Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Arsenal yapata ushindi wa kwanza huku ManCity ikizuiwa na Wolveshampton
Arsenal ilirekodi ushindi wake wa kwanza katika ligi ya Premia chini ya mkufunzi mpya Unai Emery baada ya bao la kujifunga la Issa Diop na bao la dakika za lala salama la Danny Welbeck kuilaza West ham.
Arsenal ambayo imekuwa na safu ya ulinzi inayoyumbayumba ilitoka nyuma na kuongoza baada ya krosi ya Lacazette kumgonga Diop na kuingia.
Hector Bellerin baadaye alimuona Wellbeck ambaye alikuwa pekee katika lango la West Ham dakika za lala salama ambaye alicheka na wavu.
Nahodha wa West Ham Marko Arnautovic aliwaweka mbele wageni hao baada ya dakika 25, baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa felipe Anderson kabla ya kumfunga kipa Cech.
Nacho Monreal alisawazisha dakika tano baadaye kufuatia krosi ya Bellerin.
Wakati huohuo mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo alisema kuwa kikosi chake kilikuwa kikicheza kujifurahisha baada ya kuizuia manchester City katika uwanja wa Molineux huku kicxhwa cha Aymeric Laporte kikinusuru alama moja.
Kikosi hicho cha Guardiola kilikuwa kikishiriki katika mechi hyo baada ya kupata uhindi dhidi ya Arsenal mbali na Huddersfied.