Nyakati tofauti za maisha ya Harris na Trump ambazo huzifahamu

Chanzo cha picha, Alamy
Katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi, wapiga kura nchini Marekani wamekuwa wakikutana na picha za wagombea wawili - wakizungumza kwenye jukwaa, wakisalimiana na umati wa watu na kushuka ngazi za ndege. Huu hapa ni mtazamo tofauti utakaokufahamisha wawili hawa ni nani na wametoka wapi?
Kitambo sana hata kabla hawajaifahamu ikulu ya White House,..Kamala Harris na Donald Trump Kamala Harris na Donald Trump wanapigwa picha wakiwa na umri wa miaka mitatu.
Miongo kadhaa tofauti, Mgombea urais wa Democrats Harris aliishi miaka yake ya awali huko Oakland, California, na huku wa Republican Trump akilelewa katika eneo la Queens huko New York.
Harris (wa kushoto katika picha iliyo upande wa kushoto chini) na dada yake Maya (katikati) waliletwa na mama yao Mhindi, Shyamala Gopalan Harris, mtafiti wa saratani na mwanaharakati wa kijamii.
Babake Trump Fred Trump alikuwa mtoto wa wahamiaji wa Ujerumani na mama yake Mary Anne MacLeod Trump alizaliwa Scotland.
Walimsajili katika Chuo cha Kijeshi cha New York akiwa na umri wa miaka 13.

Chanzo cha picha, Kamala Harris / @realDonaldTrump
Harris alisoma kwa miaka mitano katika shule ya upili huko Montreal, Canada, ambapo mama yake alifanya kazi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha McGill.
Baadaye alijiandikisha katika chuo kikuu cha watu weusi, Chuo Kikuu cha Howard huko Washington DC.
Trump amesema miaka yake mitano katika chuo hicho, iliyoanza mwaka 1959, ilimpa mafunzo ya kijeshi na kumsaidia kupata ujuzi wake wa uongozi.

Chanzo cha picha, Alamy
Tangu akiwa Katika umri mdogo, Harris alifundishwa na mama yake umuhimu wa harakati za haki za kiraia na alihudhuria maandamano ya kila mwaka ya Martin Luther King Jr huko Washington mnamo 2004.
Baada ya kupata digrii kutoka Shule ya Wharton ya Chuo Kikuu cha Pennsylvania, Trump aliteuliwa kumrithi babake katika usimamizi wa biashara ya familia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Harris alirejea California, ambako aliibukia katika mfumo wa haki ya jinai wa jimbo hilo - akifanya kazi kama mwanasheria mkuu - na kutumia nafasi hiyo kushinda kinyang'anyiro cha seneti mnamo 2016.
Wakati huo huo alipoingia kwenye bunge la Congress, Trump alikuwa akiingia Ikulu ya White House kwa mara ya kwanza, baada ya kuushangaza ulimwengu kwa kumshinda Hillary Clinton.
Miaka mitatu baadaye Harris aliendesha kampeni ya urais iliyokosa msisimko, lakini alichaguliwa na mshindi wa Democratic, Joe Biden, na kuwa mgombea mwenza wake.
Walifanikiwa kushinda, dhidi ya Trump na Mike Pence.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tamati ya urais wa Trump na mwanzo wa muhula wa Biden-Harris ukikumbukwa kwa amri ya kutotoka nje ya kipindi cha Covid, masharti y akuvalia barakoa na ghasia za kijamii kufuatia mauaji ya polisi ya George Floyd huko Minneapolis.

Chanzo cha picha, Getty Images
Harris alipambana nyakati Fulani kuacha alama kama makam owa rais,lakini aliipata sauti yake mwaka 2022 wakati mahakama kuu ya Marekani ilipokomesha haki ya kikatiba ya kutoa mimba.
Rais Biden alifurahia,hatua ya makamo wake kuwa mtetezi wa uhuru wa kuchagua.
Wakati wa urais wake, pia aliiondoa Marekani kwenye mkataba wa mabadiliko y atabia nchi ya Paris na kuchukua hatua za kupunguza uhamiaji.

Chanzo cha picha, White House / Getty Images
Ziara ya kwanza ya kimataifa ya Harris kama makamu wa rais ilikuwa Guatemala mnamo 2021, kama sehemu ya jukumu alilopewa kupunguza idadi ya wahamiaji wa Amerika Kusini wanaofika mpaka wa kusini wa Marekani na Mexico.
Masuala ya sera za kigeni ambayo yametawala kipindi chake madarakani ni pamoja na vita vya Ukraine na Gaza, pamoja na ghasia za kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Ziara ya kwanza ya Trump nje ya nchi kama rais ilikuwa Saudi Arabia mwaka wa 2017. Trump akitetea sera za kujitenga ambazo zinahusisha kutenganisha nchi yake na migogoro ya kigeni na kukuza sekta ya viwanda ya Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images / Reuters
Wana familia mbalimbali wa Donald Trump wameshiriki katika kazi yake ya kisiasa, ingawa katika kampeni za 2024,mke wake Melania Trump ameonekana mara chache.
Kwa mke wake wa kwanza, Ivana, Trump wana watoto watatu: Donald Jr (wa pili kushoto katika picha ya chini), Ivanka (wa pili kulia) na Eric (kulia).
Alikuwa na binti, Tiffany (kushoto), akiwa na mke wake wa pili, Marla Maples. Alioa mke wake wa tatu Melania (wa tatu kushoto) mnamo 2005, ambaye alizaa naye mtoto wa kiume, Barron.

Chanzo cha picha, Alamy / AP
Harris aliingia katika kinyang'anyiro cha urais 2024 akiwa amechelewa katika mchakato huo, akichukua nafasi ya Joe Biden aliyejiondoa.
Ameweka historia kuwa mwanamke wa kwanza mweusi,mwenye asili ya Kiasia kuwania urais kwa chama kikuu, na akaendelea kutoa hotuba katika Kongamano la Kitaifa la Democrats huko Chicago, Illinois.
Katika uchaguzi huo huo, Donald Trump alipata sifa adhimu ya kuteuliwa kwa mara ya tatu na chama chake. Alizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Republican huko Milwaukee, Wisconsin - akiwa amefunga sikio lililojeruhiwa katika jaribio la kwanza kati ya mawili ya mauaji wakati wa kampeni zake.
Picha zimehaririwa na Phil Coomes

Chanzo cha picha, Reuters / EPA-EFE
Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Ambia Hirsi












