Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 11.04.2019: Pogba, Bale, Mata, Saul, Hazard na wengine

Chanzo cha picha, Getty Images
Uhusiano kati ya Paul Pogba na meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer umeanza kuzorota, kiungo huyo wa miaka 26 huenda akahamia Real Madrid. (Le Parisien via AS)
United inapania kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24. (A Bola - in Portuguese)
Gareth Bale, 29, hayupo katika mpango wa Real Madrid msimu ujao, kuna tetesi kuwa klabu hiyo ya Uhispania itamruhusu kuchagua kalbu anayotaka kuhamia.
Tayari Manchester United na Bayern Munich wameonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo. (AS)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata, 30, bado hajafanya uamuzi kuhusu hatma ya yake ya siku zijazo Old Trafford.
Mchezaji huyo raia wa Uhispania tayari amepata ofa kutoka kwa vilabu kadhaa. (Manchester Evening News)
Manchester City, Manchester United na Barcelona zinapania kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uhispania Saul Niguez, 24. (Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, anaamini kuwa uhamisho wake kwenda Real Madrid ni ''sasa la sivyo aachane na mpango huu'' . (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uingereza Danny Drinkwater, 29, ameambiwa hana maisha Stamford Bridge chini ya ukufunzi wa Maurizio Sarri. (Guardian)
Liverpool inatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ajax Mbrazili David Neres, 22, huku mahasimu wao wakimnyatia kiungo huyo. (Mirror)
West Ham inaonngoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kulia na kushoto wa Liverpool Nathaniel Clyne, 28, ambaye kwa sasa yuko Bournemouth kwa mkopo. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Reuters
West Brom iko tayari kushauriana na meneja wa Preston Alex Neil kuwa meneja wao mpya. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Chelsea Mnigeria Kenneth Omeruo, 25, anataka kugeuza mkataba wake wa mkopo Leganes kuwa wa kudumu kabla ya mwisho wa msimu huu . (Brila)
Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anataka kumsajili mshambuliaji mkali kama Jamie Vardy, 32 atakaetoa ushindani mkali kwa washindani wao. (Leicester Mercury)
Tetesi Bora Jumatano
Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa thamani ya pauni milioni 78. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa zamni wa Chelsea mtaliano Antonio Conte, 49, yuko tayari kujiunga na Inter Milan kama meneja wao mpya - ikiwa klabu hiyo itamfanya kuwa meneja anaelipwa kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Serie A. (Mail)
Vilabu vya Arsenal na Tottenham vinawania kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan Croatia Ivan Perisic, 30. (Corriere dello Sport, via Sport Witness)












