Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Mtanzania, aliyeshinda Tuzo ya Nobel, Abdulrazak Gurnah hafahamiki sana nyumbani
- Author, Priya Sippy
- Nafasi, Journalist
Abdulrazak Gurnah mzaliwa wa Zanzibar amekuwa mwandishi anayezungumziwa zaidi duniani baada ya kushinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka huu, lakini hafahamiki sana nchini Tanzania.
Mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 72 amepata sifa kwa msingi wa uandishi bora wa Kiafrika, lakini katika maduka ya vitabu vya taifa hilo la Afrika Mashariki, riwaya za Gurnah hazipatikani popote.
"Ukionesha picha yake hapa, watu wengi watakuwa wanamuona kwa mara ya kwanza," anasema Ally Saleh, mwandishi na mshairi kutoka visiwani Zanzibar, ambako Gurnah alikulia.
"Asilimia ndogo sana ya watanzania watakuwa wanafahamu kuhusu kazi zake."
Ingawa vitabu vya Gurnah kimsingi vimeuzwa nchini Uingereza, ambako ameishi kwa miongo mitano iliyopita, ingawa riwaya zake 10 zimechambua kwa ukaribu masuala ya Wazanzibari.
Anachunguza athari za ukoloni katika utambulisho wa Afrika Mashariki, na uzoefu wa wakimbizi wanapolazimika kutafuta makazi kwingine.
Gurnah mwenyewe aliondoka nchini kwake akiwa na umri wa miaka 18 - akikimbia ghasia zilizotokana na mapinduzi ya mwaka 1964 ambayo yalipindua Waarabu wachache waliokuwa wakitawala Zanzibar.
Baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuanzisha Tanzania. Mwandishi alibaki kuwa na uhusiano mkubwa na kisiwa hicho, ambacho kimekuwa msingi wa hadithi zake nyingi.
"Ni muhimu kwa Watanzania kusoma kazi za Abdulrazak. Anaangazia mambo mengi ya uhalisia wa kuwa Mtanzania ndani na nje ya nchi," anasema Mkuki Bgoya, mkurugenzi wa kampuni ya kuchapisha vitabu nchini Tanzania Mkuki na Nyota.
"Mara nyingi kama Waafrika Mashariki, tunaona ulimwengu kupitia macho ya watu wengine. Lakini kwa Gurnah, tunaweza pia kujiona wenyewe."
Walimu waliondoka
Tangu atangazwe kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel mwezi Oktoba,baadhi ya Watanzania wamebaki wakijiuliza mtunzi huyu Gurnah' ni nani?
Kumekuwa na mjadala kuhusu taifa hilo kutokutowa na tamaduni ya kusoma.
Baada ya mapinduzi ya Zanzibar , utawala mpya ulibadilisha mtaala wa elimu na kupunguza kuhamasisha fasihi.
Kwa sasa hakuna vyuo vyuo vikuu vitatu kisiwani Zanzibar vinavyofundisha fasihi kwa kutoa shahada.
"Kufuatia mapinduzi , serikali ilifunga klabu kadhaa za vitabu na maktaba.Walimu wengi wazuri waliondoka nchini humo," anasema Ismail Jussa, mwanasiasa wa upinzani kisiwani Zanzibar.
"Elimu ilikuwa inatolewa kwa usawa na hivyo kusababisha viwango kushuka ,utamaduni wa kusoma ukabaki kwa wale wengi walioathirika na mapinduzi."
Kwa upande wa Tanzania bara, hali iko hivyo hivyo , kumekuwa na kushuka kwa kasi kwa upatikanaji wa kazi za fasihi.
Kwa miaka mingi, maktaba za Tanzania, shule na maduka ya vitabu yamelenga kwenye vitabu ambavyo vinafundishiwa darasani kwa mujibu wa mitaala na kufanya upatikanaji wa vitabu vya simulizi kuwa mdogo.
Wakati hadithi zisizo na simulizi za kusadikika na magazeti kubaki kuwa na umaarufu mkubwa kwa wasomaji, ingawa kukua kwa teknolojia kumeweza kulenga kile ambacho vijana wanapenda katika mitandao ya kijamii.
Matokeo yake, Tanzania imewaacha wachapishaji wa vitabu wakihangaika kuuza vitabu vya fasihi.
