Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 28.08.2021:Mbappe, Richarlison, Haaland, Jesus, Cavani, Zouma, Witsel, Barkley

Chanzo cha picha, AFP
Paris St-Germain itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 24, ikiwa watakubaliana kuhusu mpango wa kumuuza mshindi wa Kombe la Dunia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kwa Real Madrid. (Sky Sports)
Everton wanadai pauni milioni 85 kwa mchezaji huyo wa zamani wa Watford Richarlison(Star)
PSG itamlenga fowadi wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 24, ikiwa Mbappe ataondoka. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund wa Norway Erling Braut Haaland, 21, ni mwingine kwenye rada ya PSG endapo Mbappe atahamia mji mkuu wa Uhispania. (Star)
Everton wamewasiliana na Celtic juu ya makubaliano ya mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard, 23 (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Uruguay wa Manchester United Edinson Cavani, 34, "bado yuko kwenye mipango ya United msimu huu" na "hakuna mpango wa kumuuza" baada ya kuwasili kwa Cristiano Ronaldo (Goal)
Kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson alichukua jukumu kubwa kumshawishi mshambuliaji wa Ureno Ronaldo, 36, kurudi Old Trafford miaka 12 baada ya kuondoka kwenda Real Madrid. (Mirror)
Uhamisho wa Kurt Zouma wa Pauni 25m kwenda West Ham kutoka Chelsea upo mashakani baada ya matatizo na matibabu ya beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26. (Mirror)

Chanzo cha picha, Rex Features
Sevilla wanasema Chelsea wanapitwa na muda wa kumsajili beki wa Ufaransa Jules Kounde, 22, ambaye ana kifungu cha kuachiliwa cha pauni milioni 77.1. Blues wana nia ya kusaini mchezaji huyo wa zamani wa Bordeaux. (FootballEspana)
Chelsea inaweza kuwaachiliwa wachezaji
Ross Barkley, 27, na Danny Drinkwater, 31, ili kupunguza mzigo wa kuliwapa mshahara kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa Jumanne ijayo. (Sun)

Aston Villa wana nia ya kumsajili kiungo wa Ubelgiji na Dortmund, Axel Witsel, 32. (Tuttosport - in Italian)
Wolves wamewasilisha ofa ya pauni milioni 12.8 kwa mlinzi wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car, 24 (Get French Football News)
Blackburn, Bournemouth, Swansea na Stoke zote zinataka kumsajili winga wa zamani wa vijana wa England Patrick Roberts, 24, ambaye anapatikana bure kutoka Manchester City. (Sky Sports)













