Virusi vya corona: Kwanini kuna mlipuko wa virusi vingi hatari?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita idadi ya milipuko ya virusi imeongezeka, na magonjwa yamesambaa kwa kazi - kama ilivyo kwa virusi vya corona nchini China hivi sasa vimeendelea kusambaa .Je ni kwanini?
Ni ukweli rahisi kabisa kuwa hivi sasa idadi ya watu imekuwa kubwa kuliko nyakati zote zilizowahi kutokea - Idadi ya watu duniani kwa sasa ni Bilioni 7.7 pengine na zaidi. Na tunaishi tukiwa karibu karibu sana
Watu wengi zaidi wanaoishi katika maeneo yenye nafasi ndogo inamaanisha kuwa kuna kuwa na hatari zaidi ya kupatwa na wadudu wanaosababisha ugonjwa

Chanzo cha picha, Healthmap.org
Virusi vya corona vinaelezwa kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya. Virusi huishi kwa muda fulani tu nje ya mwili, hivyo kwa kuwa karibukaribu ugonjwa huenea.
Mwaka 2014 ugonjwa ulisambaa kwa kupitia damu na maji maji mengine, lakini kwa wale wanaokuwa karibukaribu wanaweza kuambukizana.
Lakini si virusi vyote huambukizwa kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hata Zika, ambayo huambukizwa kutoka kwa mbu kwenda kwa mwanadamu. Mbu wanaosababisha Zika huishi katika maeneo ya mijini ambao huzaliana kwenye maeneo yenye watu wengi, unyevunyevu na maeneo ya joto.
Tangu mwaka 2007 binaadamu wameishi kwenye miji. Zaidi ya watu bilioni nne sasa wanaishi kwenye 1% ya ardhi ya sa 1% of the planet's land mass.
Na miji mingi ambayo tunahamia haiko tayari kwa ajili yetu. Hivyo watu wengi wanaishia kuishi kwenye maeneo duni ambayo huwa na upungufu wa maji safi au mfumo wa maji taka, hivyo magonjwa husambaa haraka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sawa Ndege au treni ya mwendo kasi virusi hivi vinasambaa kwa kasi karibu nusu ya dunia ka chini ya nusu siku. Katika kipindi cha wiki chache tangu mlipuko wa virusi vya corona visa kadhaa vya maambukizi ya virusi hivyo vimerekodiwa katika nchi zaidi ya nchi 16.
Mwaka 2019 mashirika ya ndege yalisafirisha abiria bilioni 4.5 - miak kumi iliyopita mashirika hayo ya ndege yalisafirisha abiria bilioni 2.4.
Wuhan ni kituo kikuu cha treni za kasi na mlipuko wa virusi hivyo ulitokea wakati ambapo China ilikuwa inajiandaa kwa sikuu ya mwaka mpya ambapo safari zaidi ya safari zaidi ya bilioni hufanyikakatika made across the country around Chinese New Year.
Ndege, Treni na vyombo vyombo vingine vya moto vinamaanisha kuwa virusi vinaweza kusafiri karibu umbali wa nusu ya dunia. Ndani ya wiki chache za mlipuko wa virusi vya corona, watu kadhaa walishukiwa katika zaidi ya nchi 16.
Mwaka 2019 ndege zilisafirisha abiria bilioni 4.5- miaka kumi iliyopita ilikuwa bilioni 2.4.
Wuhan ni kituo kikuu cha reli ya treni ziendazo kasi nchini China na virusi vimeingia nchini humo ambapo zaidi ya safari bilioni moja hufanyika nchi nzima wakati wa msimu wa mwaka mpya wa China.
Moja kati ya magonjwa mabaya kuwahi kurekodiwa ni pamoja na mafua makali mwaka 1918 yajulikanayo kwa jina spanish flu.
Yalianzia barani Ulaya wakati wa uhamiaji wa watu wengi, kuelekea kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia.
Wakati mafua yakisambaa, wanajeshi walikuwa wakirejea nyumbani kwa nchi zao wakipeleka mafua makali kwenye jamui zao ambazo hazikuwa na chochote cha kuzuia virusi, au kupata chanjo ya kuzuia maambukizi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti wa mtaalamu wa masuala ya virusi na magonjwa yanayosababishwa navyo, John Oxford amesema chanzo cha virusi hivyo inaweza kuwa kambia, ambazo karibu wanajeshi 100,000 walifariki kila siku.
Hata wakati wa kabla ya usafiri wa anga, ugonjwa huo ulisafiri katika karibu sehemu zote za dunia. iliua watu kati ya milioni 50 na milioni 100.
Bado spanish flu ilichukua miezi tisa kusambaa duniani. Katika dunia ambayo tunaweza kusafiri kwa siku moja, virusi vya mafua vinaweza kusambaa haraka.
Nyama zaidi, wanyama zaidi, magonjwa zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Ebola,SARS na sasa virusi vya corona vyote ni virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binaadamu, virusi vya corona vimeanzia kwenye soko la nyama mjini Wuhan - ripoti za awali zinasema inaweza kuwa kutoka kwa nyoka.
Mapenzi yetu kwa nyama yamekuwa yakiongezeka, ufugaji wa wanyama umekuwa ukiongezeka wakati sehemu mbalimbali duniani.
Nchini China masoko ya nyama yako kwa wingi kwenye maeneo ya watu wengi. Hiyo inaweza kuwa sababu ya ugonjwa huo kuanzia huko.
Pia, wakati miji yetu ikitanuka watu hukaribiana na wanyama pori. Homa ya Lassa ni moja ya ugonjwa ambao ulisambaa kwa njia hii- wakati watu wakikata miti na kutumia ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo, panya wanaoishi ardhini kama makazi huambukiza virusi ambavyo wat huvibeba na kupata homa ya Lassa.
Bila shaka hatuko tayari

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa dunia imekuwa kama kijiji, bado hatuna mfumo wa afya wa dunia ambao utaweza kupambana na vitisho vinapotokea.
Kupambana mlipuko,tunategemea zaidi serikali , ikishindwa dunia nzima inakuwa hatarini.
Hakuna sehemu nyingine iliyopitia haya zaidi kama Afrika Magharibi wakati wa mlipuko wa Ebola. Pale mifumo ya afya ya nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone iliposhindwa kudhibiti kusambaa kwa virusi.
Ebola iliua watu 11,310 Afrika Magharibi.
Ni bahati kwa sehemu nyingine duniani ni virusi vinavyosambaa taratibu lakini virusi vinavyosafiri kwa njia ya hewa au corona husambaa haraka sana.
Milipuko huweza kutokea kwenye maeneo duni ambayo yana mifumo mibaya ya afya. Kutokuwepo kwa elimu kuhusu usafi, pia idadi kubwa ya watu vyote huongeza hatari.
Mifumo michache sana ya afya iko tayari kuwekeza zaidi kwenye milipuko ya magonjwa ambayo yanaweza yasijitokeze. Wakati mafua ya nguruwe yalipojitokeza kulikuwa na dawa nyingi, lakini wakosoaji walidai kuwa kulikuwa na hatua nyingi zilizochukuliwa kwa virusi ambavyo baadae vilijulikana kuwa havikuwa vya hatari.
Habari njema

Chanzo cha picha, Getty Images













