Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 26.08.2018: Eriksen, Martial, Ramsey, Fekir, Abraham, De Gea

Paris St-Germain wako tayari kuipa Tottenham ofa ya pauni milioni 100 kwa kiungo wa kati wa Denmark mwenye miaka 26 Christian Eriksen. (Sunday Express)

Anthony Martial, 22, yuko tayari kusalia Manchester United baada ya kuvunjwa moyo kufuatia klabu yake kukataa kumuuza kuambatana na matakwa ya meneja Jose Mourinho. (Sunday Telegraph)

Na mshambuliaji Mfaransa Martial amasema atakuwa huko Old Trafford msimu mwingine baada ya kusaini mkatab wa miezi 12. (Sunday Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal wa Wales Aaron Ramsey, 27, anajiandaa kufuata mfano wa mcheaji mwenzake Mesut Ozil wa kusubiri hadi mwezi Januari kuwezesha klabu kushughulikia mkataba wake. (Mail on Sunday)

Klabu ya Ligue 1 ya Ufaransa Monaco inataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea raia wa England Ruben Loftus-Cheek, 22, kwa mkopo wa msimu nwote. (Sun on Sunday)

Chelsea wamekana ripoti kuwa mmiliki wake Roman Abramovich yuko tayari kuuza klabu hiyo. (Standard)

Matumani wa Real Madrid kumsaini mshambuliaji mfarana wa klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19, yatatokana na uchunguzi wa kifedha kwa upande wa Ufaransa. (AS - in Spanish)

Manchester United hawakufanya jitihada zozote za kumsaini beki mbelgiji Toby Alderweireld, 29, na beki raia wa England Danny Rose kutoka Tottenham msimu wa joto. (Sunday Mirror)

United wanaweza tena kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Roma raia wa Italia Lorenzo Pellegrini, 22, in January. (Sun)

Mshambuliaji Mbelgiji Eden Hazard, 27, angeweza kuondoka Chelsea kuelekea Real Madrid iwapo Zinedine Zidane angebaki kuisimamia klabu hiyo ya Uhispania. (Hiet Niewuwsblad - kupitia Talksport)

West Ham wanatathmini ofa za mikopo kutoka vilabu vya AZ Alkmaar cha Uhpolanzi na kile cha Uhispania cha Eibar kwa beki wa England mwenye miaka 19 Reece Oxford. (Mail on Sunday)

Leicester wanapanga kumwendea mshambuliaji wa safu ya kati wa Blackburn Muingereza Bradley Dack, 24, mwezi Januari. (Sun on Sunday)

Kipa wa Manchester United David de Gea, 27, hayuko tayari kusaini mkataba mpya na kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispani yuko na kipengee cha kuvunja mkataba wake sawa na kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba na raia wa Chile Alexis Sanchez huko Trafford. (Sunday Mail)

Borussia Dortmund wamekubaliana euro milioni 2.2 kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Paco Alcacer, 24, kwa mkopo wa msimu mmoja wakiwa na uamuzi wa kumnunua Mhispania huyo kwa kati ya euro milioni 20 na 25. (Bild - in German)

Mshambuliaji raia wa England Tammy Abraham, 20, atakataa ofa ya mkopo kwenda Aston Villa ili kupigania nafasi yake huko Chelsea. (Sunday Mirror)

Meneja wa New Castle Rafael Benitez anasema uwepo wake huko St James' Park hauna uhakika hadi baada ya mwezi Januari. (Newcastle Chronicle)ax. (Sport)