Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 22.09.2018: Barcelona, Man United, Arsenal, Pogba, Giroud, Herrera, Rabiot, Walcott
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, alichunguzwa na maskauti wa Barcelona wakati wa mechi ya vilabu bingwa ya ushindi dhidi ya Young Boys. (Mundo Deportivo - in Spanish)
United inaongoza vilabu vya ligi ya Uingereza kurudisha tarehe ya mwisho ya uhamisho kuwa mwisho wa mwezi wa Agosti. (Mail)
Nyota wa Spurs Christian Eriksen, Toby Alderweireld na Danny Rose wanataka malipo yao kuongezwa ili kuwa sawa na yale ya Harry Kane ambaye analipwa kitita cha £200,000 kwa wiki. (Sun)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud analengwa na klabu ya Besiktas. Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 hana kandarasi katika klabu ya Chelsea msimu ujao . (Goal - in Turkish)
Kiungo wa kati wa klabu ya Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, yuko tayari kujiunga na Manchester City kwa uhamisho usiokuwa na malipo wakati kandarasi yake itakapokwisha mwisho wa msimu huu. (Metro)
Mkufunzi wa zamani wa Swansea Carlos Carvalhal anataka kupewa fursa nyengine katika kufunza katika ligi ya Uingereza.. (Times - subscription required)
Barcelona inajiandaa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29.
Mabingwa hao wa La Liga waliwasilisha ombi lao kwa raia huyo wa Uhipania , ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford inakamilika msimu ujao wakati wa siku ya mwisho wa dirisha la uhamisho.. (Sun)
Winga wa Everton na England Theo Walcott, 29, anasema kuwa alikuwa amepoteza hamu yake kucheza soka alipoondoka Arsenal mnamo mwezi Januari.(mirror)
Kipa wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 26 Bernd Leno, ambaye alisajiliwa na klabu hiyo kutoka klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen, anasema hafurahishwi kuwa mchezaji wa Akiba wa Czech mwenye umri wa miaka 36.(Evening Standard)
Mkufunzi wa klabu ya Fleetwood Town Joey Barton anasema kuwa anataka kuifunza Marseille siku moja .
Kiungo huyo wa kati wa zamani nchini kutoka Uingereza alihudumu msimu mmoja kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ufaransa kati ya mwaka 2012-13. (L'Equipe - in French)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez bado hajui atapatiwa kitita cha pesa ngapi kutumia kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Chronicle)
Kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets, 30, anatarajiwa kutia saini kandarasi ilioimarika katika klabu ya Barcelona katika kipindi cha wiki chache zijazo.. (ESPN)
Mshambuliaji wa zamani wa Monaco na Manchester United Radamel Falcao, 32, amewekewa sanamu yake katika mji wa nyumbani kwao huko Colombia.. (Mail)
Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Pedro, 31, anasema kuwa mbinu za mkufunzi Maurizio Sarri ni mabadiliko muhimu kutoka zile za mtangulizi wake Antonio Conte. (Mirror)
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa
Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 30, anasema hakuwa na mpango wa kuondoka stamford Bridge msimu huu licha ya vilabu vya Manchester United na Barcelona kuonyesha dalili ya kumsaini. (Express)
Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 20, anapata mafunzo zaidi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Manchester United Romelu Lukaku.
Meneja wa England Gareth Southgate amemtuma naibu wake Steve Holland kumtazama Jack Grealish wakati wa ushindi wa Aston Villa dhidi ya Rotherham siku ya Jumanne wakati anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 23. (Birmingham Mail)
Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 33, anasema itakuwa vigumu kwa mtoto wake wa umri wa miaka nane ambaye pia anaitwa Cristiano kucheza mpira kama yeye. Ronaldo Junior anaichezea Juventus Academy. (BeIn Sports, via Sun)
Totttenham wametupilia mbali madai kuwa uwanja wao mpya hautakuwa tayari ifakapo mwanzo wa mwaka 2019. (Sky Sports)
Mkuu mpya wa kandanda huko Arsenal Raul Sanllehi, anataka kumsaini wing'a raia wa Argentina Cristian Pavon, 22, kutoka Boca Juniors. (Football London)
Beki wa Manchester City Aymeric Laporte, 24, anasema ataendelea kuwepo kuichezea Ufaransa licha ya ripoti kuwa huenda anageuza uzalendo wake kwa Uhisania. (Manchester Evening News)
Mshambualiaji wa Liverpool Sadio Mane, 26, amemshauri Roberto Firmino kucheza dhidi ya Paris St-Germain licha ya jeraha lake la jicho.
Mshambuliaji huyo wa Brazil ambaye pia ana miaka 26 alitoka nje na kufunga bao la ushindi siku ya Jumanne. (Liverpool Echo)
Kiungo wa kati wa England James Milner, 32, anasema alipigwa marufuku ya kuvaa nguo nyekundu akiwa mtoto kwa sababu baba yake alikuwa anaichukia Manchester United. (FourFourTwo)
Kipa wa Arsenal Petr Cech, 36, anacheza kupata hatma yake kwa Gunners wakati yuko katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba huku akikabiliwa na ushindani kutoka kwa Mjerumania Bernd Leno, 26. (Evening Standard)
Mtoto wa wing'a wa zamani wa Manchester City, QPR na England Shaun Wright-Phillips, 36, alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza kablka ya mechi yao na Lyon. D'Margio Wright-Phillips, 16, pia yeye ni wing'a na anachezea kikosi cha City chini ya miaka 18. (Mail)
Bora Kutoka Jumatano
Manchester City bado hawajaanza mazungumzo ya mkataba na wing'a mwenye miaka 23 Raheem Sterling, lakini sasa wanataka kufanya mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba huo ambao utakamilika mwaka 2020. (Sun)
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametajwa k amamtu anayeweza kuwa mwenyekiti wa siku za usoni wa shirika linalosimamia Ligi ya Premia. Hilo lilifanyika wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni ya klabu za England. (Daily Mail)
Brighton wanataka kumteua mkurugenzi wa kiufudi wa FA Dan Ashworth katika nafasi sawa na hiyo kwenye klabu yao.
Mlinzi wa Leicester raia wa England mwenye miaka 25 Harry Maguire amekana ripoti kuwa wachezaji hawakufurahishwa baada ya wao kusafiri kwa magari badala ya ndege kwa mechi huko Bournemputh. (Leicester Mercury)
Afisa mmoja wa West Brom aliondoka klabu hiyo baada ya uamuzi wa kukosa kununuliwa Virgine van Dijk kutoka Celtic licha ya kumpendekeza. (Scottish Sun)