Super League: Ivory Coast ndio itakayoathiriwa zaidi iwapo marufuku ya Fifa itathibitishwa

Serge Aurier (left) and Nicolas Pepe are two Ivorian regulars who could face being banned
Maelezo ya picha, Serge Aurier (Kushoto) na Nicolas Pepe ni raia wawili wa Ivory Coast ambao huenda wakapigwa marufuku kushiriki mechi za kombe la dunia

Ivory Coast ndio timu ya Afrika itakayoathiriwa ikiwa wachezaji wa Ligi mpya ya Ulaya inayopendekezwa (ESL) watapigwa marufuku kucheza soka ya kimataifa.

The Elephants wana wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza katika vilabu ambavyo vimesema vinataka kushiriki katika ligi mpya ya ESL - Serge Aurier akiwa Tottenham; Nicolas Pepe wa Arsenal; Franck Kessie wa AC Milan; na wachezaji wa Manchester United Eric Bailly na Amad Diallo.

Mohamed Salah wa Misri, Riyad Mahrez wa Algeria na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon pia watakosa mechi hizo ikiwa shirikisho la soka duniani Fifa litatekeleza onyo yake ya hapo awali kwamba wachezaji wote watakaojitokeza kwenye ESL watapigwa marufuku kwenye mashindano ya kimataifa kama Kombe la Dunia.

Kama ilivyo sasa jumla ya timu 13 za Afrika zitawapoteza wachezaji wake

Kufikia sasa vilabu 12 bora barani Ulaya vimekubali kujiunga na ESL, zikijumuisha sita kutoka Ligi Kuu ya England - Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham.

vilabu hivyo vya Ligi Kuu vitajiunga na AC Milan, Atletico Madrid, Barcelona, Inter Milan, Juventus na Real Madrid.

Liverpool's iconic African front two would both be out

Senegal inaweza kupoteza wachezaji watatu -mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, kipa wa kwanza Edouard Mendy wa Chelsea, na Moussa Wague - wa Barcelona, ingawa kwa sasa anaichezea kwa mkopo PAOK Salonika ya Uigiriki.

Liverpool:

  • Mohamed Salah - Misri
  • Sadio Mane - Senegal
  • Naby Keita - Guinea
  • Joel Matip - Cameroon
  • (Taiwo Awoniyi - Nigeria - kwa mkopo Union Berlin)

Chelsea:

  • Edouard Mendy - Senegal
  • Hakim Ziyech - Morocco
  • (Baba Rahman - Ghana - kwa mkopo PAOK Salonika)
  • (Victor Moses - Nigeria - kwa mkopo Spartak Moscow)

Manchester City:

  • Riyad Mahrez - Algeria

Manchester United:

  • Eric Bailly - Ivory Coast
  • Amad Diallo - Ivory Coast

Tottenham Hotspur:

  • Serge Aurier - Ivory Coast

Arsenal:

  • Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon
  • Thomas Partey - Ghana
  • Nicolas Pepe - Ivory Coast
  • Mohamed El Neny - Egypt

AC Milan:

  • Ismael Bennacer - Algeria
  • Franck Kessie - Ivory Coast

Atletico Madrid:

  • Geoffrey Kondogbia - Central African Republic

Barcelona:

  • (Moussa Wague - Senegal - kwa mkopo PAOK Salonika)

Inter Milan:

  • Achraf Hakimi - Morocco

Juventus:

  • Hamza Rafia - Tunisia (Katika kikosi cha chipukizi cha Juve)

Real Madrid:

  • Hakuna