Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 10.06.2021:Georginio Wijnaldum, Hakimi, Benitez, Sterling, De Gea, White, Xhaka, Lingard

Chanzo cha picha, Getty Images
Georginio Wijnaldum amesaini mkataba wa miaka mitatu na Paris St-Germain baada ya kuondoka Liverpool kwa uhamisho wa bure.
Kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 30, aliamua kupinga kutia saini kandarasi mpya Anfield na kuhamia mji mkuu wa Ufaransa baada ya kuhusishwa na Barcelona.
"Ninajiunga na moja ya vikosi bora huko Uropa na ninataka kuleta hamu yangu na kujitolea kwa mradi huu wa kipekee ," Wijnaldum alisema.
Wijnaldum alijiunga na Liverpool akitokea Newcastle United kwa pauni milioni 25 mwaka 2016.
PSG inaeleweka kutoa ofa nzuri kuliko Barca na uwepo wa meneja Mauricio Pochettino pia unafikiriwa kuwa sababu ya uamuzi wa Wijnaldum.

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kulia na nyuma wa Inter Milan na Morocco Achraf Hakimi,22 ambaye amekuwa akinyatiwa na Paris St-Germain. (Times, subscription required)
Kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anagombea nafasi ya ukufunzi iliyoachwa wazi Everton. (Mail)
Barcelona wanatafakari uwezekano wa kumnunua winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26, ambaye anaonekana kuwa mrithi mahiri wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele,24, ikiwa hatasaini mkataba mpya. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wanafanya mazungumzo na winga wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram - kabla ya kumsajili msimu huu wa joto . (RMC Sport - in French)
Kipa wa Uhispania David de Gea, 30, anatarajia kusalia Manchester United msimu ujao. (Sun)

Chanzo cha picha, Reuters
Arsenal wamejiunga na Liverpool, Tottenham na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlinzi wa Brighton na England Ben White, 23. (Mirror)
Roma wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 28, kutoka Arsenal. (Corriere dello Sport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa RB Leipzig raia wa Austria Marcel Sabitzer, 27,ambaye awali alihusishwa na tetesi za kuhamia Tottenham, anataka kuondoka klabu hiyo ya Bundesliga na huenda akanunuliwa kwa karibu euro milioni 15 msimu huu. (Athletic, subscription required)
Burnley wamefikia mkataba mpya na kocha wao Sean Dyche, 49, ambaye anatarajiwa kurejea dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu huu. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wameongeza juhudi za kumsajili Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu kutoka Manchester United baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza kutemwa katika kikosi michuano ya Ulaya. (Sun)
Porto wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Liverpool na Serbia Marko Grujic baada ya kuwa katika klabu hiyo msimu uliopita kwa mkopo. Porto hata hivyo inakabiliwa na upinzani kutoka klabu za Ujerumani na Italia ambazo pia zinawania saini ya nyota huyo wa miaka 25. (Athletic, subscription required)

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency
Leicester City wanamenyana na Wolfsburg na Lyon katika jaribio la kumsaini winga wa Bournemouth Mholanzi Arnaut Danjuma,24. (Voetbalzone - in Dutch)
Leeds United wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Fulham Harrison Reed, 26, msimu huu wa joto. (Mail)
Winga wa Newcastle Muingereza Jacob Murphy, 26, anatakiwa na Galatasaray. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Roma Jose Mourinho amewasiliana na mshambulizi wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27, ambaye anaongoza orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili. (Goal - in Italian)
Mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos, 35, ana matumani ya kuanza mazungumzo ya mkataba na Real Madrid na yuko tayari kuongeza mkataba wake wa sasa. (AS)

Chanzo cha picha, Getty Images
Deportivo Alaves wanataka kusaini mpya mkataba wa mkopo wa winga wa Manchester United na Uruguay Facundo Pellistri,19. (Noticias de Alava - in Spanish)














