Nicolas Pepe: Arsenal imemsaini winga wa Lille kwa dau lililovunja rekodi la klabu hiyo

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wamemsaini winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutoka Lille kwa dau lililovunja rekodi la timu hiyo la £72m.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alitia saini kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa Emirates baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya Jumanne.
Pepe alifunga magoli 35 katika mechi 71 za ligi ya Ufaransa akiichezea Lille baada ya kujiunga kutoka klabu ya Angers 2017.
''Kuwa hapa na kuandikiksha mkataba na klabu hii kubwa ni baraka kwangu''.
Amekuwa mchezaji wa nne aliye ghali katika historia ya ligi ya Premia baada ya wachezaji wawili wa Man United Paul Pogba £89m na Romelu Lukaku £75m na beki wa Liverpool Virgil van Dijk £75m.
Pepe aliongezea: Ilikuwa muhimu kufanya uamuzi ulio sawa na nimeshawishika kwamba Arsenal ni chaguo bora.
Wakati wa msimu wa 2018-19 katika Ligue 1 ni mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe aliyekuwa na mabao mengi na usaidizi zaidi ya Pepe, ambaye atavalia jezi nambari 19 ya Arsenal.
''Nicolas ni mchezaji aliye na haiba ya juu na mwenye talanta ambaye alikuwa akisakwa na timu nyingi za Ulaya'' , alisema mkufunzi wa Gunners Unai Emery.
Kumsajili winga mwenye haiba ya juu limekuwa lengo letu katika dirisha hili la uhamisho na sasa nafurahi anajiunga nasi ataongeza kasi, nguvu na ujuzi kwa lengo la kupata magoli mengi katika timu yetu.
Mass turnover at Lille?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pepe alikuwa mchezaji wa pili kuthibitishwa kuondoka Lille siku ya Alhamisi huku mchezaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 21 rafael Leao akijiunga na AC Milan mapema siku ya Akhamisi kwa dau la £27
Hiyo inamaanisha kwamba Lille imejipatia kitita cha £135m kutoka kwa wachezaji wakati wa dirisha la uhamisho huku Thiago Mendes na Yousouf Kone akijiunga na Lyon kwa dau la £19.8m na £8.1m mtawalia huku naye Anwar El Ghazi akiandikisha mkataba wa kudumu katika klabu ya Aston Villa kwa dau la £8.1m baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.
Ikilinganishwa wametumia £42.4m kwa kuwanunua wachezaji msimu huu huku mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen akijiunga kutoka klaby ya Ubelgiji ya RSC Charleroi kwa dau la £10.8m.
Lille ilimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita katika ligi ya daraja la kwanza ikiwa na pointi 16 nyuma ya PSG.m.












