Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maisha ya Donald Trump katika picha
Donald John Trump alizaliwa mwaka 1946 mjini Queens huko New York Marekani.
Ni mwana wa nne kati ya ndugu zake watano, alikuwa na ndugu wawili - Fred Jr na Robert - na ndugu wawili wa kike, Maryanne na Elizabeth. Elizabeth ndiye ndugu yake pekee aliye hai.
Baba yake mzazi Fred aliendesha kampuni ya ujenzi iliyopata ufanisi mkubwa viungani mwa jiji la New York. Alijiunga mara ya kwanza na biashara ya familia yake mwaka 1968, lakini baadaye akaanzisha biashara yake mwenyewe huko Manhattan.
Uwekezaji katika biashara za mchezo wa kamari, condominiums, viwanja vya gofu zilifuata katika miji ya Atlantic City , Chicago na Las Vegas hadi India, Uturuki na Ufilipino.
Maisha ya kifahari ya Donald Trump yamemuwezesha kupata umaarufu katika ulimwengu wa biashara mjini New York hasa katika ulingo wa burudani kupitia kipindi cha televisheni cha The Apprentice.
Trump ameoa mara tatu na amejaaliwa na watoto watano. Alifunga ndoa mara ya kwanza na Ivana Zelníčková mwaka 1977 .
Trump alimuoa mke wa tatu Melania Knauss mwaka 2005. Walikutana mara ya kwanza alipokuwa na umri wa miaka 52 na yeye akiwa 28.
Safari yake ya kisiasa mwaka 2015 alipotangaza azma yake ya kuwania Ikulu ya White House katika mkutano wa waandishi wa habari katika jumba la Trump Tower akizungukwa na familia yake. Kauli mbiu yake: “Make America great again”.
Baada kinyang'anyiro kikali cha kampeni iliyokumbwa na utata, na kumshinda mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton na kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani mwaka 2017.
Urais wake ulikumbwa na msukosuko hasa kwa washirika wa Marekani, mara nyingi alilumbana waziwazi na viongozi wa kigeni. Alijiondoa katika mikataba mikuu ya hali ya hewa na biashara na kuanzisha vita vya kibiashara na China.
Mwaka wa mwisho wa urais wake ulikabiliwa na ukosoaji mkali kutokana na jinsi alivyoshughulikia janga la Covid. Trump alilazimika kujiondoa katika kampeni ya uchaguzi wa mwaka wa 2020 baada ya kuambukizwa virusi vya corona.
Trump alishindwa na Joe Biden katika uchaguzi wa urais wa 2020 lakini alikataa kukubali matokeo, kudai kuwa uchaguzi huo ulichakachuliwa. Januari tarehe 6 aliwashinikiza wafuasi wake kuandamana hadi majengo ya Bunge la Marekani jijini Washington.
Maandamano hayo yaligeuaka kuwa ya ghasia na mienendo kuelekea siku hiyo ndio kiini cha kesi mbili za jinai zinazomkabili.
Wengi walidhani taaluma yake ya siasa imefikia kikomo lakini alitangaza tena azma yake ya kugombea urais katika hatua ambayo ilimuweke kifua mbele miongoni mwa wanachama wengine waliokuwa na nia ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi wa 2024.
Trump alianza kampeni ya kugomea tena urais wa Mareakani akikabiliwa na makosa 91 ya jinai.
Mwezi Mei 2024 alipatikana na makosa 34 yanayohusiana na ulaghai kwa kutoa malipo kwa mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels kuelekea uchaguzi mkuuu wa mwaka 2016.
Aliporejea katika ulingo wa siasa aliponea jaribio la mauaji baada ya kijana wa miaka 20 aliyejihami kwa bunduki kumpiga risasi katika mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania.
Siku kadhaa baadaye aliidhinishwa kuwa mgomea urais wa Republican katika kongamano la kitaifa la chama hicho .
Ushindi wa Trump utamfanya kuwa rais wa Marekani aliye na umri mkubwa zaidi. Atakuwa na miaka 82 kufikia mwisho wa mhula wake madarakani.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi na kuhaririwa na Seif Abdalla