Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia2018: Mambo muhimu unayofaa kujua robo fainali
Mechi moja mabao saba, Lukaku na Hazard kufufuka na kuitoa Japan, nayo Uingreza kushinda kwa penalti mara ya kwanza.
Kombe la Dunia la kuvutia zaidi nyakati hizi linaingia hatua ya robo fainali. Hapa tunaangazia tunayotarajia kwenye mechi nne zitakazoamua atakayeingia nusu fainali ikiwemo mfaransa anayeipenda Uruguay lakini hana budi kuwatema nje....
'Mfaransa mpenda Uruguay anayesaka kuwatoa marafiki zake'
Uruguay v Ufaransa (Ijumaa, 6 Julai - Nizhny Novgorod)
Ni Urafiki kando, kazi kwanza wakati straika wa Ufaransa Antoine Griezmann atacheza dhidi ya rafiki zake ambao ni walinzi wa Uruguay, Diego Godin na Jose Gimenez, wanaoitumikia klabu ya Atletico Madrid.
Baada ya Uruguay kujikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia, ni Griezmann ndiye alienda uwanja wa ndege wa Madrid kuwapokea wachezaji wake waliorejea, Godin na Gimenez, huku akiwa amevaa jezi ya Uruguay.
Griezmann amesema anahisi kuwa "Muuruguay wa kuchanganya".
"Ni uraia ninaoenzi, taifa linalopenda na mechi hii itakuwa ni ya hisia nyingi kwangu."
Kiungo wa Uruguay Nahitan Nandez, anungana na kauli za Griezmann.
"Griezmann ni Muuruguay, anajitambua kuwa hivyo. Kwake, itakuwa ni mechi spesheli kama tu ilivyo. Matumaini yetu ni kuwa atakumbuka yeye ni Muuruguay na kutotugeuka uwanjani!"
Antoine Griezmann
Lakini Luis Suarez, mfungaji wa Uruguay anayepiga timu ya Barcelona anapinga kauli hii.
"Ni mfaransa na hafahamu kuwa Muuruguay inamaanisha nini," alisema Suarez.
"Hatujui sisi ni kina nani au ni nini tunapaswa kufanya ili tufanikiwe kwenye soka.
Anajivunia tamaduni zetu, na anazungumza lugha sawa- lakini tunahisi namna tofauti."
Achia mbali mapenzi ya Atletico Madrid,mchuano unatarajiwa kuwa mkali na wa ajabu.
Mtaifa yote yamejihami kwa washambulizi matata ulimwengu wa soka na wote wamewaondoa mataifa tajika kwenye soka hatua ya mchujo.
Ufaransa inajigamba kuwa na watatu kati ya wachezaji watano ghali mno duniani punde tu uhamisho wa Kylian Mbappe wa euro milioni 180m (£159m) kutoka Monaco hadi Paris St-Germain utakapokamilishwa.
Mbappe alikuwa chipukizi wa kwanza kuyatandika magoli mawili tangu gwiji wa zamani wa Brazil, Pele, timu yake ya Ufaransa ilipowanyoa Lionel Messi na Argentina 4-3 mechi iliyopita.
Uruguay - iliyowakung'uta Ronaldo na Ureno - inajidai kwa kuwa na Suarez na Edinson Cavani ambaye ni mfungaji mwenye mabao Zaidi historia ya Paris St-Germain, kwenye safu ya ufungaji. Wawili hawa wana jumla ya mabao 98 ya kimataifa.
Ubelgiji kujutia kuizima Uingereza?
Brazil v Ubelgiji (Ijumaa, 6 Julai - Kazan)
Ubelgiji huenda inajutia kutua kwenye upande mgumu wa mechi zilizosalia Kombe hili kwa kunyakua nafasi ya kwanza kundi G.
Walitoka nyuma 2-0 na kuwalisha upanga Japan katika ngarambe kali Jumatatu - ilikuwa timu ya kwanza kuandikisha matokeo aina hiyo tangu 1970 - lakini wamezawidiwa kwa kukutanishwa dhidi ya timu inayopigiwa upatu kuinua Kombe mwaka huu na walioliinua mara tano kufikia sasa - Brazil.
Ingefungwa na Uingereza, Ubelgiji haingepata pingamizi kuinua kombe hilo la dhahabu tarehe 15 Julai.
Ubelgiji - isiyopoteza mechi 23 mpaka sasa - ndio moja kati ya timu mbele pekee Urusi kushinda mechi zake zote nne ilizocheza.
Wamefichua makali yao dhidi ya Japan na kuwanyamazisha wakosoaji wake waliotilia shaka uwezo wao wa kuwaangamiza wapinzani walipowadhalilisha Japan huku mlango wa kutokea ukiwakodelea macho na kutishia kuwanyima nafasi ya robo fainali.
"Tulipokuwa nyuma 2-0 dhidi ya Japan tulihisi kisaikolojia kuwa 'Sawa, hatuna la kupoteza',hilo lilituweka huru," alisema kocha wa Red Devils Roberto Martinez
"Hili tutalidumisha dhidi ya Brazil, ila tu hisia hizi zitakuwa kuanzia sekunde ya kwanza."
