Afcon 2021: Darubini ndani ya kundi F - Algeria, Mali, Mauritania na Gambia

Algeria lift the Africa Cup of Nations trophy in 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Algeria wanatazamia kutetea taji la Kombe la Mataifa ya Afrika waliloshinda mwaka wa 2019

Michuano ya 33 ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanza Jumapili nchini Cameroon, ikiwa imecheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la corona.

Hapa, tunaangazia kundi F, ambalo linajumuisha Tunisia, Mali, Mauritania na Gambia.

Ratiba

Jumatano, 12 Januari: Tunisia v Mali, Mauritania v Gambia

Jumapili, 16 Januari: Gambia v Mali, Tunisia v Mauritania

Alhamisi, 20 Januari: Gambia v Tunisia, Mali v Mauritania

Tunisia

Farouk Ben Mustapha in action for Tunisia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Farouk Ben Mustapha alikuwa nahodha wa Tunisia hadi fainali ya Kombe la Kiarabu, ambapo walichapwa 2-0 na Algeria baada ya muda wa ziada.

Souhail Khmira (mwandishi wa habari za michezo wa Tunisia): Kwa kuzingatia mchezo wa Tunisia katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia na Kombe la Kiarabu nchini Qatar, kusonga mbele kwenye Kombe la Mataifa haitakuwa kazi rahisi.

Bosi Mondher Kebaier amekosolewa kwa kushindwa kupata matokeo ya kuridhisha, na chaguo lake la wachezaji limekuwa likitiliwa shaka mara kwa mara na mashabiki.

Tunisia wamekuwa wakichagua aina ya uchezaji ya kulinda, ambayo inabadilikabadilika kulingana na wapinzani wao.

Mchezaji wa Esperance de Tunis, Mohamed Ali Ben Romdhane ni mmoja wa wachezaji wa kutazamwa zaidi, Hannibal Mejbri (Manchester United) naye ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi chache alizocheza huku Wahbi Khazri akibaki kuwa mmoja wa watu wenye thamani kubwa.

Tunisia inasalia kuwa mojawapo ya timu bora licha ya matokeo yao duni hivi karibuni, huku Carthage Eagles mara nyingi wakifanikiwa kuwashangaza mashabiki wao kwa kufuzu dakika za mwisho.

Mali

Mali team in October 2021

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mali went unbeaten in 2022 World Cup qualifying to reach Africa's play-offs for the tournament in Qatar

Baba Cissouma (Mwanahabari katika jarida la March nchini Mali): Kwa ushiriki wake wa 12 katika Kombe la Mataifa, Mali inataka kupanda kwenye jukwaa la juu zaidi kwa mara ya kwanza.

The Colts wa kocha Mohamed Magassouba walikuwa wakielea katika kufuzu kwa dimba hili, na walifanya vyema walipofika hatua ya muondoano ya Kombe la Dunia pia: kushinda tano na kutoka sare mchezo mmoja kati ya sita, wakiwa na mabao 11 na kutofungwa.

The Eagles watafurahi kucheza nchini Cameroon, ambapo walifika fainali za Kombe la Mataifa ya 1972 na Ubingwa wa Mataifa ya Afrika 2020.

Mali inaweza kutegemea ukomavu na umbo la wachezaji chipukizi wa kikosi hicho, takriban wote ni mabingwa wa Afrika katika ngazi ya U-17, washindi wa medali za fedha katika Kombe la Dunia la U17 au washindi wa shaba wa Kombe la Dunia la U-20 kati ya 2015 na 2017.

Mauritania

Mauritania ahead of a game against Syria at the 2021 Arab Cup

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mauritania ilichapwa mabao 5-1 na wapinzani wao wa kundi la Kombe la Mataifa ya Afrika, Tunisia kwenye Kombe la Kiarabu mwezi Novemba

Lassana Camara (Mwandishi wa habari wa Mauritania): Baada ya mtihani wa kwa kocha Didier Gomes da Rosa kwenye Kombe la Kiarabu, wakati umefika kwa Mfaransa huyo kufanya ujenzi mpya wa timu.

Da Rosa, ambaye alimrithi mshirika wake Corentin Martins mnamo Novemba, aliweza kufahamu kundi lake au sehemu yake.

Ikumbukwe wachezaji wengi wakuu hawakuwepo wakati wa Kombe la Waarabu, wakiwemo Aboubakar Kamara (Aris), Ibrehima Coulibaly (Le Mans) na Aly Abeid (Valenciennes).

The Mourabitounes wanapata wapinzani wawili wa zamani katika Kundi F. Watunisia wanachukuliwa kuwa wapinzani walubwa huku wenyeji wa Mali waliwatisha wakati wa toleo la awali la Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri.

The Gambia

Tom Saintfiet on the side lines

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa Gambia Tom Saintfiet amezifundisha timu za taifa katika mashirikisho manne tofauti ya Fifa

Momodou Bah (Mwandishi wa Habari za Michezo, Gambia): Gambia itakuwa miongoni timu mbili geni nchini Cameroon, baada ya kuwashangaza wababe wa soka barani humo kwa kufuzu kwao kihistoria mwezi Machi.

Nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi ilianza kampeni yake katika hatua ya awali mnamo Oktoba 2019 na kumaliza kileleni mwa kundi lao la kufuzu, ambalo lilijumuisha wapinzani walio na viwango vya juu na wenye sifa nchini Gabon, DR Congo na Angola.

Tangu kuteuliwa kwake Julai 2018, Tom Saintfiet amegeuza matokeo Scorpions, akiandikisha ushindi wao wa kwanza katika kipindi cha miaka mitano dhidi ya Benin mwezi huo wa Novemba. Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Togo na Namibia amekosolewa vikali kwa aina yake ya uchezaji na vigezo vyake vya uteuzi.

Tunisia na Mali ndizo zinazopewa nafasi kubwa katika kundi hilo lakini ikiwa timu nne kati ya sita zilizo katika nafasi ya tatu zimehakikishiwa kutinga hatua ya mtoano, Gambia itafurahia nafasi yao ya kusonga mbele.

Mshambulizi wa FC Zurich Assan Ceesay amekuwa mwindaji haramu wa mabao huku Musa Barrow (Bologna), Ablie Jallow (FC Seraing), Omar Colley (Sampdoria) na nyota wa zamani wa Manchester United Saidy Janko wakitarajiwa kucheza sehemu kubwa.