Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Ukraine inaweza kulinda anga yake bila usaidizi wa Marekani?
Kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kutakuwa na athari kubwa zaidi kwa uwezo wa Ukraine wa kutoa ulinzi wa anga, wataalam wana uhakika na hili.
Hii inamaanisha nini na je, kuna uwezekana wa kupata suluhisho?
Kusimamishwa kwa msaada wa Marekani kulijulikana mnamo Machi 4. Utawala wa Ikulu ya White House ulieleza kuwa hatua hii itadumu hadi "Ukraine itakapoonyesha kwamba kweli inaunga mkono mazungumzo ya amani na Urusi."
Huo ndio wakati ambapo Marekani itarejesha msaada wake wa silaha huku ikiibua swali la je kweli, itarejesha ilichokuwa imeanzisha kwa Ukraine.
Wakati huo huo, vikosi vya wanajeshi vya Ukraine vitalazimika kutegemea washirika wa Ulaya na kutafuta akiba ya ndani.
Hata hivyo, hali hili si jambo jipya kwa Ukraine. Serikali hiyo tayari imewahi kujikuta katika hali kama hiyo mara mbili tangu Urusi kuanza uvamizi wake.
Kuanzia mwanzo wa uvamizi hadi mwisho wa mwaka 2022, wakati mifumo ya kwanza ya ulinzi wa anga ya kigeni (IRIS-T wa Ujerumani na NASAMS wa Marekani na Norway) ulifika Ukraine.
Wakati huo huo, Ukraine ilipokea mfumo tata wa makombora wa ulinzi wa Patriot kwanza, ambao uliweza kukabiliana na makombora ya kibalistiki ya Urusi, mnamo mwezi Aprili 2023.
Mara ya pili Ukraine kujikuta bila msaada wa Marekani ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 2024, kwa sababu ya wafuasi wa Trump kuvamia Bunge, misaada ya kijeshi kutoka White House ilisitishwa kwa karibu nusu mwaka.
Athari iliyopo ya "usitishaji" wa sasa wa msaada wa kijeshi kwa Ukraine ni hatari kiasi gani?
Ulinzi wa anga wa Ukraine unajumuisha nini?
Kuelewa hali ilivyo kwa sasa nchini Ukraine ni lazima kwanza kujua ina mifumo gani ya kulinda anga yake yenyewe.
Ili kuweza kupambana na kulenga adui kwenye anga, kuna silaha kama ndege zisizo na rubani na makombora.
Vile vile, vikosi vya ulinzi vinatumia mifumo ya makombora iliyotengenezwa na Sovieti kama S-300, mifumo iliyoboreshwa (FrankenSAM) na mifumo ya Magharibi (NASAMS, IRIS-T, Hawk, Skyguard, Crotale), na kuna mifumo ya kupambana na ndege za kivita inayohamishika, bunduki kubwa ya caliber, na mifumo ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga kama Gepard.
Kama haitoshi, kuna ndege za kivita (pamoja na ndege ya Magharibi F-16 na ndege ya Mirage) na helikopta za kivita zinahusika kikamilifu katika kupambana na mashambulizi ya anga.
Lakini ili kuweza kuharibu makombora ya Kirusi ya balistiki na yenye kulenga anga ya aeroballistic, Ukraine ina betri tano tu za mifumo ya Patriot ya Marekani na mifumo miwili ya Franco-Italia SAMP/T.
Aina hii yote hii ni ya teknolojia ambayo hufanya kazi tofauti.
Baadhi ya mfumo wa ulinzi wa anga, mfumo wa zamani wa Buk ulioboreshwa, ilipewa jina la FrankenSAM, hutumiwa karibu na uwanja wa vita kulinda vikundi vya wanajeshi.
Mifumo ya masafa marefu kama vile NASAMS, Patriot, na SAMP/T hulinda anga katika maeneo fulani ya kimkakati. Ingawa mwanzoni mwa mwaka 2024, Ukraine ilitumia mfumo wa Patriot karibu na uwanja wa vita kwa muda kushambulia ndege za Urusi, waliachana nao baada ya kupoteza vifaa kadhaa vya kurushia makombora.
Kwa vyovyote vile, kuanzia takriban mwisho wa 2022 hadi mwanzoni mwa 2023, Ukraine ilikuwa karibu kabisa kutegemea mifumo ya ulinzi wa anga ya Magharibi, haswa katika suala la vifaa, rada, na makombora ya kupambana na ndege za kivita.
Marekani imeendeleza msaada muhimu kwa Ukraine hasa kwenye makombora ya mifumo ya Patriot na, kwa kiasi fulani, kwa NASAMS.
Maswali kuhusu roketi
"Tatizo kuu ni makombora. Sasa tunalenga kutafuta wapi pa kuyapata na nini kinaweza kuchukua nafasi ya silaha za Marekani. Hili ndilo jukumu kuu," chanzo kikuu katika kambi ya ulinzi na viwanda ya Ukraine kiliiambia BBC.
Ni makombora mangapi ambayo Ikulu ya White House ilitoa kwa Ukraine kwa ajili ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot, hilo halijafichuliwa.
Ingawa, kwa mfano, mwishoni mwa Novemba 2024, vyombo vya habari viliripoti juu ya nia ya Marekani ya kutuma kwa haraka makombora 500 ya kujilinda ya mifumo ya NASAMS na Patriot. Hii inapaswa kuwa iliwawezesha kijilinda hadi kufikia mwisho wa mwaka.
Mamlaka ya Marekani pengine ilipeleka makombora mengine 90 ya Patriot mwishoni mwa Januari mwaka huu. Awali yalikuwa ya Israeli na waliyachukua.
Mbali na Marekani, makombora ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani pia yalipelekwa Ukraine na nchi za Ulaya, lakini kwa idhini ya Marekani.
Uholanzi, Uhispania, na Ujerumani zilitangaza hadharani usafirishaji kama huo. Kwa jumla, nchi 17 ulimwenguni kote zina makombora ya Patriot.
Ni wazi, vikosi vya wanajeshi vya Ukraine bado vina akiba ya makombora ya Magharibi, lakini sio mengi.
Kuweka idadi kubwa ya silaha kama hizo kwenye eneo la Ukraine ni hatari, kwani inaweza kuwa shabaha ya adui, alielezea Yuriy Ignat, msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Anga.
Nini cha kufanya na nini cha kubadilisha
Naibu Mkuu wa Zamani wa Wafanyikazi na Mkuu wa Jeshi la Ukraine kwa Ulinzi wa Anga, Jenerali Ihor Romanenko, ana uhakika kwamba bila usaidizi wa Marekani, uwezo wa jeshi la Ukraine wa kudungua maeneo ya angani "hautaathirika" sana. Ila jambo lingine ni mfumo wa ulinzi wa makombora, ambao ulitegemea msaada wa Marekani.
"Kulenga maeneo ya angani, uwezo utapungua lakini sio kwa kiasi kikubwa. Lakini kwa ulinzi wa kupambana na makombora, yaani, kudungua makombora ya balistiki, hili litakuwa changamoto," alisema mtaalamu kutoka BBC Ukraine. "Utegemezi wa vifaa na makombora ni mkubwa, kwa hivyo, hali ya ulinzi wa makombora kwa Ukraine inaweza kuwa mbaya."
Miongoni mwa mifumo ya ulinzi wa makombora inayofanya kazi nchini Ukraine ni mfumo wa makombora wa ulinzi wa anga wa Franco-Italia SAMP/T.
Betri ya kwanza ilipelekwa Ukraine mwaka 2023, ya pili ilitakiwa kufika katika msimu wa joto wa 2024.
Kwa hakika hakuna taarifa za umma kuhusu ufanisi wa mfumo huu moja kwa moja wakati wa vita nchini Ukraine. Tofauti na mfumo wa Patriot, sio nchi za utengenezaji au mamlaka ya Ukraine, hakuna ambayo imezungumzia utendakazi wa SAMP/T. Baadhi ya waangalizi mwaka 2024 walisema mifumo hiyo bado iko tete.
Hata hivyo, hata kama hitaji na hamu ni kubwa, mifumo hii ya ulinzi wa anga ya Franco-Italia haitaweza kuchukua nafasi ya ile ya Patriot ya Marekani.
Pia kuna matatizo na kasi na kiasi cha utengenezaji wa kombora ya mfumo wa SAMP/T.
Vile vile, kuna kombora la Aster 30, ambalo lina uwezo wa kuharibu maeneo lengwa ya anga katika safu ya zaidi ya kilomita 120, na maeneo lengwa ya makombora ya balistiki ni katika safu ya hadi kilomita 25.
Majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya Aster 30 B1NT yalifanyika tu Oktoba mwaka jana.
Haijulikani ni makombora mangapi ya Aster ambayo Kyiv ilipokea kutoka Ufaransa na Italia, lakini mwishoni mwa 2024, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastian Lecornu alizungumza juu ya kupelekwa kwa kundi jipya la makombora haya. Pia alisema kuwa aliagiza kuharakisha utengenezaji wa makombora mapya.
Ukraine inapaswa kufanya nini katika hali hii?
Makombora machache ya Patriot na SAMP/T yanafaa kutumiwa mahususi kupambana na maeneo lengwa ambayo ni magumu kulindwa kwa mifumo mingine ya ulinzi wa anga.
Haya ni pamoja na makombora ya balistiki ya Iskander, Kn-23 ya Korea Kaskazini, ya hypersonic Kinzhal na Zircon, pamoja na makombora ya cruise Kh-22.
Kulingana na ujasusi wa Ukraine, Urusi inapanga kuongeza uzalishaji wa makombora ya balistiki, pamoja na makombora ya Kh-101, ambayo hutumiwa mara nyingi katika kurusha makombora Ukraine.
Urusi pia inaongeza uzalishaji wa ndege zisizo na rubani kama vile "Shahed" na zinazofanana na hizo. Tayari sasa, mamia ya ndege hizo yanarushwa kila siku katika eneo la Ukraine.
Kulingana na BBC, katika baadhi ya matukio, makombora ya gharama kubwa ya Patriot yalitumiwa hata kuharibu ndege zisizo na rubani za Shahed.
Imefasiriwa na Asha Juma
Imefasiriwa na Asha Juma