Je, huyu ndiye mnyama mzito zaidi kuwahi kutokea duniani?

Chanzo cha picha, ALBERTO GENNARI
Wanasayansi wamegundua mnyama mzito zaidi kuwahi kutokea kwenye Sayari ya Dunia.
Ni nyangumi wa zamani, aliyetoweka kwa muda mrefu ambaye ana uzani wa karibu tani 200.
Mifupa ya kiumbe huyo ilichimbwa katika jangwa kusini mwa Peru, kwa hiyo imepewa jina Perucetus colossus.
Mabaki yake yanaonesha kuwa aliishi karibu miaka milioni 39 iliyopita.
"Mabaki hayo yaligunduliwa miaka 13 iliyopita, lakini umbo lake ilimaanisha kwamba ilichukua miaka mitatu hadi Lima (mji mkuu wa Peru), ambako yamechunguzwa tangu wakati huo," alisema Dk Eli Amson, -mfanyakazi katika timu ya ugunduzi inayoongozwa na mtaalam wa palaeontologist Dkt Mario Urbina.

Chanzo cha picha, GIOVANNI BIANUCCI
Mifupa kumi na minane ilipatikana kutoka kwa mamalia wa baharini, aina ya zamani ya nyangumi anayejulikana kama basilosaurid. Hizi ni pamoja na vertebrae 13, mbavu nne na sehemu ya mfupa wa nyonga.
Lakini hata kwa kuzingatia vipengele hivi vya vipande na umri wao, wanasayansi bado waliweza kufafanua kiasi kikubwa kuhusu kiumbe hicho.
Hasa, ni dhahiri kwamba mifupa ilikuwa mnene sana, iliyosababishwa na mchakato unaojulikana kama osteosclerosis, ambayo mashimo ya ndani yanajazwa. Mifupa pia ilikuwa na ukubwa mkubwa, kwa maana ilikuwa na ukuaji wa ziada kwenye nyuso zao za nje kitu kinachoitwa pachyostosis.

Chanzo cha picha, GIOVANNI BIANUCCI
Hizi hazikuwa sifa za ugonjwa, timu ilisema, lakini badala yake marekebisho ambayo yangempa nyangumi huyu mkubwa udhibiti muhimu wa kuruka wakati wa kutafuta chakula kwenye maji ya kina kifupi. Vipengele vinavyofanana vya mifupa vinaonekana kwa mfano katika manatee wa kisasa, au ng'ombe wa baharini, ambao pia wanaishi maeneo ya pwani katika sehemu fulani za dunia.
Wanapokabiliwa na mifupa ya spishi iliyotoweka kwa muda mrefu, wanasayansi hutumia mifano kujaribu kuunda upya umbo la mwil.
Wanafanya hivyo kulingana na kile wanachojua kuhusu biolojia ya viumbe hai vinavyofanana.
Inatabiriwa kuwa mnyama huyo angekuwa na urefu wa 17-20m, ambayo sio ya kipekee. Lakini uzito wake wa mifupa pekee ungekuwa mahali fulani kati ya tani 5.3 na 7.6. Na kufikia wakati unapoongeza viungo, misuli na blubber, inaweza kuwa na uzito kulingana na mawazo popote kati ya tani 85 na tani 320.

Chanzo cha picha, R.SALAS-GISMONDI & N.VALENCIA
Dkt. Amson, mtunza kumbukumbu Jumba la Makumbusho ya Jimbo la Ujerumani la Historia ya Asili Stuttgart, anatumia idadi ya wastani ya 180.
Nyangumi wakubwa wa bluu waliorekodiwa wakati wa unyonyaji wa kibiashara walikuwa katika kiwango hiki.
"Tunachopenda kusema ni kwamba Perucetus yuko katika uwanja sawa na nyangumi wa bluu," aliambia BBC News.

Moja ya vilinganishi vilivyotumiwa na timu ya utafiti katika uchunguzi wake ni nyangumi wa bluu ambaye atafahamika sana kwa mtu yeyote ambaye ametembelea Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili huko London.
Kwa jina la utani la Tumaini, mifupa ya mnyama huyu ilijivunia nafasi yake katika taasisi hiyo ilipotundikwa kutoka kwenye dari kwenye jumba kuu mnamo 2017.
Lakini kabla ya kusakinishwa, mifupa ilichanganuliwa na kuelezewa kwa kina na sasa ni rasilimali muhimu ya data kwa wanasayansi kote ulimwenguni.












