Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
UEFA: Manchester City yachapwa 2-1 na Lyon nyumbani Etihad, Man Utd washinda 3-0
Kampeni ya Manchester City kwenye mashindano ya Klabu bingwa barani Ulaya imeingia doa baada kuanza vibaya kama mabingwa watetezi wa ligi kuu England akipoteza mbele ya Lyon katika uwanja wa Etihad kwa kuchapwa 2-1.
Maxwel Cornet aliifungia Lyon goli la kwanza baada ya makosa ya Fabian Delph kushindwa kuutoa mpira nje baada ya krosi iliyopigwa na Fekir.
City ambao wanapewa kipaumbele cha kufanya vizuri kwenye Klabu bingwa walijikuta wakiongozwa kabla ya mapumziko, nahodha wa Lyon, Fekir alifunga goli la pili kwenye umbali wa mita 25 baada ya makossa kutoka kwa Fernandinho.
Bernardo Silva aliwapa matumaini City baada ya kufunga goli akisaidiwa na Leroy Sane, lakini wenyeji walikosa bahati ya kupata mabao, wakashindwa kuepuka kupoteza mchezo wao wa kwanza kwenye mashindano hayo makubwa Ulaya.
Matokeo kamili ya mechi za Jumatano
- Ajax 3-0 AEK Athens
- Shakhtar Donetsk 2-2 Hoffenheim
- Benfica0-2 Bayern Munich
- Man City 1-2 Lyon
- Real Madrid 3-0 Roma
- Viktoria Plzen 2-2 CSKA Moscow
- Valencia 0-2 Juventus
- Young Boys 0-3 Man Utd
Mchezo kundi F Shakhtar Donetsk dhidi ya Hoffenheim walitoa sare ya 2-2 katika mchezo uliochezwa kwenye nchi ya Ukraine mapema Jumatano na kufanya Manchester city kuwa timu ya mwisho kwenye kundi lao.
City ilionekana kama wangeendelea kutawala soka la Ulaya baada ya kufanikiwa kupata alama 100 katika msimu uliopita kwenye Ligi Kuu England.
Pamoja na majaribio kadhaa kutoka kwa beki Aymerici Laporte, Gabriel Jesus na Sergio Aguero walishindwa kupata magoli kutokana na ubora wa mlinda mlango wa Lyon, Anthony Lopes.
City ilionekana ikosa maelekezo muhimu kutoka kwa kocha mkuu Pep Guardiola kutokana na adhabu anayoitumikia.
Kocha wa Manchester city alikuwa anaushuhudia mchezo akiwa jukwaani akitumikia adhabu yake aliyoipata msimu uliopita katika hatua ya robo fainali dhidi ya Liverpool.
Kocha msaidizi Mikel Arteta ambaye pia ni kiungo wa zamani wa Arsenal alichukua majukumu ambayo hata hivyo yalionekana kumzidi.
Hata hivyo City watahitaji kupambana ili waweze kuja kuongoza kundi lao kama walivyofanya msimu uliopita.
Kikosi cha Guardiola kiliishia hatua ya nane bora msimamo uliopita na hakijawai kuvuka hatua hiyo.