Vitabu - bidhaa ya anasa
Duka la vitabu la TPH , ambalo ni kampuni pacha wa Mkuki na Nyota, iliyopo Tanzania bara jijini Dar es Salaam, ni miongoni mwa maduka ya vitabu nchini humo ambayo yanauza kazi za Gurna.
"Tuliona pengo kubwa katika sekta ya uchapishaji vitabu nchini Tanzania, inayojikita katika vitabu ambavyo havihusiani na elimu.
Haswa kwa vitabu ambavyo vimeandikwa na wazawa wenyewe wa Tanzania," anasema bwana Bgoya.
"Riwaya za Gurnah huwa zinachukua muda mrefu sana kuuzika, hivyo hatukuweka vitabu vingine."
Kwa mahitaji ya wateja wachache, inatufanya kuweka bei ya juu ya kuuzia vitabu , hivyo kuwafanya watu wengi kushindwa kununua vitabu.
"Soko ni dogo na haliwezi kuwa na vitabu vingi," alisema.
"Bei ya vitabu imekuwa ghali sana, na katika suala la uchumi, vitabu vinakuwa bidhaa za anasa."
Mpaka sasa , kazi za Gurnah hazijajumuishwa katika mtaala wa elimu ya fasihi katika shule za nchini Tanzania licha ya kuwa kuna waandishi wa Afrika na kiswahili ambao riwaya zao zinasomwa shuleni.
"Kazi yake imetambulika nje ya Zanzibar na amekuwa nje ya nchi hiyo tangu mwaka 1967," anasema bwana Jussa.
"Hivyo anajulikana na wasomaji wachache ambao huwa wanawafuatia waandishi wa fasihi au riwaya wa Zanzibar."
Vitabu vya tafsiri ya Kiswahili vinakuja
Miongoni mwa sababu kwa kazi za Gurnah kutofahamika nyumbani ni kwa sababu anaandika kwa lugha ya kiingereza - na sio kwa kiswahili, lugha ambayo inazungumzwa na Watanzania wengi na ndiyo lugha mama ya mshindi wa Tuzo ya Nobel.
Amekuwa akipata simu nyingi za kumshawishi atafsiri riwaya zake kwa lugha ya kiswahili.
Dkt Ida Hadjivayanis, mhadhiri wa Kiswahili wa School of Oriental and African Studies (Soas) mjini London, tayari alikuwa ameanza kulifanyia kazi suala hili kabla hata Gurnah kushinda Tuzo ya Nobel.
Kwa sasa anamalizia tafsiri ya kwanza ya Kiswahili ya kitabu chake, kiitwacho Paradise, ambacho kitatolewa mapema mwaka ujao.
Kitabu cha Paradise, kilichapishwa mwaka 1994, ni hadithi ya mvulana aliyekulia nchini Tanzania mwanzoni mwa Karne ya 20 - ilikuwa riwaya yake ya mafanikio, iliyokuwa kwenye tuzo kadhaa za kifahari, na Dk Hadjivayanis ana matumaini kuwa tafsiri yake itamletea wafuasi wapya kwenye kazi zake.
"Historia, ukweli na kumbukumbu zetu zote zimejikita katika kazi hiyo kwa namna ya kupendeza," anasema msomi huyo ambaye pia anatoka Zanzibar.
"Nadhani kama kazi yake inaweza kusomwa Afrika Mashariki ingekuwa na matokeo kama haya."
Huku umaarufu wa Gurnah umekuwa katika ulimwengu wa fasihi, wengi wanasema sasa ni wakati wa kuhakikisha riwaya zake zinakuwa sehemu ya utamaduni wa Afrika Mashariki.
Maduka ya vitabu kote nchini, kama TPH, yameagiza nakala mpya za riwaya za Gurnah baada ya kuwa na maombi mengi kuhusu vitabu vyake.
"Wachapishaji wanapaswa kufanya sehemu yao katika kukuza mshindi wetu wa Tuzo ya Nobel na serikali inapaswa kufanya hivyo pia," anasema Dk Hadjivayanis.
Bado kuna kazi kubwa sana ya kufanya na kuhakikisha anabaki kwenye ramani.
"Hatuwezi kubadili utamaduni wetu wa kusoma mara moja, hivyo kwa yeye kusomwa hatua za kwanza ingekuwa ni kuweka vitabu kama Paradise na After Lives katika mtaala wa kufundishia shuleni.Vingine vingefuata."
Unaweza kusoma pia: