Nini kitaamua uchaguzi wa Marekani na kwanini kuna ushindani mkali sana?

Chanzo cha picha, Getty Images
Anthony Zurcher
Mwandishi wa Amerika ya Kaskazini
Haijatokea kamwe katika historia ya hivi karibuni ya kisiasa za Marekani kwamba matokeo ya urais yamekuwa ya mashaka sana- Huu ni ushindani usio wa kawaida.
Huku uchaguzi uliopita uliamliwa kwa ushindi wa kura chache - ushindi wa George W Bush wa 2000 dhidi ya Al Gore ulikuwa wa kura mia chache huko Florida - kila mara kumekuwa na hisia kuhusu ni mwelekeo gani mbio hizo zilikuwa zikielekea katika siku za mwisho za uchaguzi.
Katika uchaguzi wa mwaka 2016, hisia hazikuwa sahihisi juu ya mgombea anayeweza kushinda . Katika mwaka huo, kura za maoni zilimpatia ushindi Hillary Clinton na kushindwa kugundua harakati za mwisho zilizokuja kuchelewa ambazo zilimuwezesha Donald Trump kushinda.
Wakati huu, hata hivyo, mishale yote inaelekeza katika mwelekeo tofauti. Hakuna mtu anayeweza kufanya utabiri wa ni nani atakayeshinda kwa njia yoyote.
End of Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images
‘Kurusha sarafu juu’
Kura nyingi za maoni za mwisho kuhusu nani anayeweza kushinda ziko katika kiwango cha makosa, kitaifa na katika majimbo saba muhimu ya vmpambano wa kura ambayo yataamua uchaguzi.
Kulingana na takwimu na ukubwa wa sampuli za maoni, hii inamaanisha kuwa mgombea yeyote anaweza kuwa mbele.
Kumekuwa na mshangao wa kushangaza, ambapo uchunguzi wa hivi karibuni wa kuaminiwa wa Iowa ambayo inaongozwa na Republican Harris aliongoza katika uchunguzi huo- mfano wa kushangaza
Lakini kwa wastani mkubwa wa upigaji kura na mifano ya utabiri ambayo inatafsiriwa, vinaonyesha hili kama kurusha sarafu.
Bado kuna uwezekano wa kupata ushindi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa sababu tu matokeo ya uchaguzi huu hayana uhakika, hiyo haimaanishi kuwa matokeo halisi hayatakuwa na maamuzi - mabadiliko ya asilimia chache kwa njia yoyote, na mgombea anaweza kufagia kura za majimbo yote yenye ushindani mkubwa wa kura.
Iwapo utabiri wa wapiga kura unakasoro na wanawake zaidi wanaelekea kwenye uchaguzi, au wakazi zaidi wa vijijini, au wapiga kura vijana zaidi - hiyo inaweza kubadilisha matokeo ya mwisho.
Pia kunaweza kuwa na mshangao kati ya makundi muhimu ya idadi ya watu.
Je, Trump kweli atawavutia vijana weusi na watu wa jamii ya Latino ambao kampeni yake imetabiri? Harris anashinda juu ya idadi kubwa ya wanawake wa jadi wa Republican, kama timu yake inavyotarajia? Je, wapiga kura wazee - ambao wanapiga kura kwa uaminifu kila uchaguzi na huwa wanaegemea upande wa kulia - wakihamia kwenye safu ya Kidemokrasia?
Mara baada ya uchaguzi huu tukitazama taswira ya uchaguzi wa nyuma tutaweza kuelezea kwa ufupi sababu kwa nini mgombea aliyeshinda alijitokeza.
Labda, kwa mtazamo wa juu juu, jibu litakuwa wazi. Lakini mtu yeyote anayesema anajua jinsi mambo yatakavyotokea sasa hivi anakudanganya - na na kujidanganya yeye mwenyewe.
Ukuta wa Bluu na Ukuta Mwekundu
Katika majimbo mengi ya Marekani, matokeo ya kura ya urais ni ya uhakika. Lakini kuna majimbo saba muhimu yyenye ushindani mkubwa wa kura ambayo yataamua uchaguzi huu.
Hata hivyo, si majimbo yote yenye mpambano sawa wa kura. Kila mgombea ana "ukuta" wa majimbo matatu ambayo hutoa njia ya moja kwa moja ya White House.
