Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi na Ukraine: Putin aonya kuhusu silaha za Magharibi za masafa marefu
Urusi itaongeza orodha ya maeneo ambayo itayalenga nchini Ukraine iwapo nchi za Magharibi zitatuma silaha za masafa marefu Kyiv, amesema rais wa urusi Vradimir Putin.
Onyo hili linakuja huku makombora yakiripotiwa kuyatikiza baadhi ya maeneo yam ji mkuu wa Ukraine Kyiv Jumapili, yakiwa ni mshambulio ya kwanza ya anga kufanyika katika mji huo baada ya wiki kadhaa.
Urusi inasema ilipiga vifaru vya kijeshi vilivyotolewa na Muungano wa Ulaya nchini Ukraine. Ukraine inasema kilikuw ani kiwanda cha ukarabati wa leri kilichopigwa.
Katika tukio jingine, Jenerali wa Urusi aliuawa katika mapigano katika jimbo la Donbas.
Urusi imelenga tena juhudi zake za kijeshi katika Donbas mwishoni mwa mwezi machi baada ya kurudi nyuma kutoka Kyiv.
Huku Urusi ikiendelea kusonga mbele kwa mafanikio ya taratibu lakini imara katika vita vyake vya ardhini- nchi kadhaa zimeahidi kutuma silaha za kisasa Kyiv.
Hivi karibuni kabisa , Marekani ilitangaza kuwa itatuma mfumo wa kisasa wa ufyatuzi wa maroketi yanayofahamika kama (HIMARS), wenye unaouwezo wa kufyatua maroketi yanayoongozwa kulenga maeno yaliyobainishwa , na yanayoweza kulenga hadi umbali wa kilomita 70 au (maili 45) - mbali kuliko kule yanakoweza kufika makombora ya ambayo Ukraine inayo kwa sasa.
Maafisa wa Ikulu ya White House nchini Mareknai wanasema kuwa wamekubali kutoa makombora hayo tu baada ya kupata hakikikisho kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky kwamba hayatatumiwa kulenga maeneo yaliyopo ndani ya Urusi.
Msaada huo wa silaha pia unajumuisha helikopta, silaha za kujikinga na mashambulio, magari ya mkakati na vipuli.
Ujerumani pia imeahidi kutuma mfumo wake wa kisasa zaidi wa anga - unaojulikana kama -Iris-T - ili kuiwezesha Ukraine kuukinga mji wote wa Kyiv dhidi ya mashambalio ya anga ya Urusi.
Katika mahojiano na televisheni ya taifa ya Urusi, Bw Putin amesema : "Kwa ujumla yote haya ni kuonyesha wasi wasi usio na sababu kuhusu siilaha za ziada kwa Ukraine, kwa maoni yangu, hili lina lengo moja- kuzorotesha mzozo wa silaha kuufanya uwe mrefu sana iwezekanavyo."
Kiongozi huyo wa Urusi alisema kwamba kile ambacho Marekani ilikuwa inakipeleka Ukraine "hakina jipya " lolote.
Lakini alionya dhidi ya kutuma makombora ya masafa marefu: "iwapo yanapelekwa , basi tutakuwa na msimamo wetu juu ya hili na kutumia silaha zetu, ambazo tunazo za kutosha, kufanya mashambulio katika maeneo hayo ambayo bado hatujayashambulia ."
Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine alizitaka nchi za Magharibi kuendelea kuimarisha usambazaji wa silaha kwa nchi yake ili kuisaidia kuishinda Urusi
"Tayari tumeingia katika vita vya muda mrefuna tutahitaji msaada wakati wote. Nchi za Magharibi lazima zielewe kwamba msaada wake hauwezi kuwa kitu cha wakati mmoja, bali kitu ambacho kinaendelea hadi tupate ushindi ," Hanna Malyar aliviambia vyombo vya habari vya Ukraine.
Mapigano makali yanaendelea kwa sasa mashariki mwa mji wa Severodonetsk. Kuchukuliwa kwa mji huu kutawezesha jimbo la Luhansk kutwaliwa na vikosi vya Urusi na washirika wake wanaotaka kujitenga na Ukraine, ambao pia wanadhibiti maeneo mengi ya jimbo jirani la Donetsk. Majimbo haya mawili yanaunda jimbo lenye viwanda vingi la Donbas.
Gavana wa Luhansk Serhiy Haidai alisema kuwa vikosi vya Ukraine vinashikilia takriban nusu ya mji wa Severodonetsk, baada ya kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi.
Alisema kuwa watu 15,000 walibakia katika mji huo, lakini ''uokoaji wa watu kwa sasa hauwezekani ".
Rais Volodymyr Zelensky amesema kuwa alitembelea katika Lyshchansk, mji ulio mkabala na Severodonetsk unapovuka mto Donets , Jumapili kama sehemu ya ziara mpya inayolenga kuyazuru maeneo ya vita ambayo pia alitembelea eneo la Zaporizhzhia lililopo kusini mwa nchi.
"Ninajivunia kila mtu niliyekutana naye, kila mtu niliyemsalimia kwa mikono yangu, kila yeyote niliyezungumza nayena wameelezea kuniunga mkono," alisema katika video iliyotolewa na huduma yake ya mawasiliano.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine