Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mkusanyiko wa habari muhimu za michezo: Fifa yampiga marufuku rais wa soka wa Palestina kutokana na matamshi ya Messi
Fifa yampiga marufuku rais wa soka wa Palestina kutokana na matamshi ya Messi
Fifa imempiga marufuku ya miezi 12 rais wa shirikisho la soka la Palestina baada ya uambia mashabiki kuchoma tishati za Messi na picha.
Jibril Rajoub pia amepigwa faini ya £15,826 kwa kuchochea chuki na ghasia huku taarifa hiyo ikitolewa kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Israel na Argentina.
Mechi hiyo ilitarajiwa kuchezwa mwezi Juni mjini Jerusalem lakini ikafutiliwa mbali.
Rajoub sasa hatosimamia mechi zozote katika kiwango chochote.
Mwez Juni , waziri wa maswala ya kigeni nchini Argentina Jorge faurie alikuwa amesema kuwa anaamini kwamba wachezaji wa taifa lake hawako tayari kucheza memchi dhidi ya Israel.
Mkufunzi wa Chelsea asema Hazard aondoki ng'o
Eden Hazard atasalia katika klabu ya Chelsea msimu huu na hatma ya Reuben Loftus Cheek itaangaziwa upya mwezi Disemba kulingana na mkufunzi Maurizio Sarri.
Hazard, 27, amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid na yeye na Loftus-Cheek hawajaanzishwa mechi yoyote msimu huu wa 2018-19.
Dirisha la uhamisho la Uhispania linafungwa 31 Agosti.
Sarri alisema: Siwezi kuuza bila bila ya kuwa na hakika ya kununua mchezaji mwengine wakati huohuo.
Hivyobasi nadhani kwamba Eden hazard atasalia nasi kwa msimu wote ujao.
Kiungo wa kati Loftus Cheek alikuwa katika kikosi cha Uingereza katika kombe la dunia baada ya kuonyesha umahiri wake katika klabu ya Cruystal palace ambapo yuko kwa mkopo msoimu uliopita
Kocha wa Arsenal amtaka Ramsey kusakata soka
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amemwambia Aaron Ramsey kucheza soka licha ya mazungumzo ya kandarasi yake yanayoendelea katika klabu hiyo.
Kandarasi ya Ramsey inakamilika msimu ujao lakini Emery amempatia changamoto kiungo huyo kuonyesha uwezo wake wa kuisaidia timu hiyo.
''Namtaka ajishughulishe na mazoezi, mechi na mchezo wake kila siku'', aliserma Emery.
Raia huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 27, aliwachwa nje katika kikosi cha kwanza dhidi ya Chelsea lakini huenda akarudi na kucheza dhidi ya West ham Jumamosi.
Alipoulizwa iwapo anaona Ramsey hana mwelekeo, Emery alijibu: Sijui, lakini tugange yaliopo.
Villa yamsaini winga wa Everton Bolasie
Winga wa Everton Yannick Bolasie amejiunga na klabu ya Aston Villa kwa mkopo wa muda mrefu
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Toffees kutoka Crystal Palace mwaka 2016 kwa dau la £25m katika kandarasi ya miaka mitano.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo alikuwa amehusishwa na uhamisho wa Middlesbrough.
"lengo langu kuu hapa ni kuhakikisha kuwa klabu hii inapanda ngazi. Klabu ya kiwango kama hiki inafaa kucheza katika ligi ya Premia'' , Bollasie aliambia tovuti ya klabu ya Aston Villa
"Nilitazama uwanja wa Villa Park na uwanja wa mazoezi, na mimi na familia yangu tukasema 'wow'. Kila mahali ni ligi ya Premier .
Kipa wa Tottenham ashtakiwa kwa kundesha gari akiwa mlevi
Nahodha wa klabu ya Tottenham Hugo Lloris ameshtakiwa kwa kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kusimamishwa na maafisa wa polisi magharibi mwa London.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 alisimamishwa na maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria mjini Gloucester mapema siku ya Ijumaa.
Lloris amekuwa katika klabu ya Spurs tangu ajiunge na Lyon 2012, akiichezea klabu hiyo ya Uingereza mara 256.
Raia huyo wa Ufaransa amemomba msamaha akisema na kisa ambacho hakiuwezi kukubalika kabisa.