Tuzo ya amani ya Nobel : Je hawa ndio washindi waliozua utata zaidi?

Mshindi wa wa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2021 atatangazwa leo saa saba mchana. Je kutakuwa na mkanganyiko wowote kama ilivyokuwa katika matukio kadhaa katika tuzo zilizopita?

Tuzo hizi zinatajwa kuwa na heshima kubwa duniani, Nobel Peace Prize ni miongoni mwa tuzo sita ambazo zilianzishwa na hayati Alfred Nobel ambaye alikuwa mwanasayansi wa Uswizi na mfanyabiashara

Lakini kutokana na uhalisia wa kisiasa, tuzo za amani zimekumbwa na mvutano mara kadhaa kuliko tuzo nyingine tano.

Baadhi ya migongano iliyojitokeza na kuondoa umuhimu wa tuzo hizi ni:

Barack Obama

Watu wengi hawakuelewa wakati rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alipopata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2009 -akiwemo Laureate mwenyewe.

Hata Obama aliandika ujumbe mwaka 2020 , kufuatia kutangazwa kwake kuwa mshindi na kuhoji tuzo hiyo ni ya nini?

Alikuwa madarakani kwa miezi tisa tu na kupata tuzo ya Nobel, jambo ambalo lilikosolewa kuwa maamuzi ya mapema sana, kwanza siku ya mwisho ya kutuma majina ya washiriki ilikuwa imepita siku 12 baada ya Obama kuapishwa.

Mwaka 2015, mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya Nobel , Geir Lundestad, aliiambia BBC kuwa kamati ambayo ilifanya maamuzi ya ushindi huo ilijutia maamuzi yake.

Jeshi la Marekani lilitumwa nchini Afghanistan, Iraq na Syria wakati wa utawala wa rais Obama.

Yasser Arafat

Kiongozi wa zamani wa Palestine alipewa tuzo mwaka 1994 akiwa pamoja na waziri mkuu wa Israel wa wakati huo Yitzhak Rabin na waziri wa mambo ya nje wa Israeli Shimon Peres kwa kazi yao na kupata tuzo ya amani ya Oslo - ambapo miaka ya 1990s kulikuwa na matumaini ya kupata suluhu ya mgogoro wa Israeli na Palestine

Maamuzi ya kupewa tuzo kwa Yasser Arafat, aliyehusika katika shughuli za kijeshi , ilikosolewa na Israel na maeneo mengine.

Kiukweli, kuchaguliwa kwa Arafat kulisababisha mvutano hata kwa wana kamati wenyewe.

Mwanachama mmoja wa kamati , Kare Kristiansen ambaye ni mwanasiasa wa Norway, aliacha kazi kwasababu ya kupinga hilo.

Aung San Suu Kyi

Mwanasiasa huyo maarufu alishinda tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 1991 kwa mapambano yake yasiyo ya vurugu dhidi ya utawala wa jeshi huko Myanmar

Lakini zaidi ya miaka 20 baadaye, Aung San Suu Kyi alikosolewa vikali kushindwa kuongea dhidi ya mauaji ya watu wengi na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa Waislamu wa Rohingya katika nchi yake, Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa yalikuwa 'mauaji ya kimbari'.

Hata kulikuwa na wito wa kiongozi huyo kunyang'anywa tuzo hiyo, lakini sheria zinazosimamia tuzo hizo za Nobel haziruhusu hatua kama hiyo.

Abiy Ahmed

Mwezi Disemba mwaka 2020, waziri mkuu wa Ethiopia alipewa tuzo ya amani kutokana na jitihada zake za muda mrefu za kutatua mgogoro wa mpakani na Eritrea.

Lakini muda mfupi baada ya kupewa tuzo hiyo, swali lilkuwa, je yalikuwa maamuzi sahihi kwa kiongozi huyo kupewa tuzo.

Jumuiya ya kimataifa ilimkosoa Abiy Ahmed kwa kupeleka majeshi kaskazini mwa eneo la Tigray.

Mapigano ambayo yamesababisha maelfu ya watu kuuawa.

Wangari Mathai

Aliyekuwa mwanaharakati wa Kenya ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza mwafrika kupata ushindi wa tuzo ya Nobel mwaka 2004.

Lakini alitakiwa kuchunguzwa baada ya kuibuka na maoni yake dhidi ya VVU na Ukimwi.

Wangrai Mathai alisema virusi vya ukimwi , vilikuwa vimetengenezwa kama silaha ya kibailojia kwa lengo la kuwateketeza watu weusi.

Hakuwa na ushahidi wa kisayansi kutetea madai yake.

Henry Kissinger

Mwaka 1973, waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati huo Henry Kissinger alipata tuzo ya amani.

Kumpa tuzo kwa mtu ambaye alihusika katika baadhi ya sera zenye utata za Marekani, kama vile kampeni ya mabomu huko Cambodia na kuunga mkono mauaji ya kijeshi yaliyotokea kusini mwa Marekani .

Kissinger alipata tuzo ya pamoja na kiongozi wa kaskazini mwa Vietnam Le Duc Tho kwa jukumu lake la kufanya majadiliano ya kusitisha vita Vietnam.

Washindi wawili wa tuzo ya Nobel waliacha tuzo hizo na gazeti la New York Times liliandika kuwa hiyo ni tuzo ya vita ya Nobel.

Gandhi

Tuzo ya Nobel inajulikana kwa mapungufu yake ya kushindwa kumpa tuzo ya amani Mahatma Gandhi.

Licha ya kuwa kiongozi huyo wa India alipendekezwa mara kadhaa katika karne ya 20 lakini hakuwahi kupata tuzo.

Mwaka 2006, Mtaalamu wa historia Geir Lundestad, aliyekuwa rais wa kamati ya wanaochagua washindi wa tuzo ya amani , alisema kutotambuliwa kwa mchango wa Gandhi, lilikuwa kosa kubwa katika historia ya tuzo za Nobel.