Jinsi ya kuishi katika nchi ambayo bei ya bidhaa inapanda kwa karibu asilimia 109 kila mwaka

K

Kwa Yanina, kuishi katika nchi yenye mfumuko mkubwa wa bei sio jambo geni: alipofungua duka lake dogo miaka kumi iliyopita katika kitongoji cha Buenos Aires, mfumuko wa bei wa kila mwaka ulizidi asilimia 25.

Licha ya kwamba bei ya bidhaa iliendelea kuongezeka hadi mara mbili kwa mwaka, watu "walijitahidi" na waliweza kujikimu kimaisha, anasema.

"Kati ya bidhaa kumi walizonunua, nne zilikuwa za msingi," aliiambia BBC Mundo.

Lakini kwa vile bei ilipanda kwa kasi, kuongezeka maradufu ndani ya mwaka mmoja kutoka karibu 50% kwa mwaka hadi 95% mwaka 2022, mwenendo wa ununuzi wa wateja ulibadilika hali ilipokuwa mbaya zaidi mwaka huu - mnamo Aprili takwimu ya mwaka hadi mwaka ilipanda hadi asilimia 108.8.

"Sasa wananunua bidhaa muhimi tu, waliacha kununua bidhaa zingine," alisema.

Mamilioni ya Waargentina hawana hata uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kimsingi. Kulingana na data iliyotolewa mwishoni mwa Machi na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu na Sensa (Indec), Waajentina wanne kati ya kumi ni maskini.

Na hali ni mbaya zaidi miongoni mwa watoto: zaidi ya nusu ya wale walio chini ya umri wa miaka 14 (54.2%) wanaishi katika mazingira ya umaskini, ambao ni sawa na karibu watoto milioni sita.

Wanauchumi wanatarajia kuwa takwimu hii itaendelea kuongezeka mwaka huu kutokana na msukumo mpya ambao umechangia mfumuko wa bei mwezi Machi na Aprili, kufikia asilimia 7.7 na 8.4 kwa mwezi mtawaliwa.

Kiwango hicho ni cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mgogoro wa kiuchumi wa 2001na 2002, ambao ulikuwa mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Kuongezeka kwa bei kuliifanya Argentina kufikia hali mbaya zaidi, kupita Venezuela kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa ya mfumuko wa bei wa kila mwezi (ingawa takwimu ya kila mwaka ya Venezuela bado ni karibu mara tano zaidi ya ile ya Argentina).

Mfumuko wa bei ni jambo ambalo huathiri kwa kiasi kikubwa wale walio na kipato cha chini, kwani bei zinazopanda zaidi ni zile za vyakula, ambazo ni gharama kubwa zaidi kwa familia zinazofanya kazi.

Maelezo
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kando na hilo sekta za kipato cha chini kabisa hazina ulinzi dhidi ya kupanda kwa bei kwa sababu watu hufanya kazi zisizo rasmi, ambazo hazijashughulikiwa na chombo ambacho kimetumika katika miaka ishirini iliyopita kulinda watu dhidi ya mfumuko wa bei: usawa.

Haya ni makubaliano kati ya vyama vya wafanyakazi, makampuni na serikali kuboresha mishahara kwa kuzingatia kupanda kwa bei za bidhaa.

Lakini wale ambao wana kazi ambazo hazijasajiliwa -kulingana na INDEC ni asilimia 35.5 ya nguvu kazi ya Argentina- hawana usawa.

Hata wale waliojiajiri, ambao ni sekta ya uchumi ambayo imekua zaidi katika miaka ya hivi karibuni hawajasazwa.

Kulingana na utafiti wa Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo ya Kazi na Uchumi (Ielde), na data ya INDEC, kazi 8 kati ya 10 mpya zilizobuniwa baada ya janga la corona zilikuwa nafasi za mishahara ambazo hazijasajiliwa au kujiajiri bila taaluma.

Mwaka 2022, makundi yote mawili yaliwakilisha zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya nguvu kazi (yaani, leo ni zaidi ya idadi ya wafanyikazi waliosajiliwa katika uhusiano wa utegemezi).

Una msharara lakini ni maskini

Lakini ukweli ni kwamba kuwa mfanyakazi "pekee" hakuhakikishii ulinzi dhidi ya mfumuko wa bei nchini Argentina pia.

Kwa sababu, ingawa kuna kazi - kiwango cha ukosefu wa ajira ni cha chini, 6.3% kulingana na INDEC - mishahara iko chini.

Kima cha chini cha mshahara mwezi Aprili kilikuwa peso 80,342 kwa mwezi (karibu dola 170 za kimarekani).

Mbali na kuwa mshahara wa chini kabisa katika Amerika ya Kusini, baada ya Mvenezuela, hakuweza kulipia gharama za chini za familia, kwani kikapu cha msingi cha chakula cha Aprili (ambacho ni pamoja na vifaa vinavyohitajika na watu wazima wawili na watoto wawili) kilikuwa peso 191,228, kumaanisha ni zaidi ya kima cha chini cha mishahara miwili.

Na hiyo haijumuishi hata gharama za makazi.

Cinthia, 37, ambaye aliingia katika duka la Yanina kumnunulia mjukuu wake

pipi, aliambia BBC Mundo kwamba ana kazi thabiti kama msimamizi katika hospitali ya uzazi na watoto.

K

Hata hivyo, anadai kuwa alilazimika kwenda kuishi na wazazi wake kwa sababu hakuweza kuendelea kulipa karo ambayo ilikuwa ikiongezeka kutokana na mfumuko wa bei.

"Sikuweza kujikimu kwa mshahara wangu. Na wazazi wangu hawakuweza kujikimu japo walikuwa wakipata malipo ya baada ya kustaafu," anasema.

Hata wakiishi pamoja, hawana tena hela za kutosha kula chakila kizuri siku ya Jumapili, Sasa wanakula nyama choma mara moja kwa mwezi.

Pia hawezi kumnunulia mjukuu wake pipi anayopenda anapotembelea, kwa sababu "bei imepanda mara dufu."

"Siku zote tulikuwa na mfumuko wa bei nchini Argentina, lakini hali imebadilika baada mshahara kuathiriwa na kukosa thamani," anasema. "Sasa hata ukiwa na kazi wewe ni maskini."

Kulingana na shirika la ushauri la Labor Capital Growth (LCG), wafanyakazi waliosajiliwa walipoteza karibu asilimia 20 ya uwezo wao wa kununua bidhaa katika miaka mitano iliyopita na wale ambao wanafanya kazi zisizo rasmi walipoteza karibu mara mbili ya uwezo huo.

Wakati huo huo, uchunguzi wa hivi punde zaidi wa Shirika la Uchunguzi wa Madeni ya Jamii nchini Argentina, uliochapishwa mwishoni mwa 2022 na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Argentina (UCA), ulionyesha kuwa karibu theluthi moja ya wafanyakazi wote ni maskini.

Noti

Chanzo cha picha, BCRA

Katika harakati ya kukabiliana na ongezeko la mfumuko wa bei, Benki Kuu ya Jamhuri ya Argentina (BCRA) ilitangaza kuzindua noti mpya ya peso 2,000, ambayo itakuwa na thamani kubwa zaidi.

Ingawa noti hiyo ilitolewa mwezi Februari, bado haijabainika ni lini itaanza kusambazwa (vyanzo vya habari kutoka Mint vililiambia vyombo vya habari kuwa itapatikana "katikati ya mwaka").

Kwa Waargentina wengi, kama Cynthia, noti hiyo mpya ni pungufu.

"Leo $2,000 ndio kiwango cha chini kabisa unachotakiwa kuuwa nayo ili kununua chochote. Kwa viwango hivi vya mfumuko wa bei wanapaswa kutoa noti $5,000 au $10,000," anasema.

Pia anadokeza kwamba katika hali hizi za bei kupanda kwa kasi ni vigumu kubaini thamani ya vitu unavyonunua.

"Sijui nitalipa pesa ngapi kununu keki hizi. Jana zilikuwa za bei moja na labda leo bei imebadilika," anasema.

Ripoti ya kampuni ya ushauri ya Focus Market kuhusu noti hiyo ambayo kwa sasa ni ya thamani kubwa zaidi nchini Argentina (dola 1,000) ilifichua ni kiasi gani cha uwezo wa kununua ambayo imepoteza tangu ilipoanza kutumika mwezi Novemba 2017.

Kulingana na taarifa thamani yake ni karibu mara 18 kuliko ilivyokuwa wakati ilipozinduliwa. Kumaanisha: kile kilichonunuliwa leo na noti ya dola 1,000 mwaka 2017 kinaweza kupatikana kwa kulipa dola 56.18 tu.