Maisha ya Donald Trump katika picha

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump
Muda wa kusoma: Dakika 6

Donald John Trump alizaliwa mwaka 1946 mjini Queens huko New York Marekani.

Ni mwana wa nne kati ya ndugu zake watano, alikuwa na ndugu wawili - Fred Jr na Robert - na ndugu wawili wa kike, Maryanne na Elizabeth. Elizabeth ndiye ndugu yake pekee aliye hai.

Baba yake mzazi Fred aliendesha kampuni ya ujenzi iliyopata ufanisi mkubwa viungani mwa jiji la New York. Alijiunga mara ya kwanza na biashara ya familia yake mwaka 1968, lakini baadaye akaanzisha biashara yake mwenyewe huko Manhattan.

Donald Trump akiwa na baba yake Fred mjini New York

Chanzo cha picha, New York Daily News Archive/Getty Images

Donald Trump akiwa katika ofisi yake iliyopo katika jumba la Trump Plaza mjini Manhattan mwaka 1987.

Chanzo cha picha, Getty Images

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump akipiga picha ndani ya kasino ya Taj Mahal katika Jiji la Atlantic, New Jersey.

Uwekezaji katika biashara za mchezo wa kamari, condominiums, viwanja vya gofu zilifuata katika miji ya Atlantic City , Chicago na Las Vegas hadi India, Uturuki na Ufilipino.

Maisha ya kifahari ya Donald Trump yamemuwezesha kupata umaarufu katika ulimwengu wa biashara mjini New York hasa katika ulingo wa burudani kupitia kipindi cha televisheni cha The Apprentice.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump, aliyevalia shati jekundu na koti jeupe , amesimama katika ukumbi katika jumba lake la kifahari.
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump anasoma gazeti kwenye helikopta yake wakati akipaa juu ya Majumba mawili ya twin Towers huko mjini New York .
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump anayetabasamu, ameketi akiwa ameambatana na mwanawe Donald Trump Jr. na bintiye Ivanka Trump kwa ajili ya fainali ya msimu wa 6 ya The Apprentice.

Trump ameoa mara tatu na amejaaliwa na watoto watano. Alifunga ndoa mara ya kwanza na Ivana Zelníčková mwaka 1977 .

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald na Ivana Trump
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald na Melania Trump walipiga picha kwenye hafla ya Vanity Fair Oscar Party ya 2005 huko Los Angeles, California. Melania alivaa vazi linalometameta naye Trump akivalia vazi la tuxedo.

Trump alimuoa mke wa tatu Melania Knauss mwaka 2005. Walikutana mara ya kwanza alipokuwa na umri wa miaka 52 na yeye akiwa 28.

Safari yake ya kisiasa mwaka 2015 alipotangaza azma yake ya kuwania Ikulu ya White House katika mkutano wa waandishi wa habari katika jumba la Trump Tower akizungukwa na familia yake. Kauli mbiu yake: “Make America great again”.

.

Chanzo cha picha, Bloomberg/Getty Images

Maelezo ya picha, Trump anazungumza kwenye mnara wa Trump huko New York chini ya bendera ya bluu inayosema Make America Great Again. Anatangaza kuwa atawania uteuzi wa urais wa chama cha Republican 2016, huku familia yake ikitazama kando.
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump akionyesha dole gumba kwa umati wakati wa hotuba ya kukubalika kwake katika hafla ya usiku wa uchaguzi huko New York.
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hillary Clinton akishuka jukwaani huku Donald Trump akipiga makofi wakati wa mjadala.

Baada kinyang'anyiro kikali cha kampeni iliyokumbwa na utata, na kumshinda mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton na kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani mwaka 2017.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais mteule Donald Trump akitembea kando ya zulia la bluu linalotazamwa na maelfu ya watu anapowasili kwa sherehe za kuapishwa kwake mjini Washington, DC.
.

Chanzo cha picha, Bloomberg/Getty Images

Maelezo ya picha, Trump akitabasamu ameketi kwenye dawati lake la Oval Office katika Ikulu ya White House mbele ya kamera na wahudumu wa televisheni.

Urais wake ulikumbwa na msukosuko hasa kwa washirika wa Marekani, mara nyingi alilumbana waziwazi na viongozi wa kigeni. Alijiondoa katika mikataba mikuu ya hali ya hewa na biashara na kuanzisha vita vya kibiashara na China.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kansela wa wakati huo wa Ujerumani Angela Merkel akiinamia meza kuzungumza na Donald Trump wakati wa mkutano wa kilele wa G7 mwaka 2018 nchini Canada. Wamezungukwa na viongozi wa dunia akiwemo Theresa May, waziri mkuu wa Uingereza, Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa, Shinzo Abe, waziri mkuu wa Japan, na John Bolton, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani.
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Theresa May, aliyevalia nguo nyekundu, anamshika mkono Trump wakati wanatembea karibu na Ikulu ya White House.

Mwaka wa mwisho wa urais wake ulikabiliwa na ukosoaji mkali kutokana na jinsi alivyoshughulikia janga la Covid. Trump alilazimika kujiondoa katika kampeni ya uchaguzi wa mwaka wa 2020 baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

.

Chanzo cha picha, Bloomberg/Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump, akiwa amevalia koti jeusi, anavua barakao yake ndani ya White House mjini Washington mnamo Oktoba 2020. Bendera nne za Marekani zimesimamishwa nyuma yake.

Trump alishindwa na Joe Biden katika uchaguzi wa urais wa 2020 lakini alikataa kukubali matokeo, kudai kuwa uchaguzi huo ulichakachuliwa. Januari tarehe 6 aliwashinikiza wafuasi wake kuandamana hadi majengo ya Bunge la Marekani jijini Washington.

Maandamano hayo yaligeuaka kuwa ya ghasia na mienendo kuelekea siku hiyo ndio kiini cha kesi mbili za jinai zinazomkabili.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump akiinua kusalimia umati wa watu kwenye mkutano wa Januari 06, 2021, uliofanyika mjini Washington, DC. Mwanachama mmoja anashikilia bango la Trump.
.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mlipuko uliosababishwa na silaha ya afisa wa polisi wang'arisha mbele ya jengo la Capitol hill la Marekani mjini Washington tarehe 6 Januari 2021. Wafuasi wa Trump wamekusanyika hapo.

Wengi walidhani taaluma yake ya siasa imefikia kikomo lakini alitangaza tena azma yake ya kugombea urais katika hatua ambayo ilimuweke kifua mbele miongoni mwa wanachama wengine waliokuwa na nia ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi wa 2024.

Trump alianza kampeni ya kugomea tena urais wa Mareakani akikabiliwa na makosa 91 ya jinai.

.

Chanzo cha picha, Handout/Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump, mwenye koti la buluu na tai nyekundu, anapiga picha kwa ajili ya kuhifadhi katika Gereza la Fulton County mnamo 24 Agosti 2023, Atlanta, Georgia.

Mwezi Mei 2024 alipatikana na makosa 34 yanayohusiana na ulaghai kwa kutoa malipo kwa mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels kuelekea uchaguzi mkuuu wa mwaka 2016.

Aliporejea katika ulingo wa siasa aliponea jaribio la mauaji baada ya kijana wa miaka 20 aliyejihami kwa bunduki kumpiga risasi katika mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania.

.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Trump, akiwa ametapakaa damu usoni mwake, anainua mkono wake wakati akiondoka kwenye jukwaa la kampeni baada ya kupigwa risasi. Amezungukwa na maajenti wa huduma ya siri wa Marekani. Bendera ya Marekani inapepea kwa nyuma.
.

Chanzo cha picha, Bloomberg/Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump anaonyesha dole gumba kwa umati kwenye Kongamano la Kitaifa la Republican huko Milwaukee. Ana bandeji nyeupe kwenye sikio lake la kulia.

Siku kadhaa baadaye aliidhinishwa kuwa mgomea urais wa Republican katika kongamano la kitaifa la chama hicho .

Ushindi wa Trump utamfanya kuwa rais wa Marekani aliye na umri mkubwa zaidi. Atakuwa na miaka 82 kufikia mwisho wa mhula wake madarakani.

.

Chanzo cha picha, The Washington Post/Getty Images

Maelezo ya picha, Donald Trump ameketi kwenye dawati la ofisi yake huko Trump Tower, New York. Dawati limefunikwa na magazeti na karatasi. Dirisha nyuma yake limejaa tuzo, vikombe na picha zilizoandaliwa.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Seif Abdalla