushambulia eneo la Urusi.

Badala yake, tangu mwaka 2022, Urusi imekuwa ikitumia pesa zake kikamilifu na kufanikiwa kutumia silaha za nyuklia, ikijaribu kuitishia Marekani na washirika wake kuachana na uungaji mkono wao kwa Ukraine.

Aidha, mawakala wa Urusi wamezindua kampeni ya vurugu kote Ulaya, wakishambulia viwanda vya kijeshi na miundombinu ya mawasiliano kwa kiwango ambacho serikali za Magharibi zinaelezea kuwa sio kawaida.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vita nchini Ukraine ni sehemu ya mgogoro wa kimataifa, linaandika WSJ. Katika picha ni athari ya makombora ya Zaporizhia

Kwa haya yote, hali ya sasa haiwezi kuitwa vita vya ulimwengu, WSJ linakili. Licha ya kuongezeka kwa hali hiyo, mataifa makubwa hayana vita moja kwa moja, angalau bado.

"Hivi bado ni vita vya wakala," chapisho hilo linamnukuu seneta wa Republican James Rishi, ambaye anatarajiwa kuongoza kamati ya uhusiano wa kigeni ya seneti ya Marekani mnamo 2025.

Nchi za Magharibi haziko tayari katika vita vikubwa

Mataifa ya Magharibi, kwa mujibu wa chapisho hilo, yalikadiria nguvu na jukumu la kimkakati la ushirikiano kati ya Urusi, China, Iran, na Korea Kaskazini.

Hapo awali, upungufu kama huo ungeweza kusababisha matokeo mabaya, kama ilivyokuwa kwa mataifa ya mrengo wa kulia katika Vita vya Pili vya Dunia.

"Tunaweza kuwa tumepunguza kiwango cha muungano huu mpya na umuhimu wake wa kimkakati kwetu. Tulianguka katika mtego wa kuangalia kila nchi tofauti bila ya uhusiano wao na kusudi la kawaida," WSJ linamnukuu mkuu wa ujasusi wa Australia Andrew Shearer akisema.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya taifa ya mkakati wa ulinzi ya Marekani, China kwa sasa iko mbele ya Marekani katika uzalishaji wa zana za kijeshi, na msingi wa viwanda vya ulinzi wa Marekani hauwezi kukidhi mahitaji ya Marekani yenyewe na washirika wake.

"Huu ni mhimili wa uovu ambao umekuwa ukifanya kazi pamoja kwa muda mrefu," anasema naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine Serhiy Boev. "Sasa muungano huu wa kimataifa unaendelea na uchokozi wake dhidi ya Ukraine. Lakini kuna malengo mengine mengi."

Wachambuzi wanakadiria kuwa kushindwa kwa Ukraine kunaweza kugharimu nchi za Magharibi mara kadhaa zaidi ya msaada wake wa sasa kwa Kyiv.

Katika tukio la ushindi wa Urusi, nchi za Magharibi zitakabiliwa na haja ya kutumia dola bilioni 808 zaidi katika ulinzi katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuliko ilivyotolewa katika bajeti ya sasa.

Ulaya haiko tayari na haijajiandaa

Ukweli ni kwamba Vita Vikuu Vya Tatu Vya Dunia tayari vimeanza, na Ulaya haijajiandaa kwa ajili ya vita, pia ilisemwa na Balozi wa Ukraine nchini Uingereza, aliyekuwa kamanda mkuu wa majeshi ya Ukraine, Valeriy Zaluzhny.

Wakati huo huo, kamanda mkuu wa zamani wa majeshi ya Ukraine anaamini, "katika mwaka 2024 tunaweza kudhani kwa usahihi kabisa kwamba Vita vya Dunia vya III vimeanza," tangu Urusi ilipoanza kutumia askari wa Korea Kaskazini na makombora katika vita dhidi ya Ukraine, makombora ya Shahed ya Iran yanawauwa Waukraine huku "makombora ya Kichina yanalipuliwa Ukraine."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla