Polisi wafuatilia wahalifu wa misimamo mikali Ufaransa

Ufaransa ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na matukio ya ugaidi hivi karibuni
Maelezo ya picha, Ufaransa ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na matukio ya ugaidi hivi karibuni

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amesema kuwa polisi wanafuatilia watu karibu elfu kumi na tano nchini Ufaransa wanaotuhumiwa kuwa na msimamo mkali.

Valls amewaambia waandishi wa habari kuwa mashambulio kadhaa ya waislamu yamezuiliwa ,amesema mashambulio mawili yalizuiliwa wiki iliyopita.

Waziri mkuu wa Ufaransa Manual Valls
Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Ufaransa Manual Valls

Polisi walimkamata kijana mmoja nyumbani kwao Paris siku ya jumamosi kwa tuhuma za kupanga shambulio la kisu.