Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Man Utd inaweza kumzuia Mainoo kuondoka

Kobie MAINO

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Meneja wa Manchester United Ruben Amorim huena akamzuia kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 20 kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari ingawa Napoli imeonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Metro)

Chelsea na Bayern Munich zinaongoza vilabu kadhaa vilivyo mbioni kumsajili Mainoo.

Tottenham iko tayari kusubiri hadi msimu ujao wa kiangazi kumsajili beki wa Brighton wa Uholanzi Jan Paul van Hecke, 25. (Football Insider)

Spurs inataka sana kumuuza mshambuliaji wa Wales Brennan Johnson, 24, baada ya Crystal Palace kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Team Talk)

Barcelona imepunguza kasi ya kumfukuzia mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kujiunga na AC Milan kutoka Juventus badala yake. (Sport - kwa Kihispania)

Real Madrid na Paris St-Germain wanataka kumsajili beki wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano lakini klabu hiyo ya Bundesliga inataka kujadiliana kuhusu mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Bild - kwa Kijerumani)

Igor Thiago

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tottenham, Aston Villa na West Ham zinapigana vikumbo kwa mshambuliaji wa Brentford Mbrazil Igor Thiago

Vilabu vya Tottenham, Aston Villa na West Ham zinapigana vikumbo kuwania saini ya mshambuliaji wa Brentford Mbrazil Igor Thiago, 24. (Caught Offside)

Tottenham wanafikiria kumtema Thomas Frank na kumsajili kocha wa zamani wa Barcelona Xavi. (Fichajes - kwa Kihispania)

Manchester United inapanga kuwasilisha dau la kumsajili kiungo wa Uruguay Manuel Ugarte, 24, mwezi Januari. (Football Insider)

AC Milan iko tayari kuongeza juhudi ya kupata mkataba wa Januari kwa mshambuliaji wa West Ham wa Ujerumani Niclas Fullkrug, 32. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)