Harry Maguire: Anatosha kujiunga na Man Utd kwa £80m?

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka mitano iliyopita Harry Maguire alikuwa akicheza soka ya ligi ya daraja la kwanza na sasa anakaribia kuwa mlinzi ghalizaidi duniani.
Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wake kwa kima cha £80m ili kumnyakua mchezaji huyo wa miaka 26 kutoka klabu ya Leicester City.
Lakini mchezo wake umefikia thamani ya pesa zitakazotolewa na Man U kumnunua?
BBC Michezo inaangazia safari yake ya soka.
'Mwanafunzi mzuri mara anatarajiwa kufikia upeo wa maisha yake'
Ukiambiwa utaje wanasoka bora duniani bila shaka utajipata ukiwataja wachezaji kama - Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanasifika katia safu ya mashambulizi huku umahiri wa Kevin de Bruyne wa kupanga mabao na kutoa pasi safi ukimfanya kuwa kiungo wa kati hodari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maguire, hata hivyo sio mmoja wa wachezaji tajika katika mchezo wa soka. Ukosefu wa kasi ni moja ya sababu ambazo zishawahi kumkosesha nafasi ya kujiunga na vilabu vingine.
Huddersfield wakati mmoja ilibadili nia ya kumsajili kwa £1m kwa sababu alionekana kuwa na kasi ya chini uwanjani.
Lakini Maguire amefanikiwa kufidia mapungufu hayo kwa kusoma kwa makini mkondo wa mchezo mechi ikiendelea.
"Ni mchezaji soka mwerevu sana," kocha wa zamani wa Sheffield United Micky Adams, ambaye alimsaidia kujiunga na soka ya ngazi ya juu mwaka 2011, aliiambia BBC Michezo.
"Alikuwa makini na alitaka sana kujifunza. Ni mwanafunzi mzuri na anafuatilia na kushika anachofunzwa kwa wepesi mno, hasa wakati wa mazoezi uwanjani."
Maguire alipewa nafasi ya kucheza soka ya ligi ya mabingwa na Adams akiwa na miaka 18, lakini uwezo wake uwanjani ulibainika mapema kabla ya hapo.
Mkurugenzi wa zamani wa chuo cha soka cha Sheffield United,Travis Binnion alifanya kazi na Maguire kutoka akiwa na miaka 16 na anasema alikuwa akijiamini kushinda miaka yake.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Alitaka kuwa mchezaji bora wakati wa mafunzo na kuimarisha mchezo wake kila uchao," alisema.
"Hakuwahi kuvunjika moyo kutokana na kasi yake, alitumia akili nyingi kukabiliana na hali hiyo. Alijiamini katika kiwango chochote alichopewa kucheza. Sishangai kumuona alipofika katika taaluma yake michezoni."
Ni wakati alipokuwa chuo cha mafuzo ya soka cha Sheffield United alipopata upinzani kutoka kwa- Paul Pogba.
Wachezaji hao wawili walikwa walihasimiana sana katika soka ya vijana.
Katika fainali ya ya mwaka 2011 ya kuwania taji la FA la vijana, Maguire alikuwa akichezea Blades na Pogba akichezea Manchester United.
Japo Sheffield United walishindwa, Maguire alionesha mchezo mzuri katika mechi hiyo iliyowashirikisha wachezaji kama vile Jesse Lingard na Ravel Morrison.
Kulingana na ripoti, aliyekuwa meneja wa Manchester United wakati huo Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa akitazama mechi hiyo baadae alimuita Maguire na kumwambia kuwa ana vigezo vyote vya kuwa mchezaji bora.

Chanzo cha picha, Reuters
Maguire alisubiri kwa muda kujiunga na ligi kuu ya Premia, alikini baadae Hull City ilimsajili mwaka 2014.
Kabla ya hapo aliiwakilisha Sheffield United kwa misimu mitatu katika ligi ya daraja.
Japoligi hiyo haikuwa na umaarufu wa kuwa na walinzi wakali Maguire umahiri wake katika safu ya ulinzi bila kubadili mkondo wa mchezo umeivuti Manchester United.
"Kile kinachomfanya apate sifa ya kuwa mchezaji wa kulipwa £80m ni mtindo wake wa mchezo wa kugawa pasi kwa ustadi," Michael Dawson, aliyecheza na Maguire Hull City, aliiambia BBC.
"Ana uwezo wa kutoa mpira nyuma na hapati changamoto kujitoa katika hali ngumu anapokabwa. Kigezo hicho kinamfanya kuwa mchezaji hodari."
Je ni mkali kuliko walinzi wa sasa wa Man Utd?
Manchester United haijawahi kupata mlinzi mkalikwa mika kadhaa inadaiwa tangu, Nemanja Vidic aondoke miaka mitano iliyopita.
Takwimu zinaashiria kuwa Maguire ataziba pengo hilo.
Msimu uliopita aliokoa mabao mengi dhidi ya Leister ikilinganishwa na walivyofanya mabeki waUnited - Victor Lindelof, Chris Smalling, Phil Jones na Eric Bailly.
, Inakadirikwa kuwa ,alishindia Leister makabiliano ya mpira wa kichwa mara moja katika kila dakika 22, vyema zaidi ya walivyofanya Lindelof na Jones (dakika 37 na 27 kila mmoja) na bora zaidi kuliko Bailly (dakika 49).
Smalling,hata hivyo alishinda katika vizuizi vya angani - mara moja kila baada ya dakika 20 msimu uliopita
Mchezo wake ukoje ukilinganishwa na nyota wengine wa Ulaya?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kawa pesa walizotumia, United wanaamini wamemsajili mlinzi atakaekabiliana na wachezaji nyota wa Ulaya, lakini takwimu za baadhi ya mabeki wa Ulaya zikilinganishwa zinasemaje?
Jedwali lifuatalo, Maguire ana uwezo mkubwa akilinganishwa na wachezaji mwingine na amedhibiti uwezo wa kuzuia mipira ya juu inayopigwa kwa kichwa.
Amefanya makosa machache yaliosababisha kufungwa mabao.
Maguire pia ni kiungo hatari akiamua kushambulia lango.
Tangu mwaka 2016 amechangia moja kwa moja mabao 13 ya Leicester - kufunga mabao saba na kusaidia ufungaji wa mabao sita.
Kati ya wachezaji wa fuatao, ni Sergio Ramos (17) aliyefunga mabao zaidi.
Kwa hiyo ... anatosha thamani ya kitita anachotolewa?
Maguire huenda asiwe mlinzi kamili lakini ana sifa zote za mchezaji anayetafutwa na United.












