Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tottenham,Madrid zashinda michezo yao ya klabu bingwa ulaya
Tottenham Hotspurs, wakiwa katika dimba lao la nyumbani Wembley, wamechomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund kutoka nchini Ujerumani.
Mkorea Heung-Min Son ndie aliyeanza kuwapatika Spurs, goli la kuongoza katika dakika ya 47 ya mchezo, beki Jan Vertonghen akaongeza goli la pili katika dakika ya 83.
Mshambuliaji raia wa Hispania Fernando Llorente, alihitimisha kazi kwa goli la tatu katika dakika ya 86.
Nao mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid, wakiwa ugenini nchini Uholanzi katika dimba Johan Cruijff Arena, wametakata kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ajax.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 60, Ajax walichomoa goli hilo kupitia kwa Hakim Ziyech katika dakika ya 75,
Zikisalia dakika tatu mchezo kumalizika Marco Asensio, alifunga goli la pili na la ushindi kwa Real Madrid.
Michezo mingine ya michuano hiyo itaendelea wiki ijayo tarehe 19, Liverpool watakuwa wenyeji wa Bayern Munich, huku Lyon wakiwalika Fc Barcelona.
Tarehe 20, Atletico Madrid watacheza na Juventus, nao Schalke 04 wakiwapokea Manchester City.