Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.12.2019: McTominay, Solskjaer, Eriksen, Emery

Mkufunzi wa Man UNited Ole Gunnar Solskjaer amehakikishiwa kazi yake Old Trafford
Maelezo ya picha, Mkufunzi wa Man UNited Ole Gunnar Solskjaer amehakikishiwa kazi yake Old Trafford

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameambiwa kwamba kazi yake ipo salama na mmiliki wa klabu hiyo na kwamba hawatamuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino.. (Mail)

Manchester United wana mpango wa kumpatia kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 23 Scott McTominay mkataba mpya wa £60,000 kwa wiki . (Sun)

Everton iliwasiliiana na mkufunzi wa zamani wa Arsenal Unai Emery kuhusu pengo la mkufunzi katika klabu hiyo ya Goodison Park. (Sky Sports)

Aliyekuwa mkufunzi wa zamani Arsenal Unai Emery atafutwa na Everton kuijza pengo la kocha mkuu
Maelezo ya picha, Aliyekuwa mkufunzi wa zamani Arsenal Unai Emery atafutwa na Everton kuijza pengo la kocha mkuu

Manchester United imeendeleza lengo la la muda mrefu la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham Hotspur Christian Eriksen, 27, mwezi Januari ,lakini inakabiliwa na upinzani kwa saini ya raia huyo wa Denmark.. (90min)

Rasi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kwamba mlango upo wazi kila mara iwapo mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atahitaji kurudi katika klabu hiyo.. (La Repubblica, via Goal)

Arsenal inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Inter Milan na Juventus kwa saini ya beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Roma. (Mirror)

Arsenal inamsaka beki wa Man United Chris Smalling ambaye yuko katika klabu ya Roma kwa Mkopo
Maelezo ya picha, Arsenal inamsaka beki wa Man United Chris Smalling ambaye yuko katika klabu ya Roma kwa Mkopo

Newcastle na Bournemouth zinamchunguza mshambuliaji wa Hull City mwenye umri wa miaka 22 Jarrod Bowen. (90min)

Bologna wamewasiliana na klabu mbili za ligi ya Premia kuhusu mshambulaiji wa Wolves raia wa Itali Patrick Cutrone, 21, na mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean. (Le Repubblica - in Italian)

Mkurugenzi wa Bologna Walter Sabatini amesema hakuna uwezekano wowote wa kumsaini Zlatan Ibrahimovic baada ya kufichua kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 raia wa Sweden ameamua kule atakakohamia . (Mail)

Mkurugenzi wa Bologna Walter Sabatini amesema hakuna uwezekano wowote wa kumsaini Zlatan Ibrahimovic
Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa Bologna Walter Sabatini amesema hakuna uwezekano wowote wa kumsaini Zlatan Ibrahimovic

Mkufunzi wa klabu ya Dalian Yifang Rafael Benitez amesema haoni sababu ya kurudi katika kuifunza klabu ya Ligi ya Premia kwa sasa .{Sky Sports)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard ana wasiwasi kuhusu kuanzisha matumizi mwezi Januari baada ya marufuku ya timu hiyo kuondolewa. (Evening Standard)

Rais wa Besiktas Ahmet Nur Cebi amesema kwamba hakuna uwezekano kwa mshambuliaji wa Evertonna Uturuki Cenk Tosun, 28 kuhamia klabu hiyo. (Hayatta Besiktas Radio station, via Liverpool Echo)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

United Chris Smalling ameifungia Manchester United mabao 18 katika kipindi cha miaka 8 aliyojiunga na klabu hiyo

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, United Chris Smalling ameifungia Manchester United mabao 18 katika kipindi cha miaka 8 aliyojiunga na klabu hiyo

Arsenal inaongoza Everton na Leicester katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, muda wake wa mkopo Roma utakapomalizika. (Mirror)

Aston Villa bado inataka kumsaini Pedro mwezi Januari, huku winga huyo wa Uhispania wa miaka, 32, akiwa tayari kuondoka Chelsea. (Telegraph)

Juventus imempatia Erling Braut Haaland ofa ya mshahara wa euro milioni tatu sawa na(£2.5m) kwa mwaka baada ya kubaini kuwa mshambuliaji wa miaka 19 wa Red Bull Salzburg ana kipengee cha kuweza kuondoka kwa euro milioni 30 (£25.3m). (Corriere dello Sport - in Italian)

Erling Braut Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Juventus imempatia Erling Braut Haaland(kushoto) ofa ya mshahara wa euro milioni tatu sawa na(£2.5m) kwa mwaka

Naibu mkufunzi wa Manchester City Mikel Arteta sasa yuko katika orodha ya Arsenal watu watakaomrith Unai Emery baada ya Brendan Rodgers na mchezaji wa zamani wa Patrick Vieira kuonesha ishara ya kujiunga na Leicester na Nice. (Express)

Lakini Vieira anasema hhiyo haimaanishi kuwa hajalishwi na hali ilivyo katika uwanja wa Emirates Stadium. (Canal+, via Mail)

Na tetesi zinaarifu kuwa Vieira amewaambia marafiki zake kuwa kuchukua kazi ya Arsenal. (Daily Star)

Patrick Vieira na Thierry Henry

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Patrick Vieira na Thierry Henry walikuwa wachezaji wenza wa Arsenal na waliisaidia Ufaransa kushinda Kombe la dunia na mashindano ya Ulaya

Mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Niko Kovac pia anapania nafasi ya kazi Arsenal na anajiandaa kuhudhuria mechi ya ligi ya premia ya Gunners watakapokipiga dhidi ya West Ham siku ya Jumatatu . (Goal)

Licha ya tetesi zinazomhusisha na AC Milan, Bologna na Napoli, Zlatan Ibrahimovic, 38, huenda asirejee katika ligi kuu ya Italia maarufu Serie A baada ya kuondoka LA Galaxy, anasema ajenti wake Mino Raiola. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mkurugenzi wa soka wa AC Milan Frederic Massara anasema klabu yake inamsubiri Ibrahimovic kufanya maamuzi kuhusu hatua yake ya baadae. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Zlatan Ibrahimovic

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa soka wa AC Milan Frederic Massara anasema klabu yake inamsubiri Ibrahimovic kufanya maamuzi kuhusu hatua yake ya baadae

Wamiliki wa Paris St-Germain wanakaribia kupata sehemu ya umiliki wa Leeds ya thamani ya £120m itakayowawezesha kuchukua klabu hiyo ikiwa itafika ligi ya Primia. (Daily Star)

West Ham imewasiliana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kumrudisha kipa wa Jamhuri ya Ireland Darren Randolph, 32, katika klabu hiyo. (90min)

Inter Milan inataka kumsajili beki wa kulia kushoto wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, mwezi Januari. (Calciomercato - in Italian)

Tetesi Bora Jumapili

James Rodriguez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid iko tayari kumwachilia mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez

Real Madrid iko tayari kuwaachilia mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, na winga wa Wales Gareth Bale, 30, kama sehemu ya makubaliano ya kumpata kiungo wa kati wa Manchester United na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Eldesmarque via Sunday Express)

Naibu mkufunzi wa Manchester City Mikel Arteta atalazimika kupitia mchakato mrefu wa mahojiano ikiwa anataka kuwa meneja wa kudumu wa Arsenal. (Sunday Telegraph)

Mikel Arteta alianza kazi ya ukufunzi Manchester City mwaka 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mikel Arteta alianza jukumu la ukufunzi Manchester City mwaka 2016

Manchester City hawawezi kumsaini Jadon Sancho kutokana na kipengele walichoafikiana kama sehemu ya mkataba uliowawezesha kumuuza kwa klabu hiyo ya Ujerumani. Lakini mabingwa hao wa ligi ya Primia hawatakubali mpango wa kulipa ofa yoyote ya kumpata tena winga huyo. (Sunday Mirror)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 19, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari, licha ya tetesi zinayomhusisha na Manchester United. (Manchester Evening News)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amethibitisha kuwa Jadon Sancho, 19, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amethibitisha kuwa Jadon Sancho, 19, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari

Mkufunzi wa Barcelona Ernesto Valverde amedokeza kuwa kiungo wa kati Arturo Vidal huenda akajiunga na Manchester United. (Sunday Mirror)

Real Madrid lazima ikusanye £84m katika mauzo ya mwezi Januari ili kufikia sheria ya usawa wa malipo kwa wachezaji. (Sunday Mirror)

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kuwa anamtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32, asaini kandarasi ya kurefusha muda wake katika klabu hiyo. (Marca)

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lionel Messi, 32, kusaini kandarasi ya kurefusha muda wake Barcelona

Meneja Jose Mourinho anataka kumsaini beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral kujiunga na Tottenham, na tayari ameungana na Arsenal na Manchester United katika kinyang'anyiro cha usajili wa kiungo huyo wa miaka 21-. (Sun)