Mwanafunzi aliyefariki Madagascar kwa 'kufungua mlango wa ndege '

Alana Cutland alikuwa akisomea masomo ya sayansi ya mazingira katika chuo cha Robinson College

Chanzo cha picha, FAMILIA YA CUTLAND

Maelezo ya picha, Alana Cutland alikuwa akisomea masomo ya sayansi ya mazingira katika chuo cha Robinson College

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Cambridge alianguk na kufa nchini Madagascar baada ya kufungua mlango wa ndege ndogo ikiwa angani, wamesema polisi.

Alana Cutland, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Milton Keynes - Buckinghamshire, nchini Uingereza alifariki dunia wiki iliyopita, kulingana na taarifa iliyothibitishwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza.

Polisi katika kisiwa hicho cha Afrika wamesema haijabainika wazi ni kwanini alifungua mlango wa ndege hiyo ndogo ilipokuwa angani. Dhana moja ambayo inachunguzwa ni kwamba huenda alipata athari mbaya za dawa za kutibu ugonjwa wa malaria.

Familia yake inasema imesikitishwa sana na kifo cha binti yao abaye walimta kama "msichana mwenye akili, na huru ".

Jafisambatra Ravoavy, ambaye ana cheo cha kanali katika polisi ya Madagascal, amemthibitishia mwandishi wa BBC kuwa Bi Cutland alifungua mlango wa ndege baada ya ya ndege hiyo kupaa angani kutoka kwenye eneo uwanja wa ndege uliopo eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi , kaskazini mwa Madagascar, tarehe 25 Julai.

Alikuwa akisomea masomo ya sayansi ya mazingira katika chuo cha Robinson College na alikuwa kisiwani humo kupata uzowefu wa kazi.

Chanzo cha kifo chake bado hakijathibitishwa na mamlaka za Uingereza.

Polisi wanatumia helicopta na barabara kuusaka mwili wake.

Alana Cutland alikuwa kisiwani humo kupata uzowefu wa kazi

Chanzo cha picha, FAMILIA YA CUTLAND

Maelezo ya picha, Alana Cutland alikuwa kisiwani humo kupata uzowefu wa kazi

Katika taarifa, familia yake ilisema kuwa alikuwa ni msichana mwenye kibaji cha kudensi, akiwa ni mtu anayependa kujifunza mambo mapya "ambaye alitoa nuru kwa kila chumba alichoingia ,na kuwafanya watu watabasamu kw akuwa kwake tu pale ".

"alikuwa mkarimu kila wakati na mtu aliyeisaidia familia na marafiki zake , jambo ambalo lilimfanya ajenge urafiki na watu wa aina mbali mbali maishani mwake, ambao tunafahamu fika watamkosa sana," walisema.

Dr David Woodman, kutoka chuo cha Robinson College, amesema kuwa "walishitushwa sana na taarifa ya kifo cha Alana " na wanatuma salamu zao za rambirambi kwa familia yake.

"katika kipindi cha miaka yake miwili hapa shuleni, alitoa mchango mkubwa sana katika mambo mbali mbali za kimaisha katika chuo hiki - tutamkosa sana sote ," alisema.

Madagascar ni kisiwa kilichopo kwenye mwambao wa kusini mashariki mwa Africa, ambacho ni maarufu kwa mbuga za kipekee za wanyamapori.