Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 26.08.2021: Mbappe, Ronaldo, Arteta, Kane, Guardiola, Loftus-Cheek

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus imemwambia Cristiano Ronaldo kwamba wako tayari kumuuza msimu huu - lakini hilo litafanyika tu iwapo mahitaji yao yataafikiwa.
Mshambuliaji wa Portugal Ronaldo ,36, amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake.
Hatma yake imekuwa ikichunguzwa na akawachwa nje katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika mechi ya ufunguzi wa ligi ya Serie A dhidi ya Udinese.
Ajenti wa Ronaldo Jorge Mendes amewasiliana na klabu kuu barani Ulaya kuhusu kumsajili Manchester City na Paris St-Germain.
Manchester City wanaweza kumgeukia mshambuliaji wa Juventus na Ureno Ronaldo, 36, baada ya nahodha wa England, Harry Kane kusema anabaki Tottenham. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Paris St-Germain wanataka dau la £188m kutoka Real Madrid kwa ajili ya mshambuliaji wake Mfaransa Kylian Mbappe, 22. (Le Parisien - in French)
Kane, 28 amesikitishwa na mwenyekiti wa Tottenham chairman Daniel Levy kutoruhusu aondoke na naweza akasaini mkataba mpya. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja Pep Guardiola ataondoka Manchester City pale mkataba wake utakapomalizika msimu wa mwaka 2022-23 ili kupumzika kabla ya kuhamia kufundisha timu za taifa. (Globo, via Manchester Evening News)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta hayuko katika hatari ya kutimuliwa kibarua chake licha ya washika bunduki hao kuanza vibaya msimu hiu wa ligi kuu ya England.
Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anahusishwa na mipango ya kuchukua nafasi ya Arteta. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Roma Jose Mourinho amepanga kutumia £13.5m kwa ajili ya kiungo wa Chelsea muingereza Ruben Loftus-Cheek, 25. Nyota huyo aliwahi kidogo kufanya kazi na Mourinho wakati mreno huyo aliporejea kuifundisha Chelsea kwa mara ya pili. (Mail)
Manchester United haitaweza kupeleka dau kwa ajili ya kiungo wa Rennes mfaransa Eduardo Camavinga, 18, au kiungo wa Atletico Madrid na Hispania Saul Niguez, 26, kama haitauza wachezaji wake kupata fedha za kuingia sokoni. (ESPN)
Chelsea wanaelezwa wako katika nafasi nzuri ya kumsajili Niguez, huku Atletico wakiwa tayari kumuuza Mhispania huyo. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sevilla wanasema walikataa ofa ya Chelsea kwa ajili ya mlinzi wake mfaransa Jules Kounde,22 na hawahitaji kuuza wachezaji. (Goal)
Kiungo wa Barcelona Ilaix Moriba huenda akatua Chersea ama RB Leipzig kama kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 raia wa Guinea hataongeza mkataba mpya na wakali hao wa Laliga. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Winga wa Arsenal na Brazil Willian, 33, anajaribu kukamilisha uhamisho wake kuelekea Corinthians. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Koungo wa zamani wa Arsenal na England Jack Wilshere, 29, anafikiria kustaafu soka baada ya kukosa ofa ya kujiunga na klabu yeyeote tangu aachwe na klabu ya Bournemouth. (Athletic)
Kiungo wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets amekubali kukatwa tena mshahara wake ili kusaidia wakali hao wa Laliga kupunguza mzigo wa mishahara klabuni. (ESPN)














