Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.02.2019: Icardi, Neymar, Dybala, De Gea, Felix, Saiss, Pogba, Bin Salman
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26, ametaka kuhamia klabu yake ya zamani Juventus ikiwa miongoni mwa mipango ya kubadilishana na Douglas Costa, 28 anayetaka kuhamia Man United. (Tuttosport, via Star)
Chelsea wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na raia wa Argentina Mauro Icardi, 25, ambaye hivi majuzi alipokonywa wadhfa wa nahodha wa klabu hiyo baada ya Real Madrid kupunguza hamu yao ya kutaka kumsaini. (Sun)
Real inamlenga mshambuliaji wa PSG na Brazil mwenye umri wa miaka 27 Neymar mwisho wa msimu huu hatua ambayo huenda ikaharibu mipangilio ya uhamisho wa mshambuliaji nyota wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard.(Sunday Times - subscription required)
Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa Juventus na Argentina 25 Paulo Dybala na itaipatia klabu hiyo ya Serie A mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 25, katika makubaliano hayo. (Sunday Mirror)
United imejiandaa kumpatia kipa wao David de Gea, 28, kandarasi ya muda mrefu yenye thamani ya £90m - ikiwa ndio mshahara mkubwa katika historia ya soka ya Uingereza na wana matumaini kwamba kipa huyo wa Uhispania atatia saini kandarasi hiyo. (Sunday Times - subscription required)
Klabu ya Manchester United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lyons mwenye umri wa miaka 22-year-old Tanguy Ndombele huku mchezaji huyo pia akinyatiwa na Juventus. (Metro)
Na Manchester United inashindana na Paris St-Germain kumsajili kiungo mshambuliaji Joao Felix, 19, mwenye thamani ya ununuzi wa £105m kutoka Benfica. (Mirror)
Kipa wa Arsenal aliye kwa mkopo David Ospina, 30, anawania uhamisho wa Marekani Kusini , huku mchezaji huyo wa Colombia akiona uwezo wake wa kuichezea klabu hiyo ukiendelea kudidimia katika klabu ya Napoli tangu kurudi kwa kipa wa kwanza Alex Meret. (Goal)
Beki wa Roma raia wa Ugiriki Kostas Manolas, 27, ambaye anawaniwa na Arsenal na Manchester United, anataka kuongezwa £12.5m zaidi kwa kuondoa mkataba wa kuondoka kutoka kwa kandarasi yake. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Wolves Romain Saiss, 28, ananyatiwa na Atletico Madrid, huku klabu hiyo la La liga ikitaka kumnunua mchezaji huyo wa Morocco kucheza nchini Uhispania. (Lions de l'Atlas via Birmingham Live)
Arsenal inajiandaa kuwasilisha ombi kwa klabu ya Bayer Leverkusen kumnunua kiungo wa kati Kai Havertz, 19, iwapo Mesut Ozil ataamua kuondoka katika klabu hiyo ya The Gunners. (TalkSport)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, anaamini atajiunga na Barcelona mwisho wa msimu huu. (Le Parisien - in French)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 30, atachelewesha kuongoeza kandarasi yake na klabu hiyo ya Uhispania hadi mwisho wa msimu huu. (Marca)
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman ataimarisha ombi lake la £3.8bn ili kuinunua klabu ya Manchester United msimu ujao. (Sun)