Huu ndio mchuano utakaoshuhudia wengi wa mastaa waliosalia Urusi Kufikia sasa - Barcelona, Chelsea, Liverpool, Manchester City na Paris St-Germain watawakilishwa na angalau mchezaji mmoja.
Neymar ni mmoja wa wachezaji wa kupendeza ngarambe hizi - Ingawa sio kwa kila jambo.
Amesajili mabao mawili Urusi - lakini sarakasi zake pindi anapoumia,zimemletea kejeli kutoka mashabiki.
Ingawa safu ya ushambulizi ya Brazil ndio imepokea sifa nyingi, mabeko wao pia wanastahili kongole kwani wamefungwa bao moja tu katika mechi tisa walizocheza. Aidha, katika Kombe la Dunia Urusi wameruhusu shuti tano tu kwenye lango lao.
Uingereza iliingia Kombe la Dunia na kikosi kipya, kisichobabaishwa na masaibu yake ya awali.
Wathibitisha haya walipoiondoa Colombia kwa matuta raundi ya mchujo - mara ya kwanza Three Lions kushinda kupitia mikwaju.
Msisimko wa Uingereza umeongezeka baada ya mwanya wa kuingia fainali kujitokeza kutokana na wapinzani 'dhaifu' wanaowasubiri- Sweden - Russia/Croatia.
Kambini Uingereza, wanafahamu wazi kuwa, ni fursa ya kipekee ya kuandikisha matokeo sawa na ya 1990 walipofika nusu fainali au ubingwa wao wa Kombe la Dunia 1966.
Hata hivyo meneja wa Uingereza Gareth Southgate anazungumza kwa makini.
"Hatujasali rekodi nzuri dhidi yao, tumekuwa tkiwadharau kila mara," Alisema.
Sweden hata licha ya kuwa bila mfungaji mahiri Zlatan Ibrahimovic, walimaliza mbele ya uholanzi mechi za kufuzu, kabla ya kuichuja Italia mechi ya mikondo miwili.
Walichangia kuporomoka kwa Ujerumani walipomaliza viongozi wa Kundi F.
Hilo liliwapa motisha na uwezo wa kuwatimua Uswizi raundi ya muondoano.
Uingereza na Sweden walitoka sare 2-2 mnamo 2006, Joe Cole akifunga zinga la kwaju.
Marudio ya matokeo aina hiyo huenda yakawapa 'magwiji wa mapenalti' Uingereza nafasi nyingine kupiga matuta.
Urusi v Croatia (Jumamosi, 7 Julai - Sochi)
Ni mkwaruzano kati ya Urusi, taifa kubwa zaidi duniani, na Croatia, taifa lenye watu milioni 4.1 - lakini la kuzalisha wachezji wenye vipaji na wasakataji hodari wa soka.
Croatia, kwa kuwa na Luka Modric na Ivan Rakitic, wamefarijika kuwa na viungo wawili wenye umuhimu mkubwa kwa vilabu vyao - Real Madrid na Barcelona.
Urusi, timu inayoorodheshwa nafasi za chini ndani ya Kombe la Dunia wanaloandaa,walianza safari bila kupewa motisha na mtu yeyote ndani na nje ya taifa lao.
Walivuma kutoka kundi rahisi, lakini pia wakawaduwaza mabingwa wa zamani wa dunia 2010, Uhispania kwa njia ya mikwaju hatua iliyotangulia.
Wanahitaji ushindi katika michuano miwili ijayo - dhidi ya Croatia na Sweden au Uingereza - kutua fainali.
Kwa upande wake, Croatia inashirik robo fainali kwa mara ya pili.
Mnamo 1998, miaka mitano baada ya kujitenga na Yugoslavia na kuwa mwanachama wa FIFA, walifika nusu fainali - na huenda wasipate nafasi nzuri ya kufika fainali kama ilivyo sasa.
Mfungaji wao Mario Mandzukic na mlinzi Vedran Corluka wamezidi miaka 30 huku winga wa Inter Milan Ivan Perisic akiwa na miaka 29.
Shujaa wa Croatia Davor Suker - mshindi wa kiatu cha dhahabu 1998 - ameiambia BBC:
"Itakuwa mechi ngumu dhidi ya Urusi. Walivyowafunga, Uhispania imependeza.
"Kwa Croatia, ni vizuri tumeshiriki mashindano 10 katika mashindano 12 iliyotangulia.
Sisi ni taifa lenye watu milioni nne unusu, kwa hivyo ni rekodi nzuri pamoja na viwango vya wachezaji tunaozalisha. Najivunia kuwa mmoja wao."
Fomu hii ya Urusi Kombe la Dunia ndio fomu yao bora katika historia yao Kombe la Dunia.
Hawajawahi kufuzu kwa hatua ya wakiwa taifa lililojitenga, lakini walifika nusu fainali 1966 wakiwa kwenye muungano wa USSR.