Diego Maradona: Aliyekuwa daktari wa Maradona achunguzwa kuhusiana na kifo cha nyota huyo

Daktari wa maradona alitoa mahojiano yaliyowaliza watu baada ya kifo cha nyota wa kandanda
Maelezo ya picha, Daktari wa maradona alitoa mahojiano yaliyowaliza watu baada ya kifo cha nyota wa kandanda

Waendesha mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa Diego Maradona kwa uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea siku nne zilizopita .

Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo- Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.

Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.

Dokta Luque bado hajashitakiwa. Anakana kufanya kosa lolote.

Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kujganda kwa damu , uliofanikiwa mapema mwezi wa Novemba na amekuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe.

Binti yake alikuwa amesisitizia kupata taarifa zaidi kuhusu matibabu ya baba yao.

Je uchunguzi unalenga nini hasa?

Polisi wapatao 30 walivamia makazi ya daktari dokta Luque Jumapili asubuhi - huku wengine 20 wakienda katika kliniki yake iliyopo katika mji mkuu Buenos Aires.

Uvamizi huo uliagizwa na Waendesha mashitaka wanaojaribu kujenga picha kwamba kuhusu siku zamwisho za maisha ya Maradona nyumbani kwake.

Walichukua kompyuta, simu za mkononi na taarifa za matibabu, wanasema maafisa.

Maafisa wanaangalia rekodi za matibabu ya mchezaji nyota wa soka

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maafisa wanaangalia rekodi za matibabu ya mchezaji nyota wa soka

Wanashuku kwamba nyota huyo wa soka aliruhusiwa kwake kwenda nyumbani hakukutimiza vigezo vya kumruhusu atoke hospitalini, ikiwemo kupewa wauguzi au nesi wa kumuhudumia saa 24 "wataalamu wa uraibu ",kupewa daktari anayeweza kumuita wakati wowote na gari la kubebea wagonjwa lenye vifaa vya kumsaidia kupumua.

Maafisa wanataka kufahamu kuhusu uhusika wa daktari Luque katika mipango ya kupona kwa Maradona katika nyumba ya nyota huyo.

Dokta Luque anajitetea vipi?

Katika mkutano na waandishi wa habari uliokgubikwa na hisia Jumapili , Dkt Luque - ambaye alielezewa kama daktari wa kibinafsi wa Maredona -aliangua kilio, akisema kuwa alifanya kile alichoweza kuyanusuru maisha yake ya rafiki yake. Alisema kuwa Maradona alikuwa ni mwenye huzuni katika siku za hivi karibuni .

Wakati mmoja daktari aliwakaripia waandishi wa habari : " Mnataka kujua ni upi wajibu wangu ? Kwa kumpenda, kwa kumhudumia , kwa kurefusha maisha yake , kwa kuyaboresha mpaka mwisho ."

Daktari alisema kuwa alifanya " chochote ambacho, hadi kile ambacho hakikuwezekana ".

maradona

Akizungumzia masuala ambayo maafisa wanataka kuyachunguza , dokta Luque alielezea iliyokuwa kazi yake .

''Ukiniuliza mimi, mimi nilikuwa daktari wa upasuaji wa ubongo na kazi yangu iliisha . Nilikuwa nimemalizana ," alisema akizungumzia upasuaji aliomfanyia mwezi Novemba - na akasisitiza kuwa kuruhusiwa kwa Maradona kwenda nyumbani haukuwa wajibu wake.

maradona
Maelezo ya picha, Diego Maradona "ataishi mioyoni mwetu daima"

"Maradona angepaswa kwenda kwenye kituo cha kurekebisha tabia. Hakutaka kufanya hivyo," Dokta Luque alisema,akimtaja marehemu nyota huyo kama mtu ambaye "ilikuwa vigumu kufikiria ni mtu wa aina gani ".

Anasema hajui ni kwanini hakupewa gari la ambiolansi lenye vifaa au ni nani alihusika na kutopelekwa kwa gari hilo nje ya nyumba ya Maradona.

Na aliongeza kuwa : Diego "alikuwa mtu mwenye huzuni , na alitaka kuwa peke yake, na sio kwasababu hakuwapenda binti zake , familia yake au wale waliomzingira".