Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paul Pogba na Jose Mourinho: Ipi hatma ya kiungo wakati wa Man United na mkufunzi wake?
Uhusiano kati ya Paul Pogba na mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ulionekana kugonga mwamba wiki hii.
Kanda ya video ya kiungo huyo wa kati na mkufunzi wake wakizozana katika uwanja wa mazoezi ilionekana siku ya Jumatano.
Je anelekea kuondoka katika klabu ya Man United ?
je kuna mtu anayeweza kumsajili ama atasalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ya mkufunzi wake?
Je Pogba anaweza kueleka wapi?
Juventus?
Klabu ya zamani ya Pogba Juventus, timu ya nyumbani Paris St-Germain na mabingwa wa ligi ya Uhispania Barcelona ni miongoni mwa klabu za Ulaya zinazohusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Lakini dau la juu la uhamisho wake huenda likawa kikwazo.
United iliilipa Juve wakati huo kitita kilichovunja rekodi cha £89m mwaka 2016 - lakini hiyo ni kabla ya uhamisho wa Neymar wa £200m kuelekea PSG kubadilisha soko la uhamisho .
Na malipo ya Pogba yanadaiwa kuwa £180,000 kwa wiki.
Mwandishi wa soka nchini Itali James Horncastle, ambaye alimuhoji Pogba wakati akiichezea Juve , hana uhakika iwapo klabu hiyo ya Serie A inaweza kumsajili baada ya kutumia £99m msimu huu kumnunua aliyekuwa mshambuliaji wa Real madrid Cristiano Ronaldo.
''Kumekuwa na ripoti katika kipindi cha siku chache zilizopita kwamba Pogba amekuwa akiwasiliana na wachezaji wenza wa zamani katka klabu ya Juventus'', alisema Horncastle.
''Baada ya juhudi za Juventus kumsajili Ronaldo , sio tu kwa fedha ilizotoa bali pia kuweka rekodi katika ligi ya Seria A, mbali na kumlipa Yuro 31m kwa mwaka, itakuwa vigumu sana kumsajili Pogba''.
'Huenda kukawa na mpango wa kutaka kumnunua , lakini itakuwa vigumu sana hata iwapo mkurugenzi mkuu katika klabu hiyo ya Juventus Beppe Marotta kusema hivi majuzi kwamba Pogba ni swala maalum'.
PSG?
Hali iliopo katika klabu ya PSG ni sawa. Uefa imeanzaisha uchunguzi kuhusu hali ya kifedha ya klabu hiyo ya Ufaransa na matumizi yake.
Msimu uliopita walimsajili mchezaji wa zamani wa Barcelona Neymar kwa dau lililovunja rekodi na kumuongeza kinda wa Monaco Kylian Mbappe katika makubaliano ya kumchukua kwa mkopo ambayo baadaye yalibadilika na kuwa makubaliano ya kudumu kwa dau la yuro 180m (£165.7m).
"Kwa kweli PSG ingemtaka Pogba. Ni mzaliwa wa Paris na ameishi katika mji huo'', alisema mwandishi wa Ufaransa Julien Laurens.
"Swala la kumrudisha nyumbani kama Mbappe linaweza kuwa la kuvuatia sana , kwa kuwa hawana viungo wa kati''.
"Hatahivyo kama Juventus , huku sheria ya Uefa kuhusu matumizi ikiwawekea vikwazo itakuwa vigumu sana sio tu uhamisho lakini pia mshahara.
Huenda ikawa gharama ya 20m euros (£17.9m) ama zaidi kwa mwaka.
"Sidhani kwamba wana fedha hizo , la sivypo Pogba asalie Man United kupita mwezi Januari naye Neymar akubali kwenda Real Madrid msimu ujao, ndipo kutakapokuwa na nafasi ya Pogba kujiunga na klabu hiyo. lakini mbali na hilo sioni akisajiliwa na PSG''
Barcelona?
Mwandishi wa Uhispania Guillem Balague anasema kuwa Barcelona huenda ina hamu ya kumsajili lakini inaogopa kuzungumza na ajenti wake , Mino Raiola.
Barca ina historia mbaya na Raiola, ambaye aliiikosoa klabu hiyo mara kadhaa baada ya kumuuza Zlatan Ibrahimovic baada ya mwaka mmoja
Raiola pia alidai kwamba alijaribu kumshambulia mkufunzi wa Barca Pep Guardiola baada ya fainali ya kombe la vilabu bingwa la 2011.
''Kuna ripoti nyingi zilizochapishwa zote zikimuhusu Mino Raiola ambaye anajaribu kuanzisha mjadala huu'', alisema Balague.
"Barcelona haijawasiliana na Pogba msimu huu na hawajawasilisha ombi lolote. Wamezungumzia kuhusu Pogba lakini huenda wakawa na hamu naye iwapo atakuwa anataka kuondoka.
"Wamezungumza na ajenti Jorge Mendes kuhusu wachezaji , licha ya kuwa amekuwa akihusishwa na Real Madrid hapo awali na watazungumza na Mino Raiola lakini wanamuona kama tatazo.
Wanajua kwamba kiwango cha fedha atakachoitisha wanajua hawatataka kulipa
Je Pogba atasalia Man United zaidi ya Mourinho?
Baadhi ya waandishi wanadhania kwamba Mourinho ataondoka Old Trafford kabla ya Pogba, ambaye alisajiliwa kwa shangwe na furaha wakati Mourinho alipoajiriwa.
Hornacastle alisema: Mojawapo ya sababu ambazo zilimfanya Pogba kuzozana na Mourinho ni kwamba anajua atasalia katika klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ya mkufunzi wake.
Kwa uwezo, Pogba anatambua kwamba yeye anaushawishi zaidi kwa mtazamo wa wapi klabu hiyo inahitaji, sio tu kupitia ufanisi uwanjani lakini pia kama kampuni ya burudani.
Pogba ana uwezo katika hilo zaidi ya Jose Mourinho.
Belague alisema: Mourinho ana mpango mbadala- iwapo hatafanikiwa anaweza kusema nilijaribu , kila mtu aliona nilijaribu lakini wachezaji hawakuweza kukumbatia mbinu zangu.
Je Mourinho anafaa kumchukulia vipi Pogba?
Pogba alianza msimu huu vizuri baada ya kuisaidia Ufaransa kushinda kombe la dunia nchini Urusi.
Uwanjani alianza vizuri akiweza kufunga magoli manne-ambayo ni thuluthi mbili ya mabao aliyofunga msimu ulioipita mbali na kutoa pasi moja iliosababisha bao.
Lakini Mourinho aliambia Pogba wiki hii kwamba hatowahi kuwa tena nahodha wa klabu hiyo , licha ya kutosema kwa nini alifanya uamuzi huo.
Kiungo huyo wa kati alisema kuwa klabu hiyo inafaa kushambulia , kushambulia, na kushambulia baada ya kupata sare ya 1-1 na klabu ya Wolves - lakini Mourinho amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wowote.
Mourinho sio lazima awe kama Didier Deschamps , alisema Laurens.
Deschamps alionyesha jinsi ya kumtumia Pogba , sio tu uwanjani lakini hata nje ya uwanja, ni rahisi sana.
Hivyo ndivyo walivyofanya wakufunzi Massimiliano Allegri na Antonio Conte wakiwa Juventus.
Alikuwa mchezaji mchanga wakati huo lakini sasa anahitaji kuona kwamba unamuhitaji na unamtegemea na kumuamini kuwa kiongozi.
Unahodha ulimuimarisha na lilionekana kuwa wazo zuri.
Lakini kumpokonya ulikuwa ujinga. Hajakuwa mchezaji mzuri zaidi katika klabu ya Man United lakini alikuwa na motisha baada ya kombe la duniani hivyobasi itakuwa aibu kutotegemea motisha kama hiyo.
Hivyobasi nashangazwa kumuona Mourinho akizozana naye sana huku Pogba akiwa na uhuru katika klabu hiyo kuimarisha kiwango chake cha mchezo.