Martha Koome: Mfahamu Jaji mkuu wa kwanza mwanamke Kenya

Chanzo cha picha, JUDICIAL SERVICE COMMISSION/TWITTER
Jaji Mkuu mpya wa Kenya Martha Koome ameapishwa rasmi mchana wa leo kuanza kazi ya ukuu wa wa idara ya mahakama na rais wa mahakama ya juu zaidi nchini Kenya.
Bi Koome anaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo nchini Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla hiyo ya uapisho. Jaji Koome amekula kiapo cha utekelezaji wa kazi yake kwa uadilifu katika Ikulu ya Nairobi. Kiapo hicho kilisimamiwa na Msajili Mkuu wa Mahakama Anne Amadi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Akizungumza baada ya kuapishwa kwa jaji mkuu Rais Kenyatta amesema imekuwa furaha yake kuwa rais wa kwanza kumuapisha Jaji Mkuu mpya wa kwanza mwanamke nchini humo.
Majukumu mazito yanayomngoja
Uthibitishwaji wake umekwenda haraka bila pingamizi toka alipoteuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Katika siku ambayo bunge liliidhinisha uteuzi wake, Rais Kenyatta alitumia muda wa chini ya saa tano kuufanya rasmi uteuzi huo ili kumfanya aanze kazi. Hata hivyo ana mengi ambayo yanamkodolea macho na wengi wanangoja kwa hamu kuona jinsi atakavyoyashughulikaia.
Baadhi ya mambo hayo ni kulinda uhuru wa mahakama ambao sasa umeonekana kutishiwa kufuatia uamuzi wa majaji kwamba mchakato wa kuirekebisha katiba kupitia Jopo la Maridhiano(BBI) ulikiuka sheria na ni kinyume na katiba . Pia kuna hofu kwamba uhuru wa idara ya mahakama utakuwa hatarini endapo afisi nyingine ya kudhibiti shughuli za mahakama itaundwa kama ilivyopendekezwa.
Kikubwa hata hivyo anapoanza kazi yake ni uteuzi wa jopo la majaji ambao watasikiza kesi ya rufaa iliyowasilishwana serikali kupinga uamuzi wa majaji wa mahakama kuu waliotupilia mbali mchakato mzima wa BBI.
Hilo ni suala kikubwa kisiasa nchini Kenya na Koome atahitaji ustaarabu wa kuweza kulikwea kwani kesi hiyo ina uwezo mkubwa w hata kufikishwa mbele ya mahakama ya juu zaidi ambayo yeye ndiye rais wa korti hiyo.

Chanzo cha picha, JUDICIAL SERVICE COMMISSION
Lakini je Martha Koome ni nani haswa?
Jaji Martha Koome alizaliwa katika Kijiji cha Kithiu, katika kaunti ya Meru 1960.
Jaji Koome baadaye alisomea shahada ya sheria katika Chuo kikuu cha Nairobi ambapo alifuzu 1986 na na kujiunga na chuo cha mafunzo ya Sheria nchini Kenya mwaka uliofuata.
Alianzisha Ofisi yake ya huduma za uanasheria 1988, na baadaye akajiunga na Huduma ya mahakama 2003 na kuhudumu katika mahakama tofauti kote nchini, wakati ambapo pia alihudumu kama mwanachama wa chama cha wanasheria nchini Kenya LSK.
Baadaye alijiunga na Chuo kikuu cha London ambapo alisomea shahada ya uzamili kuhusu sheria ambapo alifuzu na kupata cheti cha Sheria ya Umma ya kimataifa 2010 .
Mwaka 2011 , alipandishwa cheo na kuwa jaji wa mahakama ya rufaa na mwezi Septemba mwaka huohuo, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Muungano wa Mahakimu na Majaji nchini Kenya. Jaji Koome , katika kipindi chake cha miongo mitatu amekuwa mtetezi wa haki za wanawake na ustawi wa Watoto.
Kuna wakati mmoja alihudumu kama mwenyekiti wa baraza la kitaifa la Jopo Maalum kuhusu usimamizi wa haki za watoto ambapo alisaidia katika kufanyia marekebisho sheria ya Watoto.
Hatua hiyo pamoja na nyenginezo kuhusu ustawi wa Watoto mwaka uliopita ilimsaidia kuwa nafasi ya pili miongoni mwa watu muhimu wa mwaka 2020 nchini Kenya taji linalotolewa na Umoja wa mtaifa.
Alinukuliwa akisema: Watoto hawana sauti , hivyobasi niliamua kuwazungumzia kwasababu natambua kwamba wao ni daraja la siku za usoni na iwapo hatutawalea vizuri , siku zetu zijazo zitakuwa hatarini. Natambua kwamba watoto wapo katika mazingira magumu kutokana na umri wao mdogo.
''Pia Natmbua iwapo wanazozana na sheria ama iwapo ni waathiriwa wa makosa, ni kutokana na kufeli kwa mfumo uliopo'alisema.
Jamii na familia zimeshindwa kulinda watoto.
Jaji Koome ni mama wa watoto watatu.













