Ifahamu nchi isiyokuwepo duniani lakini watu wake wanaendelea kuishi

Chanzo cha picha, umut kacar/alamy
Sauti kubwa inasikika kutoka kwenye mitaa ya jiji la Diyarbakkar, hata kama hujui neno hata moja la lugha ya Wakurdi moyoni mwako unaweza kuhisi uchungu unaotoka kwenye sauti hiyo.
Jiji la Diyarbkar, Uturuki, linatajwa kuwa mji mkubwa wenye wakurdi wengi nchini Uturuki. Ziara ya BBC katika jiji la Diyarbkar ilifanyika wakati wa majira ya joto. Ilikuwa joto sana. Eneo lote liligeuka rangi kuwa la njano kama miale kutoka kwenye jua kali. Barabara za mji huo hasa za lami zilikuwa zinachoma kwa joto.
Mchana, mji mzima ulionekana kama kutelekezwa. Lakini nyakati za jioni, utaanza kusikia sauti za watoto, wakiruka ruka na kufanya mazingira kuonekana ya kawaida. Wanawake waliovalia mitandio kichwani, wanatoka kwenye miji yao baada ya kumaliza shughuli za nyumbani na kwenda kununua bidhaa na kurejea baadae wakiwa na shehena ya bidhaa kwenye vyombo vya usafiri.
Sehemu hii inasifika kwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba kwa uzalishaji. Makelele, na sauti za maumivu zinazosikika ilikuwa ni mwangwi kutoka kwenye mitaa ya Diyarbkar. Sauti inatoka kwenye majengo ya mji huyo.

Chanzo cha picha, umut kacar/Alamy
Sauti zinaeleza historia ya maumivu ya Kurdistan
Sauti ya miti, mbwa wakibweka na sauti zingie zinasikika kwenye mitaa. Wakati mwingine unaweza kusikia sauti za honi ya magari. Hata katikati ya sauti nyingi, sauti hiyo ya maumivu inasikika lakini kwa utofauti. Sauti hiyo inaonyesha kwa wakati mmoja mapenzi, matumaini, huzuni na kukata tamaa.
Kwenye jengo moja linaloitwa Mala Dengbez au Dengbez, jengo lenye eneo zuri la kupumzikia kwa uani. Limewekwa nakshi nakshi licha ya kwamba ni jengo la zamani kidogo. Kuna eneo la wazi la maonyesho. Hapa ndipo sauti ile ya maumivu tuliokuwa tunaizungumzia hapo awali inasikika
Kuna binti alikuwa aneelezea historia chungu ama ya maumivu ya Kurdistan. Eneo ambao zamani liliitwa Kurdistan, leo limegawanyika katika nchi nne; Syria, Iraq, Uturuki na Iran. Wakurdi wengi hawana pa kwao baada ya mgawanyo huu, wengi wao sasa wakiishi Bemulk. Kutokana na lugha yao ya kikurdi, mila, utamaduni, na historia, wakurdi wameendelea kuuweka hai nchi yao kwenye mioyoni yao.
Miaka michache iliyopita, wanamgambo wa kikurdi walianzisha mgogoro na serikali ya Uturuki. Sehemu kubwa ya Diyarbakr city iliharibiwa na mapigano ya pande hizo. Juhudi za kuujenga mji huo kuurejesha katika hali yake ya zamani. Sehemu kubwa ya mji huu uko kwneye matengenezo.

Chanzo cha picha, Terry Richardson
Mchawi wa sauti
Kwenye eneo hili la Mala Dengbez, watu wengi wamekusanyika kumsikiliza mtu anaysimulia historia ya uchungu ya wakurdi, akiwa na mustachi mrefu. akivalia shati lililochanika na ameshika tasbihi kwneye mkno wake wa kulia. Akionekana kwenda kulia na kushoto
Huyu mtu ameongea kwa saa kadhaa akibadilisha namna ya kuongea na kwa sauti tofauti tofauti. Kuna wakati ilikuwa sauti ya mazungumzo kuna wakati sauti ya mashairi kw austadi mkubwa. Alionekana kama mchawi wa sauti. Wengi waliguswa na simulizi yake, wakiitikia kwa hisia, vichwa, mikono na wakati mwigine wakionekana kufuta machozi kutokana na kuingiwa na simulizi

Chanzo cha picha, Terry Richardson)
Nini maana ya Dengbe
Neno la kikurdi la Dengbe maana yake ni mchawi wa sauti. Linaundwa na maneno mawili Deng kwa maana ya sauti na Be kwa maana ya sema.
Ukweli ni kwamba wasanii wa Dengbe ni wasanii wa hadithi, kufanya hisotria ya wakurdi iendelee kuishi.
Katika vijiji na miji ya wakurdi, imekuwa ni utamaduni kwa watu kukusanyika pamoja na kusikiliza hadithi za kihistoria zinazowasiishwa na wasanii wa simulizi. Wengi wa wasimulizi wa hadithi hizi ni wanaume. Lakini wapo waimbaji wachache wanawake ambao wanapeperusha bendera ya utamaduni wa Dengbe.
Wanaweza wasiwe na elimu, lakini ujuzi wao wa kuzungumza na sauti, wanaonekana kubeba maktaba Ya hadithi uzoefu na historia kwneye vichwa vyao, utajiri ambao umekuwa ukirithishwa kizazi kwa kizazi

Chanzo cha picha, B.O'Kane/Alamy)
Changamoto ya Dengbe
Ingawa, kwa sasa Dengbe inatambuliwa, changamoto mpya inayojitokeza mbele yake ni kwamba watu wameanza kukimbilia mijini, kwenye miji ya mbali. Mmoja wao ni Baran Setin mwenye miaka 32. Alizaliwa kijijni milimani kwenye mpaka na Armenia. Ni eneo zuri, lakini maisha ni magumu. Ameamua kikimbilia Istanbul. Miaka mingi iliyopita wakurdi waliishi hapo.
Mjomba wake Baran ni msanii wa Dengbe, amejifunza kwa baba yake. Baran anasema sauti yake haifai kuwa mchawi wa sauti (Dengbe). "Nikisikia Dengbe, hata siielewei," anasema Baran.
Haya ni maisha na simulizi za historia ya maumivu wakurdi, ngumu kuelewa neno hata moja kwa wageni hasa wakati wa Dengbe. Upo wasiwasi wa kupotea kwa historia hii kama vijana kama Baran wataongezeka. Lakini kuna matumaini pia kwamba, krithisha utamaduni kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kutasaidia utamaduni wa kikurdi kuendelea kuishi














