‘Hatuonekani katika nchi yetu wenyewe': Kuwa Muislamu katika India ya Modi

sd

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Waislamu milioni 200 wa India ndio walio wachache zaidi katika nchi hiyo yenye watu wengi duniani
    • Author, Soutik Biswas
    • Nafasi, BBC

Miaka sita iliyopita, mvulana Mwislamu alirudi akiwa na uso mwekundu kutoka shule maarufu katika mji wa kaskazini mwa India wa Agra.

"Wanafunzi wenzangu waliniita gaidi wa Pakistan," mtoto wa miaka tisa alimwambia mama yake.

Reema Ahmad, mwandishi na mshauri nasaha, anakumbuka siku hiyo vizuri.

Wakati akiwa darasani baada ya mwalimu kutoka nje. Kundi la moja la wavulana lilimnyooshea kidole na kusema, 'Huyu ni gaidi wa Pakistani. Muueni!

Alifichua kuwa baadhi ya wanafunzi wenzake walimwita mdudu. Bi Ahmad hatimaye alimtoa mwanawe shuleni hapo. Kwa sasa mtoto huyo wa miaka 16 anasoma nyumbani.

"Nilihisi mshituko kupitia uzoefu wa mwanangu, hisia ambayo sikumbuki kuwa nayo katika ujana wangu nikikulia hapa," anasema.

"Kuwepo darasani kulitulinda kama Waislamu. Lakini sasa, inaonekana darasa na fursa inayokufanya kuwa shabaha iliyo wazi zaidi."

Kuna Chuki dhidi ya Waislamu?

XC

Chanzo cha picha, Bimal Thankachan

Maelezo ya picha, Reema Ahmad alimtoa mwanawe kutoka shuleni maarufu baada ya wanafunzi wenzake kumwita 'gaidi wa Pakistani'.

Tangu Waziri Mkuu, Narendra Modi ambaye ni mzalendo wa Kihindu wa chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) alipoingia madarakani mwaka 2014, Waislamu milioni 200 wa India wamekuwa na safari yenye msukosuko.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Makundi ya Wahindu yamewaua washukiwa wa biashara wa ng'ombe na kulenga biashara ndogo ndogo zinazomilikiwa na Waislamu.

Maombi yamewasilishwa dhidi ya misikiti. Mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya wanawake wa Kiislamu. Vikundi vya mrengo wa kulia na baadhi ya vyombo vya habari vya vimechochea chuki dhidi ya Uislamu kwa shutuma za jihad.

Kwa mfano, kuwashutumu kwa uwongo wanaume wa Kiislamu kuwabadilisha dini wanawake wa Kihindu kwa ajili ya ndoa.

Na matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu yameongezeka - robo tatu ya matukio yaliripotiwa kutoka majimbo yanayotawaliwa na chama cha BJP.

"Waislamu wamekuwa raia wa daraja la pili, na hawaonekani katika nchi yao," anasema Ziya Us Salam, mwandishi wa kitabu kipya, Being Muslim in Hindu India.

Bi Ahmad - ambaye familia yake imeishi katika eneo la Agra kwa miongo kadhaa, akiwa na marafiki wengi wa Kihindu katikati mji huu uliojaa nyumba - anahisi kuna mabadiliko.

Mwaka 2019, Bi Ahmad alijitoa katika kikundi cha WhatsApp cha shule ambapo alikuwa mmoja wa Waislamu wawili tu. Hii ilifuatia kutumwa kwa ujumbe baada ya India kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo huko Pakistan yenye Waislamu wengi.

"Ikiwa watatupiga kwa makombora, tutaingia kwenye nyumba zao na kuwaua," ujumbe kwenye kundi hilo ulisema, ukirejelea maneno ambayo Modi alisema kuhusu kuua magaidi na maadui wa India ndani ya nyumba zao.

Nilipoteza uvumilivu. Niliwaambia marafiki zangu mna matatizo gani? Je, mnaunga mkono mauaji ya raia na watoto?" Bi Ahmad alisema. Aliamini katika kutetea amani.

"Mtu fulani aliuliza: Uewe unaiunga mkono Pakistan kwa sababu tu ni Mwislamu? Walinishutumu kuwa na chuki dhidi ya taifa," alisema.

"Ghafla kukata vurugu kukalinganishwa na kupinga taifa. Niliwaambia si lazima nifanye vurugu ili kuunga mkono nchi yangu. Nilijiondoa kwenye kundi."

Mabadiliko yanaonekana kwa njia zingine pia. Kwa muda mrefu, nyumbani pana ya Bi Ahmad pamekuwa ni sehemu ya matembezi kwa wanafunzi wenzake wa mtoto wake, bila kujali jinsia au dini.

Lakini sasa kwa sababu ya msamiati wa hofu wa ‘jihad ya mapenzi,’ hulazimika kuwaomba wasichana wa Kihindu waondoke kwa masaa fulani na wasibaki chumbani kwa mtoto wake.

"Baba yangu na mimi tulimweka chini mwanangu na kumwambia kuwa hali sio nzuri - unapaswa kupunguza urafiki wako, kuwa mwangalifu, usichelewe kukaa nje. Huwezi kujua. Mambo yanaweza kugeuka kuwa 'jihad ya mapenzi’ wakati wowote."

SX

Chanzo cha picha, Bimal Thankachan

Maelezo ya picha, Erum anasema mazungumzo kati ya watoto yalionyesha 'chuki iliokithiri' dhidi ya Waislamu

Mwanaharakati wa mazingira Erum, mkazi wa kizazi cha tano hapo Agra, pia ameona mabadiliko katika mazungumzo kati ya watoto wa jiji hilo alipokuwa akifanya kazi katika shule.

“Usizungumze na mimi, mama ameniambia nisizungumze na wewe,” alisikika mtoto mmoja akimwambia mwanafunzi mwenzake Mwislamu.

"Hii inaonyesha woga uliokita mizizi dhidi ya Waislamu," anasema Bi Erum.

Yeye wenyewe, alikuwa na marafiki wengi wa Kihindu, na alihisi kutokuwa salama kama mwanamke wa Kiislamu.

Katika ofisi yake ndogo kando ya barabara ya Agra yenye shughuli nyingi, Siraj Qureshi, mwandishi wa habari wa ndani na mratibu wa kuyaleta pamoja madhehebu mbalimbali, anaomboleza kuvunjika kwa ucheshi wa zamani kati ya Wahindu na Waislamu.

Anasimulia kisa cha hivi karibuni ambapo mwanaume mmoja aliyekuwa akipeleka kondoo mjini alisimamishwa na kikundi cha mrengo wa kulia wa Kihindu, walimpeleka polisi na kutupwa gerezani.

"Alikuwa na leseni, lakini polisi bado walimkamata. Aliachiliwa baadaye," Qureshi anasema.

Wengi katika jamii wanaona mabadiliko ya tabia miongoni mwa Waislamu wanaosafiri kwa treni, yaliyochochewa na matukio ambapo abiria Waislamu waliripotiwa kushambuliwa kwa madai ya kubeba nyama ya ng'ombe.

"Sasa sote ni waangalifu, tukiepuka vyakula vya vyama katika usafiri wa umma au kuchagua kuachana kabisa na usafiri wa umma ikiwezekana," asema Bi Ahmad.

x

Chanzo cha picha, Bimal Thankachan

Maelezo ya picha, Kaleem Ahmed Qureshi aliulizwa na msafiri mwenzake ikiwa chombo cha muziki alichokuwa amebeba kwenye kesi ilikuwa ni bunduki.

Kaleem Ahmed Qureshi, mhandisi wa programu, aliyegeukia ubunifu wa vito na muziki ni mkaazi wa Agra wa kizazi cha saba.

Akiwa amebeba rubab yake, ala ya muziki inayofanana na inayochezwa kwa kawaida nchini Afghanistan. Hivi karibuni akiwa katika teksi pamoja na abiria mwenza wa Kihindu kutoka Delhi hadi Agra.

"Alipoona chombo hicho, aliniomba niifungue, akihofia ilikuwa bunduki. Nilihisi hisia zake ziliathiriwa na jina langu," Qureshi anasema.

"Kuna wasiwasi huu [ambao tunaishi nao]. Ninaposafiri sasa, ni lazima nielewe mahali nilipo, ninachosema, ninachofanya. Najisikia wasiwasi hata kufichua jina langu kwa mkagua tiketi kwenye treni."

Bwana Qureshi anaona sababu ya jambo hili: "Siasa imechanganya sumu katika uhusiano kati ya jamii."

Majibu ya BJP

sd

Chanzo cha picha, anshul verma

Lakini BJP na Modi wanakanusha kuwa jamii za wachache hunyanyaswa nchini India.

"Hizi ni kauli za kawaida za baadhi ya watu ambao hawajisumbui kukutana na watu nje ya jamii zao. Hata jamii za wachache nchini India hawakubaliani na simulizi hizi tena," waziri mkuu aliambia jarida la Newsweek.

"Hakuna sababu ya Waislamu kuwa na wasiwasi," Syed Zafar Alam, msemaji wa kitaifa wa BJP, anasema, akihusisha kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu.

"Tukio dogo linatokea mahali fulani, na vyombo vya habari vinalikuza kama jambo ambalo haijawahi kutokea. Katika nchi yenye watu bilioni 1.4, matukio kama haya yanaweza kutokea kati ya jamii," anaongeza.

"Huwezi kuchukua tukio moja au mawili na kusema chama tawala kina chuki dhidi ya Waislamu. Kama mtu atalionyesha kama ni jambo linalowalega Waislamu, amekosea."

Nilimuuliza; angejibu nini ikiwa mtoto wake angerudi nyumbani kutoka shuleni, akisema wanafunzi wenzangu walinita "gaidi wa Pakistani" kwa sababu ya dini ya familia hiyo?

