Andrew Watson: Mwanasoka mweusi 'mwenye ushawishi mkubwa' ambaye hakutambuliwa

Chanzo cha picha, Rachell Dallas
Andrew Watson alikuwa nahodha wa timu wa Scotland ikiyopata ushindi wa 6-1 dhidi ya England mwaka 1881. Alikuwa mchezaji wa kwanza wa kimataifa mwenye asili ya Afrika lakini kwa zaidi ya karne, mafanikio yake makubwa hayakutambuliwa.
Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya miongo mitatu umetupa taarifa zinazomhusu: mwanamume kutoka kwa watumwa mzaliwa wa Guyana, aliklelewa kuwa mwanamume wa kizungu na kupata umaarufu kama mcheza soka bora zaidi huko Scotland.
Miaka 100 baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 64 Watson bado anabaki kutoeleweka vizuri.
Wakati Watson alihamia Glasgow mwaka 1875 akiwa na umri wa miaka 18 hakuwa amecheza soka.
Ilikuwa ni wakati mchezo wa soka ulikuwa unakua na hakukua na sheria hata moja kuhusu soka iliyokuwa inatumika.
Katika kipindi cha miaka sita alikuwa amejijenga kama mmoja wa wacheza soka waliokuwa na vipawa vya juu na wenye kuheshimika waliosaidia kukuza mchezo huo wa kukimbia na kupokezana, hatua za kwanza za kukua kwa soka hadi kufikia kile tunachokishuhudia leo.

Watson Mara mbili alicheza dhidi ya England, na kwa kila mechi Scotland waliibuka washindi. Ushindi wa pili wa bao 5-1 katika uga wa Hampden Park, ulikuwa ushindi ambao ulichangia shirika la soka la Uingereza kufanyia soka mabadiliko.
Walimuomba Watson awaonyeshe njia baada ya wao kuunda kikosi kipya cha soka; Corinthian FC ambayo baadaye ilitambuliwa kwa kuuza mchezo wa soka kote duniani.
Watson aliyepata elimu shule ya serikali alikuwa mmoja wa walimu wa kwanza.
Alichukua wajibu wa 'Scotch Professor' na kuwafunza wachezaji wenzake wa kizungu katika klabu ya Corinthian na vilabu vingine kadhaa kuhusu sayansi ya kupitisha mpira.
"Pele alikuwa mcheza soka mwenye akili nyingi sana, lakini kuna maelfu ya wacheza soka wenye akili ambao umaarufu wao hufifia muda wanapostaafu," anasema Ged O'Brien muasisi wa makavazi wa soka ya Scotland.
"Unaweza kutazama mchezo wowote wa soka ukichezwa popote pale duniani na mtu yeyote wa jinsia yoyote, kabila au tamaduni- na mzuka wa Andrew Watson utakuwa unakutazama kwa sababu wanacheza mchezo wake.
Watson bado ndiye mcheza soka mweusi bora zaidi na hakuna mtu anayemkaribia.

Chanzo cha picha, Scottish Football Museum
Wakati wa maisha yake, ushawishi wake ulijulikana kwenye mchezo. Alikuwa nahodha wa timu ya taifa iliyoshinda kombe, msimamizi, muwekezaji, na afisa wa mchezo na kwa kila mafanikio alikuwa ni mtu mweusi wa kwanza kufanya hivyo.
Wanahistoria watafiti na wasomi wamefanya kazi ngumu kuyafahamu maisha yake.

Watson alizaliwa mwaka 1856 huko Georgetown, Demerara, kituo cha biashara za wakoloni kilichoanzishwa na waholanzi, kikatwaliwa na wafaransa na kisha jina lake likabadlishwa na Waingereza waliowasafirisha watumwa kutoka Afrika kufanya kazi kwenye mashamba yake.
Sasa ndio mji mkuu wa nchi ya Guyana ambayo imekuwa jamhuri tangu mwaka 1970 miaka minne baada ya kutangaza uhuru wake kutoka Uingereza. Inapakana na Suriname, Venezuela na Brazil
Watson alihamia uingereza akiwa karibu miaka miwili. Akapata elimu katika baadhi ya shule bora zaidi nchini Uingereza. Familia yake ikapata utajiri na ikawa na ushawishi.
Mama yake Watson Anna Rose, alikuwa mawanamke mweusi aliyezaliwa kwa watumwa na kunusuriwa akiwa msichana mdogo pamoja na mama yake Minkie.
Pia kwenye familia hiyo yuko John Gladstine, mmoja wa wamiliki wakubwa zaidi wa watumwa huko West Indies na baba yake William Gladstone ambaye alihuduma kwa kipindi cha miaka 12 kama waziri mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1868 na 1894.
Katika karne ya 19 familia ya Watson ilikuwa inawekeza katika benki na reli na kupata utajiri mkubwa kipindi hicho.
Andrew Watson alizaliwa katika moja ya familia zenye nguvu za wafanyabishara wa watumwa katika histora ya biashara ya utumwa nchini Uingereza.

Chanzo cha picha, Scottish Referee
Huyu ni mwanamume aliyekuwa amebahatika sana, Binamu yake alikuwa waziri mkuu na familia yake ilimilki benki.
Baada ya kuhamia Uingereza dada yake mkubwa Annetta Watson alihudhuria shule ya Heath Grammar huko Halifax, West Yorkshire na kuendelea na masomo yake huko King's College, London, na pia Glasgow University.
Akiwa na miaka 21alipata urithi wa karibu pauni 6,000 alioachiwa baada ya kifo cha baba yake. Pesa hizo ni sawa na pauni 700,000 leo hii. Akawekeza baadhi katika klabu ya soka ya Parkgrove, na pia kwenye biashara ya maduka ya kuuza bidhaa za jumla

Chanzo cha picha, Ged O'Brien
Muda mfupi baada ya kuwasili London kama mchezaji mwaka 1882, mke wa kwanza wa Watson Jessie Nimmo Armour alifariki. Watoto wake wakawa wamebaki na nyanya na babu yao huko Glasgow kwa miaka 30 iliyofuatia.
Mwaka 1888 alikuwa kileleni kwa taaluma yake akichezea Bootle - hasimu mkuu wa Everton. Huko aliweka makao yake mapya na mke wake wa pili Eliza Kate Tyler ambaye pamoja walizaa watoto wawili zaidi, akastaafu kutoka soka na kujifunza uhandisi wa masuala ya baharini
Akaelekea baharini, akifanya kazi na kampuni moja kutoka West Indian na Pacific na kupanda cheo hadi kufikia muhandisi mkuu.

Chanzo cha picha, Scottish Football Museum
Kifo chake kilitangazwa mwaka 1921 kwenye magazeti ya The Richmond na Twickenham Times, yaliyomtaja kama binamu wa waziri mkuu Gladstone. Mchango wake kwenye soka haukutajwa.
Kwa miongo kadhaa kaburi lake Waston halikujulikana liko wapi. Lilikisiwa kuwepo Australia au Mumbai. Mitchell alikuwa mtu ambaye aligundua eneo halisi liliko kaburi hilo, katika makaburi ya Richmond, kusini magharibi mwa London.













