Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Liverpool yamzuia Federico Chiesa kuondoka
Liverpool haina nia ya kumuuza Federico Chiesa licha ya kumuacha nje ya kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa. Klabu ya Besiktas ya Uturuki ilikuwa imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Liverpool Echo)
Kipa wa Ujerumani Stefan Ortega, 32, sasa anaweza kusalia Manchester City angalau hadi Januari baada ya Trabzonspor, klabu ya Uturuki ambayo alikuwa ikimfuatilia, kuamua kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Andre Onana mwenye umri wa miaka 29 wa Manchester United badala yake. (Manchester, Evening News)
Arsenal wako mstari wa mbele kumsajili kiungo wa Stuttgart Angelo Stiller baada ya ofa ya dakika za mwisho kutoka kwa Manchester United kukataliwa katika msimu wa kiangazi, lakini Bayern Munich na Real Madrid pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 24. (Express)
Tottenham walifanya uamuzi wa dakika za mwisho wa kumsajili Senny Mayulu wa Paris St-Germain, 19, kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa huku Chelsea na Manchester City pia wakimtaka kiungo huyo wa kati. (Teamtalk)
Real Madrid inajiandaa kumsajili mlinzi wa Ufaransa Dayot Upamecano, 26, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani. (Bild - kwa Kijerumani)
Wolverhampton Wanderers inaamini hakuna masualayoyote yatakayoibuka katika mazungumzo ya kandarasi mpya na Jorgen Strand Larsen, 25, lakini itajumuisha kipengele cha chini cha kuachiliwa kwa mshambuliaji huyo wa Norway baada ya kukataa ofa mbili za zaidi ya pauni milioni 50 kutoka Newcastle msimu wa kiangazi. (Telegraph - usajili unahitajika)
Newcastle, Manchester United na Aston Villa zinamuwania Daniel Vivian wa Athletic Bilbao na huenda wakakutana na kipengele cha kuachiliwa kwa beki huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 26 cha takriban pauni milioni 35 msimu ujao. (Fichajes - kwa Kihispania)
Chelsea bado wanamtaka kipa wa AC Milan Mike Maignan, 30, licha ya kushindwa kuafikiana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa msimu wa kiangazi na wanafurahishwa na fursa ya kumsajili bila malipo mwaka wa 2026. (TBR Football)
Winga wa Lyon na Ubelgiji Malick Fofana, 20, alikuwa akinyatiwa na klabu za Chelsea na Liverpool wakati wa uhamisho wa majira ya kiangazi. (Teamtalk)
Tottenham wanaendelea kumfuatilia mlinzi wa Sunderland Dennis Cirkin na huenda wakahamia kumsajili tena beki huyo wa kushoto wa Uingereza, 23, ambaye ni zao la akademi ya Spurs, mwezi Januari. (TBR Football, nje)
Mchezaji wa Osasuna, Flavien Enzo Boyomo asakwa na vilabu vya Ligi Kuu ya England, na beki huyo wa Cameroon, ambaye ada ya uhamisho wa pauni milioni 22, anaweza kuhama katika dirisha la usajili la Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi