Tetesi za soka Ulaya Jumapili 04.08.2019: Coutinho, Sane, Pogba, Fernandes, Neres, Van de Beek, Neymar, Coutinho

Coutinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)

Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)

Mchezaji wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)

Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany - in German)

Winga wa Man City Leroy Sane

Sane anakabiliwa na uwezekano wa kupoteza £11m katika mshahara wake iwapo ataendelea kukataa kutia kandarasi mpya na Man City . (Sunday Mirror)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anapima uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco na beki wa Bournemouth Nathan Ake, 24. (Sunday Express)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco

Manchester United wamefanya mazungumzo ya kubadilishana wachezaji na Juventus ambapo mchezaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, na mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic wataelekea Old Trafford, huku naye mchezaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, akielekea Juventus. (Sunday Times - subscription required)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anataka kumsaini beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33 kwa mkopo wa miaka miwili. (Sun on Sunday)

Barcelona inajiandaa kuanza mazungumzo na PSG kuhusu kumununua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, back to La Liga. (Goal.com)

Neymar

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa manchester United ameambia klabu ya Sporting Lisbon kwamba anataka kujiunga na Tottenham. (Mail on Sunday)

Real Madrid wameafikia makubaliano na mchezaji mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uholanzi Donny van de Beek, lakini bado hawajakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo na klabu yake Ajax. (Marca)

Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anapanga kumnunua beki wa Norway Kristoffer Ajer, 21 kwa dau la £21m. (Star Sunday)

Barcelona wameafikia makubaliano na Real Betis kumsaijili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22 Junior Firpo kwa dau la £22m. (ESPN)

Junior Firipo

Chanzo cha picha, Getty Images

Burnley have joined Crystal Palace in the race to sign Real Betis' Spanish midfielder Victor Camarasa, 25, who spent last season on loan at Cardiff City. (Sky Sports)

Tottenham imejiandaa kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Ryan Sessegnon, 19, kutoka Fulham, lakini huenda ikamkosa kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 na Real Betis Giovani lo Celso kwa hatua hiyo. (Star Sunday)

Hatahivyo Spurs wanapigiwa upatu pamoja na Atletico Madrid kumsaini beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter, 25 kwa dau la £60m. (Bild, via 90min)

Beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter

Tottenham wako tayari kushinda na Roma pamoja na Juventus kumsajili beki wa kulia wa napoli na Albania Elseid Hysaj, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Chelsea msimu uliopita (Sunday Express)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anasema kuwa atamuomba mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kuongeza wachezaji zaidi kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho siku ya Alhamisi na anasema kwamba anamtaka mshambuliaji wa Uingereza Dwight Gayle, 28, kusalia katika klabu hiyo licha ya hamu kutoka klabu ya Leeds..(Newcastle Chronicle)

Leicester wameripotiwa kumlenga beki wa Getafe na Togo Djene Dakonam, 27, kujiunga na klabu hiyo ili kuchukua mahala pake beki wa Uingereza ambaye anataka kujhiunga na Man United Harry Maguire, 26. (Leicester Mercury)

Leicester wameripotiwa kumlenga beki wa Getafe na Togo Djene Dakonam,

Chelsea wako tauari kusikiliza ofa ya kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, na Uingereza Danny Drinkwater, 29. (Sunday Telegraph)

Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza Drinkwater anatakiwa na klabu ya Brighton kwa mkopo msimu huu. (Mail on Sunday)

Beki wa kushoto wa Celtic na Uskochi Kieran Tierney, 22, huenda akakosa hadi wiki nane kupitia jeraha na hivyobasi kumaliza hamu ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya £25m (Sun on Sunday)

Kierran Tierney

Mshambuliaji wa manchester City ambaye ni raia wa Ujerumani Lukas Nmecha, 20, atahudumu msimu 2019-20 kwa mkopo katika klabu ya Bundesliga ya bWolfsburg. (Manchester Evening News)

TETESI ZA SOKA JUMAMOSI

Manchester City wamekataa daul la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester City wamekataa daul la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane

Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 72 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya mshambuliaji wa Leroy Sane raia wa Ujerumani, mwenye umri wa miaka 23. (Metro)

City wanataka walipwe pauni milioni 137 kwa mauzo ya Sane ikiwa hatakuwa na haja ya kusaini mkataba wa kurefusha mkataba wake, unaomalizika Juni 2021. (Telegraph)

Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, na muwakilishi wake, na hivyo kuuweka hatarini mkataba na Juventus wa kubadilishana mchezaji wa safu ya mashambulizi Mbelgiji Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 26. (Independent)

Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala
Maelezo ya picha, Manchester United wanahangaika kufikia makubaliano na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala

Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo,mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph)

Mlizi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, ameachwa nje ya kikosi cha Leicester kitakachocheza mechi ya urafiki baina yao na Atalanta Ijumaa kutokana na hali ya sintohfahamu juu ya hali ya yake ya baadae na Foxes wanaotaka mkataba wa pauni milioni 90 ikiwa Manchester United wanasaini mkataba nae. (Telegraph)

Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80 na klabu hiyo inaweza kutumia zaidi ya pauni milioni 150 kwa ujumla kabla ya kipindi cha mwisho cha mchakato wa uhamisho kukamilika (Independent)

Manchester United ilikataa fursa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 Moise Kean, na kumruhusu mtaliano huyo kuwa huru kuhamia Everton. (90min)

Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80
Maelezo ya picha, Dau la sasa la Manchester United kwa ajili ya Maguire ni la thamani ya pauni milioni 80

Liverpool wanapima uwezekano wa kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Bordeaux na Guinea Francois Kamano na wako tayari kumgaramia kwa pauni milioni 20 kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Sun)

Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester City imeingia tena katika mazungumzo na Juventus juu ya kiungo wa safu ya nyuma kulia Mremo Joao Cancelo

Tottenham wanauangalia mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa mchezaji wa Real Beti -Giovani Lo Celso, mwneye umri wa miaka 23. (Evening Standard)

Betis wamekataa ofa kadhaa kutoka kwa Tottenham kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Lo Celso. (SevillaABC - in Spanish)

Kiungo wa kati- nyuma wa Argentina Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo.(Sun)

Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nicolas Otamendi, mwenye umri wa miaka 31, anataka kuendelea kuwepo Manchester City licha ya kuhusishwa na taarifa za kuihama klabu hiyo

Newcastle wanakaribia kusaini mkataba na winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin,mwenye umri wa miaka 22, kutoka Nice katika mkataba wa pauni milioni 16.5 . (Talksport)

Mchezaji wa safu ya nyuma-kushoto wa Brazil Dani Alves anakaribia kuhamia Sao Paulo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36- yuko huru baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Goal)

Crystal Palace wamefany amawasiliano na Cardiff City kumuhusu kiungo wa kati wa Real Betis Muhispania Victor Camarasa mwenye umri wa miaka 25