Tazama visu na shoka za mawe katikati ya nguzo za asili
Zipo simulizi nyingi za kusadikia katika maeneo mbalimbali duniani,kwa misingi ya imani na mila za jamii.
Isamila ni eneo maarufu la kihistoria ,nyanda za juu kusini mkoani Iringa nchini Tanzania ambapo kuna dhana kwamba yalikuwa makazi ya watu wa kale.
Licha ya simulizi hizi ambazo bado katika eneo hilo la Isimila kuna zana za kale,kama vile nguzo za asili, zilizogeuka kivutio kwa watalii na baadhi ya watu ambao hufika katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC, Esther Namuhisa alisafiri mpaka katika eneo hilo na kuzungumza na mkuu wa hifadhi hiyo Natalia Mamseri kuhusu eneo hilo; Video Eagan Salla