Ukuta wa Harris unaoitwa "bluu", uliopewa jina la rangi ya Chama Democtrats unaenea katika Pennsylvania, Michigan na Wisconsin katika eneo la Maziwa Makuu. Imekuwa mada ya mazungumzo mengi ya kisiasa tangu 2016, wakati Trump alishinda majimbo yote matatu ya jadi ya democrats wakati wa kuelekea ushindi.
Joe Biden alirudisha majimbo haya mwaka 2020. Ikiwa Harris anaweza kuwashikilia, hahitaji uwanja mwingine wowote wa mapambano, mradi pia atashinda wilaya ya bunge huko Nebraska (ambayo ina mfumo tofauti kidogo katika jinsi unavyotoa kura zake za wawakilishi maalumu wanaopiga wa majimbo wanaopiga kura ya urais).
Hiyo inaelezea ni kwanini ametumia muda wake mwingi katika majimbo haya ya ukuta wa bluu wakati wa kufanya kampeni ya kina, na siku kukampeni kwa siku kamili kwa kila mmoja.
"Ukuta mwekundu" wa Trump uko kando ya mpaka wa mashariki wa Marekani. Huzungumziwa mara chache lakini pia ni muhimu kwa nafasi yake ya uchaguzi. Unaanza katika Pennsylvania lakini unaenea kusini hadi North Carolina na Georgia. Ikiwa atashinda majimbo haya, atakuwa ameshinda kura mbili za wawakilishi wa maalumu wanaopiga wa majimbo wanaopiga kura za urais , bila kujali jinsi uwanja mwingine wa mpapambano ya kura utakavyopiga kura.
Hiyo inaelezea kwa nini alifanya matukio matano huko North Carolina katika wiki iliyopita.
Sehemu inayoingiliana kwenye kila moja ya kuta hizi, bila shaka, ni Pennsylvania - tuzo kubwa la uchaguzi wa uwanja wa vita. Jina lake la utani, huitwa Keystone State [jimbo la jiwe kuu], ushindi wake haujawahi kutabiriwa kwa sahihi.
Mustakabali wa Marekani usiojulikana
Wakati mwingine kupoteza maeneo katika ramani hii yote ya uchaguzi mkakati na mbinu za uchaguzi ni umuhimu wa kihistoria wa uchaguzi huu wa rais.
Harris na Trump wanawakilisha maoni mawili tofauti ya Marekani - kuhusu uhamiaji, biashara, masuala ya kitamaduni na sera za kigeni.
Rais kwa miaka minne ijayo ataweza kuunda serikali ya Marekani - ikiwa ni pamoja na mahakama za shirikisho - kwa njia ambayo inaweza kuwa na athari kwa vizazi.
Hali ya kisiasa nchini Marekani imekuwa ikibadilika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita, ikiakisi mabadiliko katika idadi ya watu ya pande zote mbili.
Chama cha Republican cha muongo mmoja uliopita kinaonekana kuwa tofauti sana na kile ambacho Trump sasa anakiongoza, ambacho kina mvuto zaidi kwa wapiga kura wenye rangi ya bluu na wenye kipato cha chini.
Kambi ya chama cha Democratic bado kinawategemea wapiga kura vijana na watu wa rangi, lakini sasa kinawategemea zaidi matajiri na wasomi wa vyuo vikuu.
Matokeo ya Jumanne yanaweza kutoa ushahidi wa ziada wa jinsi mabadiliko haya katika siasa za Marekani, tu kwa sehemu yaliyogunduliwa katika kipindi cha miaka minane iliyopita, yanabadilisha ramani ya kisiasa ya Marekani.
Na mabadiliko hayo yanaweza kutoa upande mmoja au mwingine faida katika kinyang’anyiro cha uchaguzi baadaye.
Haikuwa muda mrefu uliopita - katika miaka ya 1970 na 1980 - kwamba Warepublican walionekana kuwa na kufuli isiyoweza kuepukika ya urais kwasababu mara kwa mara walishinda kwa wingi wa kura katika majimbo ya kutosha kushinda katika kura za wawakilishi maalumu wanaopiga wa majimbo wanaopiga kura ya urais.
Uchaguzi huu unaweza kuwa wa 50-50, lakini hiyo haimaanishi kuwa hili ni jambo la jipya la kawaida katika siasa za urais wa Marekani.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












