Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 01.10.2018: Mourinho, Zidane, Sanchez, Foden, Sane, Ronaldo

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana hofu kuhusu hatma yake huko Old Trafford na anaamini kuwa maafisa wa klabu wamewasiliana na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane. (Sun)

Lakini mchezaji huyo wa zamani kimataifa wa Ufaransa analenga kuwa meneja mpya wa Juventus. (Tuttosport, via Daily Express)

Sintofahamu kuhusu hatma ya Mourinho huko United inamaanisha kuwa wachezaji 12 hawana uhakika kuhusu hatma yao wakati wanaingia mwaka wa mwesho wa mikataba yao. (Daily Mirror)

Mourinho amekosa uvumilivu kwa mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29. (London Evening Standard)

Mlinzi wa Manchester United raia wa England Luke Shaw, 23, anasema kikosi kilicheza vibaya wakati kilishindwa na West Ham siku ya Jumamosi. (Daily Telegraph)

Manchester City watangoja kabla ya kumpa ofa mpya kiungo wa kati mwenye miaka 18 Phil Foden ya mkataba mpya wa miaka mitano wa pauni 250,000 kwa wiki. (Daily Star)

Meneja wa City Pep Guardiola amemuonya wing'a mjerumani Leroy Sane, 22, akitaka asipoteze mwelekeo. (Sun)

Maajenti wa Manchester City, Liverpool na Tottenham walimtazama kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, wakati wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Genoa. (Daily Mirror)

AC Milan, Manchester United na Paris Saint-Germain walijaribu kumsaini Cristiano Ronaldo msimu huu kabla ya mreno huyo mwenye miaka 33 kujiunga na Juventus kutoka Real Madrid. (El Mundo, via Marca)

Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley atapeleka kikosi kizima na menaja Rafa Benitez kwa mlo katika jitihada za kujenga uhusiano. (Daily Mail)

Chelsea wanaamini kuwa hatua ya Maurizio Sarri kulenga usimamizi ni njia ya kuwashawishi Mbelgiji Eden Hazard na Mfaransa kiungo wa kati N'Golo Kante, 27 kusaini mikataba mipya. (Goal)

Usimamizi wa England umefurahishwa na kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 19. Rice ambaye ana mababu kutoka Ireland amecheza mara tatu kwa Jamhuri ya Ireland lakini anaweza kuhama. (Daily Mail)

Meneja wa Cardiff Neil Warnock alimsifu kipa wa Burnley Joe Hart kufuatia kushindwa kwa Cardiff kwa mabao 2-1 na Clarets siku ya Jumapili lakini akaongeza kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 31 asahau kuhusu kuitwa na England. (Lancashire Telegraph)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema anamuonea huruma mshambuliajiraia wa Misri Mohamed Salah na kuwa mchezaji huyo wa moaka 26 najitajhia kuwa katilka hali yake bora.

Bora Kutoka Jumapili

Manchester City wanataka kuvunja rekodi ya kununua wachezaji kwa kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19 kwa pauni milioni 200. (Sun on Sunday)

Manchester United wanaamini kuwa meneja Jose Mourinho anaweza kufutwa kazi mwishoni wa wiki ijayo huku wachezaji wakizungumzia uwezekano wake kufutwa walipokuwa wakirudi nyumbani baada ya kushindwa kwa mabao 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (Mail on Sunday)

Lakini United wanasema ripoti kuwa wamezungumza na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuchukua mahala pake Mourinho hazina msingi. (ESPN)

Mourinho alimkosoa mshambuliaji wa United Mchile Alexis Sanchez, 29, mbele ya wachezaji wenzake kabla ya kumtoa kutoka kwa kikosi kilichocheza Jumamosi. (Sunday Mirror)

Barcelona wanamtaka kiungo wa kati wa United Paul Pogba, ambaye aliambia wiki hii kuwa hawwezi kuwa nahodha wa Manchester United tena lakini wanaweza kumsaini mchezaji huyo wa miaka 25 msimu ujao badala ya mwezi Januari. (Sunday Express)

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 25, atauzwa kweda Juventus mwezi Januari. (Sun on Sunday)

Chelsea wanamfuatilia ndugu wa miaka 15 wa mshambuliaji Mbeljii Eden Hazard, 27, na kiungo wa kati Kylian, 23. Ethan Hazard anaichezea klabu ya Ubelgiji ya AFC Tubize. (Sunday Mirror)

Cristiano Ronaldo anaamini bao lake dhidi ya Juventus akiwa na Real Madrid lilikuwa bora zaidi kuliko la Mohammed Salah lililomshindia mshambuliji huyo wa Liverpool tuzo ya Fifa la Puskas Award. Lakini mreno huyo aliongeza kuwa Salah, 26 alistahli tuzo hiyo. (L'Equipe - in French)