Katika Picha: Nguzo za asili zilizogeuka kuwa kivutio cha utalii Tanzania

Maelezo ya video, Zana za mawe katika nguzo za asili
    • Author, Esther Namuhisa & Eagan Salla
    • Nafasi, BBC Swahili

Zipo simulizi nyingi za kusadikia katika maeneo mbalimbali duniani, kwa misingi ya imani na mila za jamii.

Isimila Natura Pillars ni eneo maarufu la kihistoria katika nyanda za juu kusini mkoani Iringa nchini Tanzania ambapo katika eneo hili kuna dhana kwamba ni makazi ya watu wa kale.

Huku, Miamba ya asili iliyosimama kama nguzo kutokana na athari ya mmomonyoko wa udongo na upepo, imekuwa kivutio kikubwa nchini Tanzania.

Nguzo zenye miundo ya kustaajabisha iliyojitengeneza kiasilia imekuwa miongoni mwa vivutio.

Wakati maeneo mengine nguzo huwa inajengwa kwa matofali lakini Isimila, nguzo zinajitengeneza kiasili.

n

Isimila maana yake ikiwa eneo la kudumu, inabeba historia ya binadamu aliyeishi zama za kale na kuzindua matumizi ya zana za mawe.Kadri siku hatimaye miaka inavyosonga mbele, kuna mabadiliko mbalimbali ya kijiografia ama yanayotokana na mifumo ya maisha ambayo huathiri uwepo wa nguzo hizi kwa pande mbili.

n

Upepo au mmomonyoko unaweza kuathiri nguzo kuanguka lakini pia inaweza kuunda mitindo ya kuvutia.

Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa.

Wageni kutoka nje na ndani ya nchi ufika hapa kwa ajili ya utalii.

Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu enzi za Zama za Mawe za Kale. Na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa tangu mwaka 1951.

m

Mbali ya kuwa na vivutio vya nguzo kubwa za asili, eneo hili pia ni hifadhi ya zana za asili za mawe…

Isamila inabeba historia ya binadamu aliyeishi enzi hizo na alifahamika kutumia teknolojia ya zana za mawe, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali.

Hifadhi inatajwa kuwa karakana ya kutengeneza zana za asili za mawe.

Teknolojia hii inatajwa kuwa ilikuwa inakuwa kidogo kidogo na ilikuwa inatumika kulingana na mazingira yao.

Zana hizo za binadamu aliyeishi miaka takribani 3000 iliyopita alitumia zana hizo katika uwindaji, kukata matunda na kujilinda na wanyama,

m
Maelezo ya picha, Haya si mawe ya kawaida bali zana za mawe zilizokuwa zikitumika zama za kale

Simulizi kuhusu zana za mawe zimebaki kuwa historia nichini Tanzania na hata duniani kote wakati watafiti wakija na ugunduzi mpya kila kukicha.Lakini bado huenda kuna vitu vingine vya kale,ama maeneo yanayoaminika kuwa na historia za kipekee hayajafikiwa na kutangazwa vya kutosha.

Licha ya zana za mawe, eneo hili lina simulizi kuhusu ziwa lililokuepo eneo hilo na wanyama wenye muonekano tofauti waliokuepo enzi hizo, mfano inasadikika kuwa eneo hilo lilikuwa na 'Twiga mwenye shingo fupi.'

b