Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 28.11.2022

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lionel Messi

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi, 35, anatazamiwa kufikia makubaliano ya kujiunga na Inter Miami msimu ujao. (Times - subscription required)

Mshambulizi wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24, anafuatiliwa na Manchester United, Newcastle na Arsenal. (Mail)

Manchester United wanatafuta uhamisho wa mkopo kwa Pulisic mwezi Januari. (ESPN)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pulisic

Liverpool wanataka kusajili viungo wawili mwaka ujao huku kandarasi ya wachezaji wao watatu wa kati wakubwa - Waingereza Alex Oxlade-Chamberlain, 29, na James Milner, 36, na rai awa Guinea Naby Keita, 27 - zikikamilika mwishoni mwa msimu. (Football Insider)

Liverpool wamefanya mazungumzo na miungano miwili ya kampuni zenye makao yake Mashariki ya Kati juu ya kuinunua. (MAIL)

Newcastle wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Vasco da Gama Mbrazil Andrey Santos, 18, mwezi Januari. (Northern Echo)

.
Maelezo ya picha, Rio Ferdinand

Rio Ferdinand anasema mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United David Beckham "atakuja na muungano wa makampuni" kuinunua klabu hiyo ya Old Trafford. (FIVE)

Chelsea imekuwa ikimsaka beki wa Ecuador na Bayer Leverkusen Piero Hincapie, 20, kwenye Kombe la Dunia. (Mirror)

Juventus wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 20. (AS - in Spanish)

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Noah Okafor

AC Milan wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uswizi Noah Okafor, 22, kutoka Red Bull Salzburg. (Calciomercato – in Italian)

AC Milan pia wanataka kumnunua kiungo wa Morocco Hakim Ziyech, 29, kwa mkopo kutoka Chelsea, kwa nia ya kuufanya uwe wa kudumu. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Barcelona itampa mkataba mpya wa miaka mitano beki wa kushoto wa Uhispania Alejandro Balde, 19. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, BBC SPORT and Twitter

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Barcelona Alejandro Balde

Inter wanapanga uhamisho wa pauni milioni 20 kumnunua beki wa kushoto wa Fulham na Marekani Antonee Robinson, 25. (Sun)

Leeds itampa mshambuliaji wa Uhispania Mateo Joseph, 19, mkataba mpya mwaka mmoja baada ya kusaini kutoka Espanyol. (Sun)