Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Real Madrid inamnyatia Micky van de Ven Tottenham
Real Madrid ina nia ya kumsajili beki wa Tottenham Micky van de Ven, 24, lakini Spurs watafikiria kumuuza beki huyo wa Uholanzi kwa takriban £70m. (Fichajes - kwa Kihispania,)
Kiungo wa Manchester United na England Kobbie Mainoo, 20, huenda akafufua tena nia yake ya kujiunga na Napoli kwa mkopo mwezi Januari ikiwa hatapata muda zaidi wa kucheza Old Trafford. (ESPN)
Arsenal itazingatia mauzo ya mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 28, na mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard, 30, katika uhamisho wa Januari. (Football Insider)
West Ham inajadili mpango wa kumsajili tena mlinda lango wa Poland Lukasz Fabianski miezi miwili tu baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 kuondoka katika klabu hiyo mkataba wake ulipoisha. (Sportsport)
Mshambulizi wa Crystal Palace Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 28, hana nia ya kuhamia Leeds United lakini akiamua kufanya hivyo huenda akajiunga na Aston Villa. (Teamtalk)
Klabu za Liverpool na Newcastle zijiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa England na Crystal Palace Adam Wharton, 21, huku Chelsea na Manchester United pia wakiwa miongoni mwa klabu zingine zinazomuwania. (Teamtalk)
Manchester United wanatumai kipa wao Andre Onana atafanya vyema katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki msimu huu ili waweze kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 29 kwa ada kubwa msimu ujao. (Football Insider)
Winga wa Manchester United Muingereza Sam Mather mwenye umri wa miaka 21 huenda akaelekea Uturuki kujiunga na mojawapo wa klabu za huko kabla dirisha la usajili kufungwa. (Manchester Evening News)
Joao Mendes, mtoto wa nguli wa Brazil na Barcelona Ronaldinho, anaondoka Burnley huku winga huyo mwenye umri wa miaka 20 akitarajiwa kujiunga na kikosi cha Hull City cha chini ya miaka 21. (Hull Daily Mail)