'Zaidi ya nusu ya Wamarekani wameathirika na upweke'

By Kathryn Armstrong & Bernd Debusmann Jr

BBC News

Loneliness

Chanzo cha picha, Getty Images

Afisa wa ngazi ya juu wa afya nchini Marekani ameonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na janga la upweke ambalo ni hatari kwa afya sawa na kuvuta sigara 15 kwa siku.

Daktari Mkuu wa Upasuaji wa Marekani Vivek Murthy aliiambia BBC News kuwa alikuwa miongoni mwa mamilioni ya Wamarekani ambao wamepitia "hisia kubwa ya upweke".

Mamlaka za afya za Marekani zinataka suala la kutengwa kwa jamii lushughulikiwe kwa uzito mkubwa na sawa kama vile linavyoshughulikiwa suala la unene au matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Takriban Asilimia 50% ya Wamarekani wote wanadaiwa kuathirika na upweke.

Vivek

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vivek Murthy

Bw Murthy alisema katika mahojiano maalumu kwamba vita vyake mwenyewe dhidi ya upweke vilikuja wakati alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kuwa Daktari Mkuu wa Upasuaji na baada ya kukamilika kw amajukumu yake ya kwanza Aprili 2017.

"Nilikuwa nimeiweka kando familia yangu na marafiki zangu wakati huo, nikifikiri kwamba ilikuwa vigumu sana kuzingatia majukumu ya kazi, na wakati huo huo kuwazingatia familia na marafiki," alisema.

"Kwa kweli nilikuwa nikiteseka kutokana na hilo, ambapo ilikuwa ni hisia kubwa za pweke iliyonifuna kila siku, wiki na ikawa miezi."

Upweke unaripotiwa kuongeza hatari ya vifo vya mapema kwa karibu asilimia 30% - kupitia matatizo ya kiafya kama kisukari, mshtuko wa moyo, kukosa usingizi na afya ya akili.

kutojichanganya kijamii pia kunahusishwa na ufanisi mdogo wa kitaaluma na utendaji mbaya zaidi kazini, kwa mujibu wa ushauri mpya.

Bw Murthy alisema kuwa upweke ni "changamoto kubwa ya afya ya umma" ambayo "tunapaswa kuizungumzia" na kushughulikia.

"Inaweza kushangaza watu kujifunza kwamba hatari kubwa ya kifo cha mapema ambayo inahusishwa na uhusiano wa kijamii inalingana na hatari ambazo tunaona kutokana na kuvuta sigara kila siku," alisema.

Vivek

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vivek Murthy
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Suala hilo limechochewa na janga la Covid-19, ambalo lilisababisha watu wengi kupunguza kuchangamana kwenye jamii.

Utafiti mmoja ulionukuliwa katika ripoti hiyo uligundua kuwa kuchangamana kumepungua kwa wastani wa asilimia 16% kati ya Juni 2019 hadi Juni 2020.

Ili kukabiliana na hili, Bw Murthy ametoa wito kwa juhudi za pamoja "kurekebisha mfumo wa kijamii wa taifa letu" ili "kukabiliana na upweke na kubadilisha utamaduni na sera".

Ushauri huo unatoa wito kwa "sera zaidi za kuunganisha umma" ambazo hutengenezwa kwa usaidizi wa ajenda ya utafiti ili kusaidia kushughulikia mapungufu katika taarifa msingi zinazozozunguka athari za kutengwa kwa jamii.

Zaidi ya hayo, Bw Murthy alisema kuwa kuna "hatua tunazoweza kuchukua kama mtu mmoja mmoja", kama vile kutumia dakika 15 kuchangamana na wapendwa wetu, kuepuka vitu vinavyoweza kukutoa kifikra tunapozungumza na watu (mfano simu au kmpyuta), "na kutafuta njia za kusaidiana".

"Huduma ni dawa yenye nguvu dhidi ya upweke," alisema. "Haya yote yanaweza kusaidia".

Mwezi Mei ni mwezi wa Uhamasishaji wa afya ya akili nchini Marekani.

Ingawa tamko hilo linalenga kuongeza ufahamu, hakuna ahadi mpya za kuwekeza ili kukabiliana na suala hilo ambazo zimetolewa kufikia sasa.