Virusi vya corona: Watu za zaidi ya 500,000 wamekufa kwa Covid-19 duniani huku Texas hali ikiwa ni ya kutisha

Idadi ya watu walioambukizwa imekua ikiongezeka kwa kasi kubwa katika Amrika Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Idadi ya watu walioambukizwa imekua ikiongezeka kwa kasi kubwa katika Amrika Kusini

Zaidi ya watu 500,000 duniani kote wamepoteza maisha yao kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins University nchini Marekani.

Tangu mlipuko wa virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka jana, kumekuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 10, kulingana na Johns Hopkins.

Nusu ya maambukizi yote yalikua yametokea nchini Marekani na Ulaya lakini sasa ugonjwa wa corona inaendelea kukua kwa kasi nchini Marekani.

Virusi hivyo vimeathiri Asia ya kusini na Afrika ambako kunatarajiwa kuwa na maambukizi mpaka mwishoni mwa Julai.

Mlipuko huo bado unaenea katika maeneo mengi ya dunia, kesi mpya zilizorekodiwa kwa siku sita zikiwa milioni moja.

Waandamanaji walishikiliwa katika mji wa Austin, Texas, kwa kukiuka maagizo ya kuvaa barakoa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji walishikiliwa katika mji wa Austin, Texas, kwa kukiuka maagizo ya kuvaa barakoa

Marekani imeripotiwa kuwa na jumla ya maambukizi milioni 2.5 na vifo 125,000 vilivyotokana na Covid-19 mpaka sasa na maambukizi zaidi katika nchi nyingine.

Majimbo ya Marekani ambayo yalikuwa yamefunguliwa wiki za karibuni haswa upande wa kusini , yameripotiwa kuwa maaambukizi yameongezeka.

Ongezeko la maambukizi mapya limeonekana zaidi huko Texas, Florida na majimbo mengine ambapo imewabidi kuweka tena zuio la biashara kuendelea.

Takwimu zinaonyesha mataifa kadhaa kutoka bara la Asia na waafrika wanaweza kupata maambukizi zaidi ya mataifa ya wazungu.

Nchi ambayo ni ya pili kuwa na wagonjwa wengi Brazil, taifa hilo lina wagonjwa milioni 1.3 na vifo vinavyozidi 57,000.

coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu corona:

coronavirus

Licha ya kuwepo kwa maambukizi mapya, jimbo la Rio de Janeiro limesema kuwa litaruhusu michuano ya mpira wa miguu kuanza kwa mashabiki kuhudhuri akuanzia Julai ,10 - kwa kiwango cha moja ya tatu ya uwezo wa uwanja wa mpira.

Waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa jimbo la Texas wa Austin

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji walikusanyika katika mji mkuu wa jimbo la Texas wa Austin

Siku ya Jumapili China iliweka marufuku ya kutotoka karibu na mji wa Beijing ili kukabiliana na mlipuko.

Karibu watu nusu milioni hawataruhusiwa kusafiri kutoka na kuingia katika Anxin ambayo iko karibu na jimbo la Hebei.

Nchini Uingereza , ikiwa na idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na corona katika upande wa kaskazini, itaweka marufuku tena kufuatia maambukizi mapya katika mji wa Leicester.

Wakati huohuo kuenea kwa maambukizi vya virusi vya corona yamegeuka kuwa hatari zaidi Marekani katika jimbo la Texas, Govana Greg Abbott alitoa angalizo.

China inahofia uwezekano wa kulipuka kwa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, China inahofia uwezekano wa kulipuka kwa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona

"Zaidi ya wiki kadhaa zilizopita , idadi ya maambukizi mapya ni kati ya 2,000, mpaka 5,000," bwana Abbott alisema siku ya Jumapili.

Majimbo kadhaa kusini na kaskazini yamerikodiwa kuwa maambukizi mengi mara tu marufuku ya kutoka nje ilipopunguzwa makali.

Idadi ya maambukizi kwa sasa inafika milioni 2.5.

Zaidi ya wagonjwa 125,000 wa corona wamethibitishwa kufariki duniani kote na zaidi katika mataifa mengine.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?