Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mchezaji wa Brazil Somalia ajiunga na al-Shabab nchini Saudia
Somália amejiunga na al-shababa lakini sivyo unavyodhania.
Wergiton do Rosario Calmon, kwa jina maarufu Somalia ameichezea klabu ya Ufaransa ya Toulouse kwa takriban miaka mitatu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Brazil sasa amehamia katika klabu ya Al-Shabab nchini Saudia.
Huku ikiwa jina al-Shabab linalomaanisha Vijana kwa kiarabu sio jina baya , mitandao ya kijamii ilikuwa na haraka kulishirikisha jina hilo na kundi la kijihad mashariki mwa Afrika.
Kundi hilo linalohusishwa na lile la al-Qaeda limekuwa likipigana na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa ,muonhgo mmja uliopita na limetekeleza msururu wa mashambulizi katika eneo hilo.
Toulouse FC ilitangaza uhamisho huo na kumshukuru Somaliua kwa taaluma yake.
Kwa wengine ulinganifu huo haukuwafurahisha
Mchezaji huyo wa Brazil anaelekea Riyadh kwa kandarasi ya miaka miwili.