Mfanyabiashara huyo wa zamani wa benki, ambaye alijiunga na chama hicho mwaka wa 2014, ana watoto wawili, mmoja yuko shuleni kwa sasa. Anajibu kwa kusema:

"Kama mzazi mwingine yeyote, ningejisikia vibaya. Ni jukumu la shule kuhakikisha mambo kama haya hayatokei. Wazazi wahakikishe hawasemi mambo kama hayo," alisema.

Vipi kuhusu mazungumzo ya BJP kuanzisha jimbo la wa-Hindu jimbo) katika nchi ambayo 79% ya watu ni Wahindu?

"Watu wanajua haya ni maneno tu. Je, serikali au chama chetu kimesema mambo kama hayo? Kwa nini vyombo vya habari vinatoa nafasi nyingi kwa watu wanaosema mambo kama hayo?" Alam anasema.

Lakini vipi kuhusu ukosefu wa uwakilishi wa Waislamu? BJP haina mawaziri Waislamu wala wabunge, na ni mjumbe mmoja tu wa bunge la mtaa (MLA) kati ya zaidi ya wajumbe 1,000 nchini kote.

Islam ambaye alikuwa mbunge wa zamani wa BJP anasema, hii haikuwa ya makusudi.

"Waislamu wanatumiwa na chama cha Congress na vyama vingine vya upinzani kutumikia ajenda zao za kuishinda BJP. Ikiwa mgombea Muislamu atateuliwa na chama na Waislamu wasimpigie kura, ni chama gani kitampa tiketi?"

Ni kweli ni 8% tu ya Waislamu wa India walipigia kura BJP 2019, na wanazidi kupiga kura dhidi ya chama cha Modi. Katika uchaguzi wa jimbo la Bihar wa 2020, 77% waliunga mkono muungano wa kupinga BJP; 2021, 75% waliunga mkono Congress huko West Bengal; na 2022, 79% waliunga mkono chama cha upinzani cha Samajwadi huko Uttar Pradesh.

Alam anasema vyama vya upinzani vinavyoongozwa na Congress vilitia "woga na wasiwasi" katika jamii ili kuhakikisha vinabakia na ushawishi. Serikali ya Modi, kwa upande mwingine, haitofautishi baina ya jamii."

"Mipango ya ustawi wa jamii inawafikia watu wote. Waislamu ndio wanufaika wakubwa wa baadhi ya mipango hiyo. Hakuna ghasia kubwa zilizotokea katika kipindi cha miaka 10 iliyopita."

Kwa kweli ghasia mjini Delhi kuhusu sheria yenye utata ya uraia mwaka 2020 ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 50, wengi wao wakiwa Waislamu.

Bw Alam alilaumu jamii hiyo kwa kujitenga yenyewe.

"Waislamu lazima wajichunguze. Wanapaswa kukataa kuchukuliwa kama wapiga kura kura, na wasishawishiwe na viongozi wa kidini.

"Modi anajaribu sana kuleta jamii pamoja ili watu waishi pamoja kwa furaha na wasipotoshwe."

Nilimuuliza kuhusu jinsi alivyoangalia mustakabali wa Waislamu nchini India chini ya uongozi wa Modi?

"Ni mzuri sana. Akili zinabadilika polepole. Waislamu wengi zaidi watajiunga na BJP. Mambo yanakwenda vizuri."

Mustakbali wa Waislamu India

sd

Chanzo cha picha, AFP

Ni ngumu kusema ikiwa mambo yanaenda sawa au la.

Ni kweli kwamba, katikati ya nyakati hizi za misukosuko, Waislamu wengi wanasema jamii yao inapitia mchakato wa mageuzi.

Vipi kuhusu mustakabali wa Waislamu wa India - ambao pia wamegawanyika katika tabaka, madhehebu, na mistari ya kikanda - katika nchi yenye watu wengi zaidi duniani?

"Watu wanazungumza kuhusu ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei kwa jumuiya ya Kiislamu. Lakini sio tu kuhusu mfumuko wa bei na ajira. Ni kuhusu haki ya kuishi," anasema Salam.

"Karibu kila mtu amechagua nchi ambako angekimbilia wakati ikiwa jambo litatokea. Wengine wamewasiliana na wajomba walioishi Canada, Marekani, Uturuki au Uingereza, ikiwa watahitaji hifadhi.

Hata mtu kama mimi, sasa nina wasiwasi kuhusu mustakabali wa familia yangu katika nchi yangu," anaandika Zeyad Masroor Khan katika kitabu chake cha City on Fire: A Boyhood in Aligarh.

Bi Ahmad pia anahisi wasiwasi wa kutokuwa na uhakika kuhusu siku zijazo.

"Mwanzoni nilidhani chuki dhidi ya Waislamu zingepita. Hiyo ilikuwa miaka 10 iliyopita. Sasa ninahisi mengi yamepotea na kuharibiwa kabisa."